Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Nimepita Kwenda Social Networks Nyingi Nimegundua Haya:
a)Wana CCM Wameumia Sana Baada ya CHADEMA Kuhairisha UKUTA
b)Baadhi ya Wana CHADEMA Analojia Wamekasirishwa Na Uhairishwaji wa UKUTA!
c)Ila Wana CHADEMA Digitali Wengi Tunaopenda Siasa za Hoja Tumeipenda Hii Kete!
d)JWTZ Na Polisi Wataendelea na Usafi na Operesheni ya VIKINDU!
Iramba huwa tupo pamoja lakini kwa hii great disappointment, sikubaliani nayo, nimesikitika na kufedheheshwa kwa hili la kushindwa kusimamia vyema kusudio lililo beba mstakabali wa taifa la kidemokrasia, nafikiri hata kuacha siasa au kuhama jukwaa ngoja nitafakari kwanza. But am greatly disappointed
 
watu mbona hamjibu swali jaman km nimwelewa vizuri mtoa hoja kauliza swari jepesi tu
Bado wapo wenye imani na CHADEMA?
Kusoma na kuelewa ulichokisoma ni janga kubwa sana.

Mtu unaweza ukamwuliza swali jepesi la moja kwa moja lakini jibu lake anakuwa analielewa yeye tu.

Na ndo maana viwango vya ufaulu kwenye shule zetu ni mdogo sana.
 
Kusoma na kuelewa ulichokisoma ni janga kubwa sana.

Mtu unaweza ukamwuliza swali jepesi la moja kwa moja lakini jibu lake anakuwa analielewa yeye tu.

Na ndo maana viwango vya ufaulu kwenye shule zetu ni mdogo sana.
minashanga kwani wengi wanaojita wapenda chadema hawapendi kujibu kwa hoja zaidi nikujificha kwenye matusi nakejeli na sio kujibu hoja zamsing
 
Huyu amenunuliwa tayari kama Profesa lipumba, jiandae kukatwa mkia
Nani katika dunia hii ameishinda Dola kwa matamko zaidi ya mapunduzi!

Ni wapi katika dunia hii viongozi wa dini wamefanikisha usuluhishi wa kisiasa, zaidi ya kukoleza machafuko!

Ni kiongozi gani wa kisiasa katika dunia hii amefanikiwa kisiasa kwa kuwa kigeugeu!

Ni nchi gani katika dunia hii mtawala aliyepewa madaraka kwa kura akaondolewa kwa nguvu!

Viongozi wa CHADEMA wanayajua yote hayo, wamebp wakitegemea watapigiwa, mh!

Akili za viongozi wa CHADEMA zimegonga UKUTA walioujenga wenyewe.
 
Nyerere hakuwa kigeugeu ndio maana anaheshimika mpka leo
... si kweli. alikuwa bepari hadi 1967 akageuka akawa mjamaa; alimuunga mkono maasi ya Ojukwu wa Nigeria baadaye akawa kigeugeu, aliua jumuiya ya EA na kuanzisha SADC na COMESA, n.k.
 
Kwanza natambua kabisa mchango wa mbowe katika ukuaji wa cdm. Uwezo wa m/kiti umefikia kikomo hili liko wazi na kwabinadam yeyote hili ni swala la kawaida wala si udhaifu. Yapo mambo mengi sana yanayothibitisha. Kashindwa kutetea, kuendeleza na kuihubiri vema misingi na agenda ambazo wanainchi tuliamini na kupata tumaini la kuwa wakombozi wetu katika kweli. Wahenga walisema "mbio za sakafuni huishia ukingoni" hoja nyepesi yenye masilahi kwaviongozi huchukua umaarufu na kudumu kwa muda mfupi sana, lakini hoja na agenda yenye masilahi na utetezi kwa wanainchi wanyonge hiyo hupokelewa kwa kasi kubwa na kudumu milele kwenye fikira za watu. Nitoe mifano ya agenda ambazo wanainchi walizielewa, zikadum kwenye fikira zao nampaka leo hawaamini kama kweli mmezitupa:- uadirifu, rushwa, mikataba mibovu, wizi na ufisadi hizi ni hoja ambazo hamkutumia nguvu kubwa sana ili kuweza kueleweka. M/kiti kaa au waachie wasomi wako wachama naamini wanaouwezo mkubwa sana wakufikiri na weredi kuendeleza pale ulipofikia, watakuja na mipango, mikakati na oparesheni itakayoendana na nyakati na mahitaji ya sasa na badae naamini mtapata uungwaji mkubwa sana bila kutumia nguvu. Tabia ya Kubadilishia gia angani inawachosha wafuasi, wanachama na wanainchi kwa ujumula. Moyo unaniuma sana napoona upinzani wa kweli unapata upofu kwa kero za wanyonge. Achaneni na sanaa za maigizo, tujikite katika siasa za ukombozi kama kweli tunalengo la kuja kushika dola
 
Huyu amenunuliwa tayari kama Profesa lipumba, jiandae kukatwa mkia

Kwanini kila anayepingana na hoja au maamuzi ndani ya cdm huishia kutungwa majina ya ajabu ajabu kama, msaliti, anatumika, kanunuliwa? Ingelikuwa vyema sana kama democracy ingeanzia ndani ya vyama vyenu kwanza😀!
 
