Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

downloadfile-1.jpeg

Swissme
 
Mie nina imani na CHADEMA

Kwa sie ambao tuliona vitisho vya gharama kubwa vilivyoonyeshwa, tumeanza kuwa na imani kuwa mpenda amani na utulivu wa wanachi ni chadema na wala sio police au wanaowatuma.
Msg sent na delivered.
 
Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
chadema zamani walikua na msimamo mkali kupinga ufisadi. kama hujui msimamo
wao wa siku hizi ni kutaka kumuingiza lowassa ikulu.
 
Missions,Plans,Visons & Objectives sucessefuly 100%.
Lengo la CDM ilikuwa siyo Physical protest kama wengi mlivyofikiria na ni wachache sana waliojaliwa na wenye kuwa na uwezo toka kwa Allah ndiyo pekee walielewa.
 
Huyu katibu mkuu wa CHADEMA anayo mikakati ya kisayansi.Anao upeo wa hali ya juu kabisa.Ukweli anawafanya ndugu zetu wa upande ule wacheze ngoma anayopiga na waache kufanya kazi.Niwatahadharishe msipokuwa makini na hawa CHADEMA hususan katibu mkuu wao hamtafanya chochote miaka hii mitano na mwisho wake mahakama ya BALLOT BOXES itawahukumu.
 
Fanya research then utupe majibu.waweza tengeneza maswali webmonkey.com then ukashare link nasi.ituakupa urahisi wa kupata unachokitaka
 
Bado nina imani kubwa sana na Chadema, kwani kilichoplaniwa before kimetimia kwa 100%, hakuna uvunjifu wowote wa amani wala umwagaji damu uliotokea.

The mission accomplished and succeed.

Nb:
Huu uzi ni mahususi kwa Chadema's followers na nitashangaa gamba mwenye chuki na upinzani toka tumboni mwa mamaye kuhusika humu.

Soma Swali, elewa Swali, jibu swali
 
Ni chadema tu wanaoipenda, kulinda, kutetea amani ya Tanzania. Amani hailindwi na mtutu bali mtutu huja baada ya kutoweka amani. Amani inaweza kurudi au isirudi kwa mtutu. Na urudi baada ya athari kubwa za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
 
Operation ukuta ilikua sio kwa ajiri ya kuondoa utawala Wa Ccm Bali ilikua political tactic ya chadema ili iendelee kua maskioni mwa watanzania na wamefanikiwa kwa asilimia zaidi ya mia moja wamezuia siasa mpaka 2020 ila kwa huo mwezi wa nane wote chadema ndo ilikua habari iliyokua ikizungumziwa sana sasa kupelekwa mbele kwa siku hii kunaipa tena chadema muda wa kuzozana na watawala na kwa watawala wasiojua kinachoendelea wanaendelea kucheza mziki wa chadema bila kujua au kwa kuzani wanawakomoa mfano mkuu wa mkoa fulani aliyetangaza siku ya kupanda miti hajui anacreate attetion ya kuwafanya CDM wawe kwenye news huku akiwa amesahau operation hii ni kwa nchi nzima mfano CDM wakienda fanyia maandamano mwanza yeye anakua kasaidia nn.. Naona CDM wataendelea kua maskion mwa watu mpaka 2020 wanafanya siasa indirect
Operation ukuta imewapa kiki CDM maradufu mpaka ccm kupoteza mvuto kwenye kuuza magazeti
Cha msingi ccm wakae kimya tuu
 
Nina imani nayo. Ukipenda namba ujue pia kufanya hesabu.
 
Chadema Saizi kinafaa kubaki makumbusho ya taifa
Kama ndio hivyo, Makumbusho hayo ndio hayo yaliyoandaliwa gwaride la mwezi mzima nchi nzima na jeshi la Polisi, usalama, na kuhitimishwa na sherehe za usafi na JWTZ ...

Hicho chama huko makumbusho nafikiri ni cha ukombozi basi ...
 
Kazi ya kuudhoofisha upinzani Tanzania na CCM kuendelea kuwa madarakani inaelekea kufanywa kwa ustadi wa hali ya juu sana kwa kuwatumia mawaziri wakuu wastaafu na hasa Edward Lowassa.Kazi ameifanya kiweredi sana kiasi kwamba yeye ndie mwenye uwezo sasa kuidhibiti CHADEMA yenyewe na vyama vingine vyote vya upinzani.Ukiangalia nyendo zake za kisiasa kwa makini utauona ukweli huu.Ni ajabu sana kwa viongozi na wafuasi wa CHADEMA kushindwa kabisa kubaini mbinu hii na mpaka sasa bado hawaoni kuwa wenzao CCM wamewazidi kete katika mchezo huu.Badala ya kuendelea kumlaumu Rais na chama kilichoko madarakani ni vizuri sasa wakajirudi na kuanza kujipanga upya kwa kuangalia kwa undani zaidi pale walipojikwaa na kufanya marekebisho ya kina,Vinginevyo hatma ya upinzani itabakia kwa chini ya mwanasiasa mmoja mmoja.
 
Maadamu katiba itaendelea kusiginwa na uongozi wa kufata sheria utaendelea kupuuzwa itafika tu siku kitanuka kama vile Gabon au Venezuela.
 
Back
Top Bottom