Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Well said Ngosha,kusema ukweli watakaoendela kuwaamini CHADEMA basi wana hitilafu kwenye
Frontal lobe yao.Watu wazima Adrenaline zao zimepanda kwa mwezi mzima,leo mwishoni kabisa wanaambiwa their workdone is equal to zero.Halafu wanapewa siku 31 zingine tena,bado wamo tu,itabidi wapimwe akili kwa kweli.
Ndio maana wanafwata mkumbo, waliambiwa Lowasa fisadi wakaruka ruka kwa furaha, wakaambiwa tena Lowasa sio Fisadi
 
Kama mtu hauna jibu si useme tu kuwa huna.

Ya nini kuzunguka na kuanza kutoa pumba?
Tuna tofautiana katika kufanya reply hapa JF mwingine anakupuuzia hakujibu ,mwingine anakuelewesha ,mwingine anakujibu anavyojiskia. Kama katoa pumba well and good hiyo ni kwa mujibu wa akili yako wewe kwake yeye ni credit.
 
Bado tuna imani kubwa sana na Chadema na tutaendelea kuwa na imani ni chama cha upinzani pekee kimeweza kutangaza maandamano na kufanikiwa kwa kiasi kabla ya kufanya baada ya kusaidia na vyombo vya dola. Tumearisha kwa muda kupisha majadiliano .
 
Mimi nina imani na chadema.
Imani itoweke kisa ukuta. Kwakwel naipenda mno maana viongozi ni wasikivu. Wamewasikilza wa2 mbali mbali pmj n viongoz wa dini so wametulia. Mtukufu angekua anackilza wa2 vzr km viongozi wa chadema saiv 2ngekua 2nakula mema
 
Kwa mchambuzi makini, Chadema ndio walio win katka issue hii na propaganda ya UKUTA licha ya kuahirishwa kwa hayo maandamano. Sababu ni nyingi sana.
1. Kwa mara nyingine tena baada ya uchaguzi kila kona ya nchi jina Chadema limevuma. Maana yake hata mtoto anayeanza kujifunza kuongea anaweza kujikuta akianza na neno chadema kuliko chama chochote cha siasa. Hii promo sio ya kitoto
2. Wamelifikisha suala la kinachodaiwa kuwa udikteta midomoni mwa karibu kila mtu. Kila mahali sasa ni kupinga au kutetea demokrasia. Yaani chadema wame -set agenda, na sasa imekuwa kila kona. Si jambo rahisi kuanzisha mjadala wa issue nyeti kama hii ktk kipindi hiki.
3. Wameshusha mzigo wa kutoaminiwa na baadhi ya watu wanaodhani au walioaminishwa kuwa chadema ni chama cha kutumia nguvu pekee. Kwamba hawapendi amani! Sasa wao wametangulia ktk meza ya mazungumzo ya kurudisha haki yao ya kuendesha siasa huku wakitupia upande mwingine wajibu wa kuja kikaoni ili kuonyesha na kujionyesha kama wana nia njema. Hili likishikana sasa, watapunguza ukubwa wa watu wasiowaunga mkono kwa sababu ya kile kinachitwa kupenda vurugu
4. Kwa mara nyingine tena tumeona nguvu kubwa ya maandalizi ya jeshi la polisi kukabili chadema. Ni kwa ushauri kwa wananchi kutokuungana na chadema, propaganda hadi vitisho. Kwa maana nyingine ile chadema wanaiita nguvu ya umma ilikuwa imeandaliwa mkakati mkali kuizima. Kwa hiyo kile kibwagizo cha peoples power kinaonekana kipindi hiki kuwa kumbe sio wakati wa kampeni tu, ni maisha kabisa
 
Mi nilisema hawa jamaa, wakiwa technical, waairishe ukuta. Ndo kilicho fanyika. Wangeumia tu, kulikuwa hamna jinsi. Na hiyo tarehe 1 October hakuna kitu kama hicho. Viva magufuli, Viva Tanzania. Na msisumbuke eti vikao vya maridhiano.
 
Audio: Huwezi kuwanunua watu mpaka uwe umeshanunuliwa tayari na waliokununua wawe wamehakikishiwa utawalipaje. Kuweni makini sana na huyu mtu wa kuogopa kama ukoma
 
Attachments

Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
IMG-20160831-WA0051.jpg
 
Leo hii kwa mkono wangu nimepokea wanachama 421 wapya kujiunga na cdm
 
Nilielewa vyema chadema na msimamo wao alipokuwepo Dr Slaa,Dr angekuwa mgombea hata angeshindwa watu wangeendelea kuwa na imani na chadema,kuliko kumleta lowasa halafu akafeli uchaguzi.
 
Waliokuwa wakiwaita wale walioikimbia CHADEMA leo hii wameudhihirishia umma kuwa wao ndio wasaliti
Mh.EL kasaliti CCM alikolelewa miaka takribani 38.
Mh.Mbowe amemsaliti dr.slaa kwa kumpokea Lowassa na kumpa kiti cha Urais mwaka jana
Mh.Mbowe huyohuyo amewasaliti watanzania bila sababu ambazo si za msingi juu ya UKUTA uliokuwa utekelezeke kesho.
Mh.Mbowe huyohuyo amemsaliti zitto kabwe na kumfukuza chamani kwa madai kuwa jamaa ni mfichua siri za kambi.
Mh.Mbowe huyohuyo amewasaliti watanzania kwa kuwa yeye ni M/kiti wa KUB kwa kuwatoa wawakilishi wao.
Mh.Mnyika amesaliti kauli yake ya kuwa UKUTA uko palepale baada ya mazungumzo na viongozi wa dini.
Ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia vipi DEMOKRASIA IKAPATIKANE NJE YA CHAMA KINACHOJINASIBU NA DEMOKRASIA?
Sitaki kuamini kuwa viongozi wote waliunga mkono hatua hii ya kuahirisha maandamano haya ya UKUTA.
MBOWE UMETUSALITI WATANZANIA,UMELISALITI TAIFA NA TAIFA HILI LITAANGAMIA KWA MKUU WA KAYA KAMA MLIVYOWEZA KUTUFAHAMISHA NINI HASA MKUU WA KAYA ANAFANYA KWA MUJIBU WA KATIBA.
NI HERI KUSALITIWA NA MWANAMKE KULIKO CHAMA,MAANA MWANAMKE UTAMPATA MWINGINE.
TAARIFA YA MBOWE IMENIUMIZA SANA LEO,KILA MTU ALIJUA SEP 1 NAINGIA MTAANI KWA HOJA ZANGU NZURI MBELE YA VIJIWE MBALIMBALI.
SITAKI TENA SIASA ZA CHADEMA,NITABAKI KUWA MTAZAMAJI WA SARAKASI HIZI ZA MWENDOKASI.
 
Wamejishushia heshima kabisa, kamwe sitawaamini watikisa kiberiti hawa, sio watu wawezao kusimamia wanalolianzisha. Ni wakati wa Mbowe kujiuzuru, kulinda heshima yake na kukinusuru chama. Hii ni baada ya kufanya makosa kadhaa ya kimsingi, ambayo yamekigharimu sana chama.
 
Back
Top Bottom