Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Chadema hawajakurupuka.
Wamefanya kile kile walichokuwa wamedhamiria.
Kukoki watu kwa kuwahadaa na matamko ya operesheni hewa.
Ni hewa kwa sababu hakuna aliyekuwa na nia ya dhati ya kuandamana tangia mwanzo.
"A publicity stunt".
Ni kweli hawajakurupuka.

CHADEMA wamefanya kile kile walichokusudia, umenena wewe Jozi 1, nikiamini unaujua undani wa UKUTA.

Je, ni mafanikio gani ya "M4C"; "SANGARA"; Peoples Power!"; "mabadiliko lowasa - lowasa mabadiliko"; "UKUTA" na mengineyo ambazo ni baadhi ya kaulimbiu na operesheni za CHADEMA.

Kumbe huwa ni matamko, kaulimbiu na operesheni hewa. Tunashukuru wewe na wafuasi wa CHADEMA mnatambua hivyo. Basi CHADEMA ni chama cha siasa hewa, au viongozi ndiyo hewa, la wafuasi ni hewa.

Ni kweli hawakurupuka, ila kwa jamii iliyozungukwa na umaskini, katika nchi tajiri, uhewahewa wa aina hiyo unadhihirisha uwezo mdogo wa viongozi wa kisasa kuwatumikia.

Viongozi wa CHADEMA wajipange upya
 
Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.
Hili ndilo lililokuwa kosa la kiufundi ambalo litaendelea kuwagharimu siku zote.
 
Chama kikubwa cha siasa huwa hakina usaliti. Ukiona chama cha siasa kinazo tabia za kuzungukana na kusalitiana, basi hata kama kina umri wa miaka 100 bado ni kichanga sana kuweza kupewa dhamana ya kuongoza nchi.
Umenena kweli mkuu!
Mi nashangaa baadhi ya watu bado wanasema eti tukutane Octoba Mosi, huu sasa ni ujinga uliopindukia, kama wametumia zaidi ya miezi miwili wakituaminisha kwamba iwe mvua liwe jua kuandamana ni must, mwisho wa siku wapoleee, na wanakuja na matamko eti oooh unajua viongozi wa dini wametuasa, wachumia tumbo wakubwa
 
Mkuu freeland, CHADEMA needs to go back to the drawing board. Mashinji might be having qualities of a good leader but his boss misses some useful skills. Na muda wa kufanya mabadiliko ya juu kabisa bado upo, kuna miaka minne mpaka ufanyike uchaguzi wa 2020.

CHADEMA ni chama kizuri sana...Tatizo Mbowe amechoka hana fikra mpya za kutuvusha...kiukweli anapaswa kukaa pembeni
 
Anachokera zaidi ni ule uwezo wake wa kujenga spirit ya kiburi miongoni mwa watu wanaomuamini. Hana kabisa humility, hawezi kujishusha akawa katika level ya mtu wa kawaida. EL pamoja na kukejeliwa sana na viongozi wa juu wa chama tawala lakini bado alikwenda kwenye sherehe ya mzee BWM, that is what we call humility, that can only be found in a true leader, it comes from heart not mind.
FAM anakosa sifa za asili za kuwa kiongozi, kwani kuongoza ni zaidi ya kuendesha vikao vya chama na kuhutubia jukwaani, mtindo wako wa maisha pia ni sehemu muhimu wa sifa za uongozi.
 
Kaka tafuteni uongozi mpya kabla ya 2020. Huyu mkazi wa pale magogoni wa sasa hana muda wa kunywa na mtu chai pale Ikulu, vikao vyake na wageni huwa havidumu kwa zaidi ya dakika ishirini. Badilikeni, siasa za humu JF na kule FB zitawapatia umaarufu wa bei rahisi sana.

Huo ndiyo ukweli ulio wazi.

It seems Mbowe is a pain in your a.ss ndiyo maana unatumia nguvu kubwa kuhamasisha eti awekwe kando.
vikao vya Ikulu havidumu kwa ziadi ya dakika ishirini kwakuwa English ni tatizo.

Sina uhakika kama uko sawa kwa kutukuza English, lugha ambayo nina uhakika ni tatizo kwako. kumbe hujui lugha ya ya Taifa si 'English' au! Umesomea "english medium school"! Hongera kwa ujuha huo. Aibu.

Mbowe kweli ni mwiba mchungu kwenye mioyo ya wapenda amani na maendeleo, nchini. Alijidhirisha kama Kiongozi mwanamapinduzi kwa kauli zake za kuchukia maouvu katika jamii (rushwa, ufisadi, ubadhirifu) na utendaji mbovu (uzembe) wa watumishi wa serikali. Laiti angesimama kama mgombea Urais wakati huo, badala ya Slaa, naamini angeshinda.

