Hawa CHADEMA ndo basi tena.
Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.
Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.
Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.
Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.
Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.
Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?
Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.
Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.
Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?
Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.
Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.
Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.