Bado sikubaliani na Tecno kuuzwa laki 6

Bado sikubaliani na Tecno kuuzwa laki 6

Mimi ni mtumiaji mzuri wa infinix ,kwa quality ya picha sijui ilikuaje but infinix s3 nilianza nayo ina quality nzuri Sana ya picha hata sasa natumia infinix note 7 lite quality ni nzuri afu mambo mengine unafanya setting ya resolution na rangi mwenyewe

Afu ni ujinga kuangalia simu kwa camera tuu,betri vipi,memory nk ndio muhimu kwangu na display ya maana
ndio maana nikaitaja a10 hapo,maana ina kila kitu unachopata kwenye infix na zaidi.

hizo picha unazosema za quality nzuri,sijui unamaanisha quality ipi,ila ukitumia simu ya zamani kabisa kama s5,utafundua uko na bomu hapo sio camera.
 
Nini matumizi ya hizi camera za kwenye simu? tofauti na kujipiga au kupiga mtu picha? Je hizo kamera zina kazi gani zaidi? Naomba nieleweshe
ni picha tu za ukumbusho ndio mhimu.


lakini picha hizi zitaishi miaka hata 50 baadae,tunataka tuzikute na uhalisia wa picha sio utumbo.
 
iPhone 4S mpaka 6 zinapokea updates OS kitambo mbona na watsap ipo isipokuwa iPhone 3G na 4 tuu ndo hawatumii watsap,

Hivi hili neno bado lipo ? Unfortunately has stopped sipendi techno hata bure
Natumia Techno lakini sioni hayo mambo mnayoyasema
 
Hivi mkuu inakuaje simu yenye display ya 720p kuweza kurekodi video za 1030p@30ps kama hiyo Tecno?

Hii simu ya RedMi inayouzwa chini ya laki 3 Kenya, huku Tanzania haiuzwi ama inauzwa bei ghali zaidi ya huko Kenya?
Display ni kitu tu kinaonesha Picha kama vile TV Hakuna mahusiano yoyote na kurecord, kinachorecord video ni camera, Hivyo ni kawaida kwa simu kuwa na uwezo mkubwa wa kurekodi kuliko display yake.

Tanzania Xiaomi hawapo official, kilikua na mizengwe na Kuna kampuni hapa Tz wameshasajili Jina Lao la MI. Hivyo hata ukiipata Xiaomi ujue ni mtu tu amenunua anauza na Mara nyingi bei zinakuwa ghali sana. Kenya zipo officially Hivyo inakuwa rahisi bei. Hio bei ya laki 3 ni Kenya tu.
 
Msihangaike na simu tumia ya uwezo wako hata tecno wapo poa ukiwa na hela ya kununua Tecno mnaumiza kichwa kwa vitu vinavyopita na fashion...
 
Tecno mkombozi wa wanyonge
Nakubaliana na Wewe.Kuna Siku nilienda kwa fundi Tecno yangu ilikuwa na shida ya screen nikabadili kwa 15,000/= tu, Wakati Kuna jamaa alikuwa na Samsung Galaxy S8,kubadili screen aliambiwa 430,000/=,nilishangaa Sana,ikabidi niulize je simu itakuwa bei gani?,Akaniambia 950,000/=,nikazidi kushangaa kwasababu simu yenyewe ilikuwa ndogo tu,very simple sikuona Cha pekee,lkn kwanini bei Ni lubwa vile.Ndipo nikajisemea moyoni Asante Tecno kwa kutujali sisi akina Yakhe.
 
Nakubaliana na Wewe.Kuna Siku nilienda kwa fundi Tecno yangu ilikuwa na shida ya screen nikabadili kwa 15,000/= tu, Wakati Kuna jamaa alikuwa na Samsung Galaxy S8,kubadili screen aliambiwa 430,000/=,nilishangaa Sana,ikabidi niulize je simu itakuwa bei gani?,Akaniambia 950,000/=,nikazidi kushangaa kwasababu simu yenyewe ilikuwa ndogo tu,very simple sikuona Cha pekee,lkn kwanini bei Ni lubwa vile.Ndipo nikajisemea moyoni Asante Tecno kwa kutujali sisi akina Yakhe.
Hiyo simu sio kwamba iko very simple kama unavyosema

Ungejaribu kuitumia hiyl S8 ndio ungejua utofauti wake na tecno

U'll never know until you have tried
 
Binafsi naamini TECNO itakuja kuwa Kampuni kubwa Ya Smartphone, Kwamba watakujaa kukaa meza moja na awa REDMI, REALMI, OPPO, NOKIA, SONY, SAMSUNG, ilaa kwa Sasa sioni kama wana simu yenye quality ya kuuzwa Laki 6

Najaribu kudadisi hivi nmeona simu ya Tecno CAMON 16 PRO, ina mwonekano wa kawaida tu.. inauzwa laki 6 na Nusu....

Naomba kuwasilishaa.
Ww kama hutaki wauze laki 6 bac mji organize nyie mtengeneze simu zenu mziuze kwa bei muipendayo !!
 
Back
Top Bottom