Kwa sasa Mbowe kakosa mwelekeo, ila imedhihirika wazi kwamba kumbe ni mjasiriamali kisiasa. Amemkaribisha mtu ambaye chama chake kilimtuhumu ni fisadi papa, kwa sababu ya umaarufu wake kisiasa, ili apate majimbo mengi ya uchaguzi (ruzuku). Angalau hiyo ruzuku basi itumike kama mtaji wa kuweka vitega uchumi vya chama, ioi kiinuke kiuchumi na kuweza kujijenga zaidi, badala ya kuendesha operesheni za kujinufaisha binafsi na kikundi cha watu wachache kwenye chama.
 
Anachokera zaidi ni ule uwezo wake wa kujenga spirit ya kiburi miongoni mwa watu wanaomuamini. Hana kabisa humility, hawezi kujishusha akawa katika level ya mtu wa kawaida. EL pamoja na kukejeliwa sana na viongozi wa juu wa chama tawala lakini bado alikwenda kwenye sherehe ya mzee BWM, that is what we call humility, that can only be found in a true leader, it comes from heart not mind.
FAM anakosa sifa za asili za kuwa kiongozi, kwani kuongoza ni zaidi ya kuendesha vikao vya chama na kuhutubia jukwaani, mtindo wako wa maisha pia ni sehemu muhimu wa sifa za uongozi.

hapa naweza kutofautiana na wewe

Mbowe ni mjengaji mzuri sana wa hoja..Tatizo alilonalo yeye ni kuwa tayari ameshakuwa spent force....kama vile alivyo maalim seif,Lipumba,Zitto na wengineo

Hawana namna mpya tena ya kufanya mambo

Lowasa huyo mwache kando...ana maluweluwe yake mengi...kiufupi he is corrupt just like others
 
Ni kweli mkuu, kinahitajika kizazi kipya cha viongozi kwenye upinzani. Lipumba aliyegombea urais mara ya kwanza mwaka 1995, leo hii keshachuja, hawezi kuwa na ideas mpya zenye kuweza kuwa na mashiko kwa vijana.
Maalim na Zitto na wenyewe wanahitaji mbadala. Maalim akafikiri kususa kutoa mkono kungemuongezea umaarufu na heshima kumbe kajisababishia kejeli nyingi mitandaoni.
 
CHADEMA wamefanya kile kile walichokusudia, umenena wewe Jozi 1, nikiamini unaujua undani wa UKUTA.

Je, ni mafanikio gani ya "M4C"; "SANGARA"; Peoples Power!"; "mabadiliko lowasa - lowasa mabadiliko"; "UKUTA" na mengineyo ambazo ni baadhi ya kaulimbiu na operesheni za CHADEMA.

Kumbe huwa ni matamko, kaulimbiu na operesheni hewa. Tunashukuru wewe na wafuasi wa CHADEMA mnatambua hivyo. Basi CHADEMA ni chama cha siasa hewa, au viongozi ndiyo hewa, la wafuasi ni hewa.

Ni kweli hawakurupuka, ila kwa jamii iliyozungukwa na umaskini, katika nchi tajiri, uhewahewa wa aina hiyo unadhihirisha uwezo mdogo wa viongozi wa kisasa kuwatumikia.

Viongozi wa CHADEMA wajipange upya
Siasa za chadema ni hewa, kigeugeu na kisicho na msimamo.
Ni aibu kwa chama cha siasa kutangaza kwa kujivuna kuwa kinabadirisha gia angani.
Na nimeona mfuasi mwingine wa ukuta anashangilia kuwa wameilazimisha serikali kutumia mipesa mingi na hivyo Magufuli hatatimiza ahadi zake hata moja.
Hawajui kuwa haya yanayotokea ni hasara kwa taifa wanayoiunda kwa makusudi.
 
Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
CDM is dead and burried.
 
Ni kweli mkuu, kinahitajika kizazi kipya cha viongozi kwenye upinzani. Lipumba aliyegombea urais mara ya kwanza mwaka 1995, leo hii keshachuja, hawezi kuwa na ideas mpya zenye kuweza kuwa na mashiko kwa vijana.
Maalim na Zitto na wenyewe wanahitaji mbadala. Maalim akafikiri kususa kutoa mkono kungemuongezea umaarufu na heshima kumbe kajisababishia kejeli nyingi mitandaoni.

Mkuu siasa za nchi hii ni shaghalabaghala sana...CCM imechoka na ni rahisi sana kuitoa...lakini hawa wa kuitoa wenyewe ndio hata hawajitambui kabisaaaaaa....bora hata CCM iliyochoka.

Mfano kwa opposition iliyo serious...Inge focus kwenye mambo ya msingi sio Events kama UKUTA.....What have we achieved so far?

