Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
Wametishwa na wametishika, maandamano ya leo yalikuwa yanasubiriwa na watu wote wapenda democrasia
 
mimi nilishapoteza imani na chadema siku nyingi sana. siku niliyojua mbowe kawauzia chadema magari ya mukutano (yale mafuso yenye majikwaa) na akaongeza cha juu. pia siku walipompa kadi lowasa na kumfanya mgombea wao nilikataa tama na siasa.
chadema=ccm=chadema=ccm. hawana tofauti. wanapinga udicteta wakati wao wanaukumbatia chamani.
 
Mtampiga vita NN
Lakini kawapa ushauri huu upinzani wa sasa umekatisha tamaa wengi

Hakuna agenda za kitaifa na nyeti za kuukuza upinzani na mkichelewa , JPM akianza kutekeleza ahadi zake moja baada ya nyingine mtapotea kabisa

Mnachotakiwa cdm , badilikeni

Zama zimebadilika
CDM ni jeshi kubwa sana
 
Huu mtego waliowekewa Chadema wangeingia mkenge ndio ungekuwa mwisho wao.

Watanzania tunaongoza kwa unafki, Nyani Ngabu yupo Marekani anataka wenzake wauwawe yeye abaki tu kwenye keyboard.

Nina imani kikao cha msajili kitapata ufumbuzi na mikutano itaruhusiwa kwa vyama vyote.

Malengo ya Chadema kisiasa yamefikiwa hakuna haja ya kutowa sadaka maisha ya watu na kusababishia ulemavu.
Kikao kimehairishwa indifinitely
 
CHADEMA Walitaka Publicity,na Wameipata!na Hata Kusema Kuwa Watumishi wa Mungu Kuwaomba Watulie Bado ni Kick Nzuri!
Na Mpaka Oktoba Mosi CHADEMA Haita Kauka Vinywani Mwenu!
Hivi Usafi Kesho Unaendelea,ahahaha!
CHADEMA Wametanguliza,wao Wamepiga Kona Fasta!
Utaona uvccm wakitumwa kufanya maandamano yao mwishoni mwa mwezi WA Tisa.
 
Chadema wamefanya kosa la kiufundi, walipaswa waendelee na Ukuta Leo hayo maridhiano yangekuja Mbele ya safari.
Mm siku nyingi sana sina Imani nao tena Ndg NN
 
Wapo ujue wamelishwa unga wa ndere.... Hawaoni na hawathubuti kuyakemea au kuyakosoa yanayofanyika ndani ya CDM wanaona tu ya wengine hawathubutu hata kumwambia Mbowe chochote evrything ndio mzee.....
 
Ndugu zangu CDM, msipozitafakari upya siasa zenu, kwa hakika baada ya muda mfupi tu chama chenu kinaweza kupotea kabisa na kubaki historia tu. Nawapenda sana ndugu zanguni CDM, lakini naomba mbadilishe mbinu za siasa. Achaneni na siasa za MAANDAMANO, MATUSI, KEJELI NA VURUGU zisizo na tija kwa wananchi. Jihusisheni na kutoa misaada kwa watu wenye shida mbalimbali, hakika mtakumbukwa na kupongezwa kwa dhati. Mtu hawezi kukukumbuka eti kwa sababu ulimsema vibaya kiongozi au kwa sababu uliitisha maandamano. Mtu atakukukumbuka kwa kumsaidia wakati wa shida. Mungu awabariki sana.
 
Chadema Saizi kinafaa kubaki makumbusho ya taifa
 
Wadau,

Nimehamasika kuweka hii kura baada ya Mdau mmoja Nyani Ngabu kuweka Uzi kua Imani yake (pengine na wengine) kwa CHADEMA imepotea baada ya CHADEMA Kuhairisha maandamno yao yaliyokua yafanyike tarehe 01/09/2016.

Post hiyo ipo humu Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Binafsi bado nina imani na CHADEMA, na hata pale baada ya kuhairishwa nahesabia kama CHADEMA imepata ushindi mkubwa sana kwa jinsi upande wa pili ulivyolichukulia hili swala serious na kujiandaa kukabiliana nalo. Nguvu iliyotumika kujaribu kuizima ni dhahiri kua dhamira ya UKUTA ilifanikiwa, ila kwa namna ingine.
 
Back
Top Bottom