Bado nani sijamu UNFOLLOW Yanga?

Bado nani sijamu UNFOLLOW Yanga?

Screenshot_20250813_233614_Instagram.jpg
 
Nikiri wazi mimi ni shabiki wa Yanga kindakindaki kutoka moyoni. Lakini kwa hiki kilichofanyika imekua chukizo kwangu na kwa wengine wengi kama mimi. Najua wengine watabeza ila tayari nime unfollow kuanzia page ya Instagram mpaka viongozi wote wa Yanga.

Katika wakati kama huu hawakupaswa kutugawa hivi. Nakiri wazi nitabaki kuwa shabiki wa mpira kwa kuangalizia mabanda umiza tu, hata jezi sinunui mmetukera sana viongozi.
Shame Shame Shame.
Ndio maana huwa mnaambiwa hamna akili.
Mbona yanga ni timu ya ccm kitambo?
Na miaka ya 90 walikuwa wakifunga goli wanashangilia "ccm..ccm..ccm!"
Unanishangaza eti ulikuwa hujui hili
 
Hapo mwenye shida ni Hersi na sio Yanga. Yanga ni taasisi ambayo ina watu nyuma yake kuanzia mashabiki, wanachama, viongozi akiwemo huyo Hersi. Amelewa sifs anataka kuikojolea timu yetu. Aache uhuni, Yanga ni kubwa yeye ni punje tu ya mchanga kwenye bahari. Aache ungese.
 
Ndio maana huwa mnaambiwa hamna akili.
Mbona yanga ni timu ya ccm kitambo?
Na miaka ya 90 walikuwa wakifunga goli wanashangilia "ccm..ccm..ccm!"
Unanishangaza eti ulikuwa hujui hili
Ambaye huna akili ni wewe. Yanga haina chembe wala harufu namambo ya siasa ni kupotoka kwa baadhi ya viongozi wanaojisahau na kulewa sifa kutaka kuihusisha na siasa. Pathetic
 
Hapo mwenye shida ni Hersi na sio Yanga. Yanga ni taasisi ambayo ina watu nyuma yake kuanzia mashabiki, wanachama, viongozi akiwemo huyo Hersi. Amelewa sifs anataka kuikojolea timu yetu. Aache uhuni, Yanga ni kubwa yeye ni punje tu ya mchanga kwenye bahari. Aache ungese.
Sasa yeye ametumia nafasi yake kuichafua Yanga. Yan ameitumia Yanga kwa maslahi yake binafsi
 
Naunga mkono hoja , hata ukiwa Shabiki wa mpira automatically lazima akili yako iwe na matatizo
Hta kama mtu atarudi kuishabikia Yanga au kuendelea kuisapoti kwa namna yoyote ile, kuna sehemu ya funzo ambayo viongozi wa klabu watakuwa wamelipata.

Na hilo ndilo jambo la msingi mashabiki wanapolalamika, si kwa lengo la kuiacha timu kabisa, bali kuonyesha kuwa kuna mipaka ya kuvumilia maamuzi yasiyo na heshima kwao.

Kwa mfano, tupo kwenye kipindi cha kuelekea msimu mpya. Hiki ni kipindi ambacho klabu humtegemea sana shabiki kwa mambo kama:

  • Ununuzi wa jezi mpya
  • Tamasha la Siku ya Wananchi (kutambulisha wachezaji wapya)
  • Kujenga morali na hamasa ya msimu mpya
Sasa fikiria mashabiki wakisema: “Hatununui jezi, hatuhudhurii tamasha.” Halafu siku ya tukio inafika, uwanja uko nusu, jezi hazijauzwa, na hamasa iko chini unadhani viongozi hawatapokea ujumbe?
 
Kwakweli viongozi wa klabu yetu wametuonesha dharau kubwa sana najiuliza kwanini hawakufanya iwe Siri?kulikuwa na ulazima gani wa kuja public kujigamba kuwa wamechangia pesa CCM? Hiki ni kiburi kwakuwa wanajua watanzania tulivyo,Leo hii tunalalamika hapa lakini subiri ligi ianze Kila mmoja atasahau yaliyotokea
 
Ni vizuri akajitokeza hadharani na kuondoa hii sintofahamu. Hata mimi Yanga damdam pamoja na kumiliki kadi ya ccm, bado sijafurahishwa hata kidogo na hiki kitendo chake cha kujipendekeza kwa Bibi wa Kizimkazi, kupitia mgongo wa klabu ya Yanga anayo iongoza.
Kumbe una kadi ya Ccm
 
Back
Top Bottom