Ngoja tusubiri labda atajitokeza mwanasiasa mwingine mwenye akili kwa sababu nchi yetu ni ya kidemokrasia
 
Huo ndiyo ukweli ulio wazi.

Sina uhakika kama uko sawa kwa kutukuza English, lugha ambayo nina uhakika ni tatizo kwako. kumbe hujui lugha ya ya Taifa si 'English' au! Umesomea "english medium school"! Hongera kwa ujuha huo. Aibu.

Mbowe kweli ni mwiba mchungu kwenye mioyo ya wapenda amani na maendeleo, nchini. Alijidhirisha kama Kiongozi mwanamapinduzi kwa kauli zake za kuchukia maouvu katika jamii (rushwa, ufisadi, ubadhirifu) na utendaji mbovu (uzembe) wa watumishi wa serikali. Laiti angesimama kama mgombea Urais wakati huo, badala ya Slaa, naamini angeshinda.

Kwa sasa Mbowe kakosa mwelekeo, ila imedhihirika wazi kwamba kumbe ni mjasiriamali kisiasa. Amemkaribisha mtu ambaye chama chake kilimtuhumu ni fisadi papa, kwa sababu ya umaarufu wake kisiasa, ili apate majimbo mengi ya uchaguzi (ruzuku). Angalau hiyo ruzuku basi itumike kama mtaji wa kuweka vitega uchumi vya chama, ioi kiinuke kiuchumi na kuweza kujijenga zaidi, badala ya kuendesha operesheni za kujinufaisha binafsi na kikundi cha watu wachache kwenye chama.
Mbowe ambaye mnamsema hana muelekeo ameisimamisha nchi kwa mwezi mzima na ataendelea mpaka sisi tutakapoamua wenyewe.
tangu lini washabiki wa yanga wakashauri kwa nia njema kocha wa simba abadilishwe??
 
Mashabiki wa Yanga wanao uwezo wa kufanya hivyo ikiwa hawauoni upinzani halisi uwanjani. Siwezi kuvumilia kuiona nyumba yako inateketea kwa moto halafu nikae pembeni wakati pengine chanzo cha moto huo kinaweza siku moja kuwa chanzo pia cha moto katika nyumba yangu.
 
Nyinyi mnaojua kingereza mbona mnafanya mambo ya kitoto. Mnabeep mtu mwenye mamlaka ya kumtia ndani mtu yoyote ndani ya dakika yoyote ile. Mbowe is the pain your big and stinky a.s.s ndio maana akipiga chafya nyinyi nyumbu mnaugua mafua.
mkuu punguza jazba Mbowe ameshindikanika tabia he is a master of the jungle.
 
Boonge la mtoto wa mjini, wengine wakiona hatua mbili mbele, kaka Aikaeli anaona tano mbele. Jamaa wa NHC wamevamia ofisi za Tanzania Daima, nahisi masuala ya kodi ya pango.
 
Natamani asikoment mtu mwingine zaid ya Mimi baada ya hapa, waishie kusoma tu na kuupuuzia Uzi huu usio na tija kwa wakati huu

Tena kwa mtu mzoefu kama Nyani Ngabu . Yaani mpaka sasa kama hujaelewa mafanikio ya UKUTA basi usiwe shabiki wa Demokrasia na mambo yake. Ni heri ukaungana na MMM.
 
Boonge la mtoto wa mjini, wengine wakiona hatua mbili mbele, kaka Aikaeli anaona tano mbele. Jamaa wa NHC wamevamia ofisi za Tanzania Daima, nahisi masuala ya kodi ya pango.
mkuu hasira za kumsindwa Mbowe mmeamishia kwenye meza na mashelf.
mnapigana na mashine hamuiwezi nyie.
 
Na hili nalo ni fursa. Unajua mwenzio akikutemea mate iwe bahati mbaya au makusudi wewe ukarusha ngumi unadhani yupi ataonekana hamnazo?
 
Mkuu Daudi, siku zote ukichokoza mzinga wa nyuki basi na viatu vyako viwe tayari mkononi, la sivyo jiandae kuyakabili manundu. Kaka Aikaeli anaponzwa na kiburi chake. JK alikuwa mpole, mwenye kupenda diplomasia zaidi, this time duh.
 
Na hili nalo ni fursa. Unajua mwenzio akikutemea mate iwe bahati mbaya au makusudi wewe ukarusha ngumi unadhani yupi ataonekana hamnazo?
Ogopa sana lidude fulani linaitwa mfumo. Linapoingia kazini, jiandae kwa maumivu, na huo mfano wako unakuwa umesahaulika kwani hautaweza kukusaidia.
 
Back
Top Bottom