Hta kama mtu atarudi kuishabikia Yanga au kuendelea kuisapoti kwa namna yoyote ile, kuna sehemu ya funzo ambayo viongozi wa klabu watakuwa wamelipata.
Na hilo ndilo jambo la msingi mashabiki wanapolalamika, si kwa lengo la kuiacha timu kabisa, bali kuonyesha kuwa kuna mipaka ya kuvumilia maamuzi yasiyo na heshima kwao.
Kwa mfano, tupo kwenye kipindi cha kuelekea msimu mpya. Hiki ni kipindi ambacho klabu humtegemea sana shabiki kwa mambo kama:
- Ununuzi wa jezi mpya
- Tamasha la Siku ya Wananchi (kutambulisha wachezaji wapya)
- Kujenga morali na hamasa ya msimu mpya
Sasa fikiria mashabiki wakisema:
“Hatununui jezi, hatuhudhurii tamasha.” Halafu siku ya tukio inafika, uwanja uko nusu, jezi hazijauzwa, na hamasa iko chini unadhani viongozi hawatapokea ujumbe?