Naiamini mbinu wanayoitumia chadema kupinga uvunjaji wa katiba na sheria za nchi. Wangeandamana kesho wangeambiwa wamewaingilia JWTZ ambao ni serikali pengine wangekamatwa wananchi wengi wasio na hatia . Tukutane 1st October.
Chadema Mimi ni CCM niliyeamuwa kuwaunga mkono kwenye maandamano.
Imetoka hiyo, utampata nani october? Kama mlishindwa kuvishawishi vyama viundavyo ukawa, hiyo october mtawezaje kuwashawishi tena hao wachache waliojitolea kuwaunga mkono kwenye ukuta?
Mbinu hiyo imeshafeli, tafuteni nyingine.
 
Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
Hakika
 
Kuna mwaka, kulitokea mtafaruku bungeni kati ya wana chadema na cuf. Basi chadema wakaombwa waombe radhi wakagoma.
Baada ya presha kua ndefu mwishowe mbowe akakubali kuomba msamaha na kutangua kauli.
Kuna neno alisema kabla hajatangua kua:- kurudisha majeshi nyuma sio kushindwa vita. Bali ni sehemu ya mkakati wa vita"


Kumbe kurudi nyuma sio kushindwa bali ni sehemu tu ya mkakati.
 
CHADEMA imekaribisha sumu kwenye chama ingawaje watu kwa uboya wao hawataki kuona! Hivi unatarajia "Muungwana" Lowassa akubaliane na wazo la kufanya maandamano yasiyo na kikomo?! Hivi unatarajia "Mstahimilivu" Sumaye akubaliane na hilo wazo wakati miaka 10 aliyohudumu kama PM ilikuwa ni full kuwacharaza CUF virungu?! Eti kuna mtu mmoja nae anaitwa Kamanda Kingunge... ashakum si matusi, hata akienda maliwatoni anakariri vifungu vya Katiba ya CCM tena ya enzi ile ya Chama kushika hatamu!!!! Huyo Katibu Mkuu wao sikutaka kumtuhumu mapema kwa kile nilichoamini tumpe muda na anajipanga... lakini leo hii sina shaka hata kidogo kusema CHADEMA wana Katibu Mkuu ambae sifa zake angefaa labda kuwa mpiga chapa wa ex Katibu Mkuu Slaa!!

Nimeshamsikiliza Mbowe mara nyingi sana tena siku ya kwanza kumsikia nilim-admire sana! Though jamaa inasemekana shule imepita kushoto, he's very intelligent na mpangiaji mzuri wa hoja! Ni vile tu ana macho ya kutisha na mweusi tii lakini Mbowe is very diplomatic!!! Sasa key persons wote CHADEMA hivi sasa ni diplomatic-- Mbowe, Lowassa, Sumaye! Mtu kama Tundu Lissu hawezi kuwa na cha kusema against any of them! The same to Lema, Mdee, Mnyika and the like!

Pole sana Dk. Slaa popote pale ulipo! Maboya wa CHADEMA wanakuita msaliti usiyefaa kwavile tu ulipinga kukaribisha mamluki kwenye chama!! Na amini amini nawaambia; hawa mamluki wataendelea kuwatafuta hadi mshike adabu!!
 
Kuna mwaka, kulitokea mtafaruku bungeni kati ya wana chadema na cuf. Basi chadema wakaombwa waombe radhi wakagoma.
Baada ya presha kua ndefu mwishowe mbowe akakubali kuomba msamaha na kutangua kauli.
Kuna neno alisema kabla hajatangua kua:- kurudisha majeshi nyuma sio kushindwa vita. Bali ni sehemu ya mkakati wa vita"


Kumbe kurudi nyuma sio kushindwa bali ni sehemu tu ya mkakati.
Kwa UKUTA sioni CDM.iliposhindwa!! Watu hatukulala usingizi mwezi mzima!! Tumefanya zoezi mpaka vitambi vimekwisha!! Jamani laiti mngejua Mbowe alivyotutesa acheni kabisa!! Kila mtu kashusha pumzi na likizo tumeruhusiwa hii leo.

Asante Mbowe!!#
 
Huo ni mchezo wa Draft,unachezwa na wakubwa wetu.Sie ni watazamaji wa mchezo kimoyomoyo tunasema "angecheza pale angekula" lkn mawazo yetu n tofauti na anaecheza kwani yeye ameiona KETE nyingine atakayokula bila kuliwa.
Binafs bado ninaimani na CHADEMA,naamini hawajakurupuka kwa maamuzi waliyofanya,bado wanazidi kuudhihirishia ulimwengu kwamba wao ni wapenda Amani na ndio maana wanatoa nafasi ya majadiliano.Japo ni tofauti na Serikali ambayo inajivunia Dola,na ilishajiandaa kuwashambulia waandamanaji .
Chadema hawajakurupuka.
Wamefanya kile kile walichokuwa wamedhamiria.
Kukoki watu kwa kuwahadaa na matamko ya operesheni hewa.
Ni hewa kwa sababu hakuna aliyekuwa na nia ya dhati ya kuandamana tangia mwanzo.
"A publicity stunt".
Ni kweli hawajakurupuka.
 
Mbona nyie mlikuwa mnapiga kelele kwenye Instagram huko na siku moja kabla ya siku ya siku ujumbe umepenyeza.

Ona hawa wenzio....hivi kweli wamekaa hata mkao wa ku rumble hawa?


Strategically Chadema wamefaulu kuifanya serikali iyumbe, wamerusha ndege, many arrests, wametumia mapesa mengi, hii yote Ni hasara inayotafsirika kwenye uchumi ulipotea. Let say watafanya mambo Kama haya muda mwingi Na serikali itakuwa inafanya hivi walivyofanya? Mwishowe serikali itaona Ni upuuzi kupoteza pesa bure.
 
Back
Top Bottom