Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Bado kuna watu wazima wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili.

images (22).jpg

Siku ya sherehe ya mwaka mpya nilikutana na dada mmoja anaitwa Veronica (hili sio jina lake halisi) ambaye nilimaliza naye shule ya msingi mwaka 1999.

Huyu dada nilikwisha kutana naye mwezi kama wa August maeneo ya Banana Ukonga huku Dar. Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana miaka takribani 15 tulipiga story nyingi sana za zamani.

Sasa nilipokutana naye tena Ijumaa ya tarehe 01 January 2020 huku Kivule ninapokaa (kwa maana aliniambia anakaa Kata moja na mimi) nilimuona anaongozana na binti mdogo wa miaka kama 9 hivi.

Tena huyo binti wamefanana kweli kweli. Basi tulipoonana tulisalimiana tena kwa furaha sana. Baada ya story kadhaa nikamuuliza, huyu ndio mtoto wako wa kwanza? Akakataa. Akasema hapana, huyu sio mtoto wangu.

images (24).jpg

Huyu ni mdogo wangu wa mwisho. Mtoto wangu ameenda kwa baba yake kusalimia atarudi shule zikifunguliwa. Sema ndio rafiki yake mkubwa sana huyu (mdogo wake wa mwisho) kwa maana wamepishana mwaka mmoja tu.

Mimi sikuwa na jambo lingine la kumwambia zaidi tu ya kumpa hongera lakini nikawa ninajisemea tu kimoyomoyo "ina maana haya masuala ya mtoto na mama kuzaa kwa pamoja bado yanaendelea katika karne hii ya 21?"

Hii issue nilikuwa ninaiona tu kwa wazee wa zamani ambapo unakuta mtu unakutambulisha "huyu ndio baba yangu mdogo/shangazi yangu tumbo moja na baba" au "huyu ndio mama yangu mdogo tumbo moja na mama" lakini ukijaribu kuwatazama actually wanalingana umri au wamepishana mwaka mmoja tu.

images (21).jpg

Mimi ni moja kati ya watu wanaokerwa sana na lugha za hawa dada/mama zetu manesi lakini linapokuja suala la kukemea wamama/wababa wanaoendeleza utamaduni huu wa hovyo mimi ninawaunga mkono sana.

Kuna mtoto wa shangazi yangu mmoja yeye ni nurse huko Geita anakwambia mama mtu mzima wa design hii akija kujifungua (wanawafahamu sana kwa maana vijijini watu ni wachache) huwa wanawachamba kwa maneno na lugha chafu mbele ya waume zao.

Kuna mama mmoja aliwahi kufariki mwaka 2006 alipokuwa anajifungua wakati bado tunakaa kule Keko. Sasa wakati wa mazishi watu wamekusanyika na wageni wanataka kujua chanzo cha kifo chake ikawa sasa ni aibu kusema kuwa amekufa kwa sababu ya "complications" za uzazi ilhali binti yake mkubwa ana mtoto wa miaka 2 tayari.

images (23).jpg

Mimi binafsi ninaona sio jambo la hekima wala busara kwa mama/baba kuendelea kuzaa watoto wengine wadogo ilhali wale "first born" wamekwisha kuwa wababa/wamama wanaokaribia ku-reproduce.

Sio vizuri mama kuonekana ana tumbo kubwa la ujauzito pindi wale "first borns" wanapokuwa wamepevuka akili.

Kwa maoni yako, ni sahihi mama na binti/mtoto kuendelea kuzaa kwa pamoja? Mtoto wa mwisho kulingana na mjukuu wa kwanza?

"HAPPY NEW YEAR 2021"

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau
=====
mimi nilishawah kuona Mama amejifungua halafu anaemkanda ni binti yake mwenye watoto wawili,kweli si sawa.Imagine mamamkwe amejifungua na unatakiwa kumpelekea zawadi ya nepi Shemeji yako aliezaliwa ambaye ni mjomba au mama mdogo wa wanao. Si sawa
 
Hao wazee wa namna hiyo mara nyingi huwa hawako responsible, anatafuta kabinti ambako hakajielewi anaishia kukapa mimba. Kunabaki mwendelezo wa mizinga ya hapa na pale kutoka kwa watoto wake wakubwa, hadi anatengeneza migogoro kwenye familia..
 
Mimi nilizaliwa kijijini.

Kaka yangu wa kwanza kazaa mtoto ambaye ni mkubwa kwangu.

Bro ana miaka 70.
Dingi naye yupo....

Sisi watoto wa mwisho ndio tunamsaidia sasa hivi.
Yalikuwa maisha ya kijijini lakini kila mtu anafanya jambo kutokana na mazingira yaliyopo kwa muda flani.

Kwa hali ya maisha ya sasa ni kazi sana kuzaa watoto wengi
 
Lakini watoto wa uzeeni ndio huwafariji wazee baada ya wakubwa wote kuanza maisha yao na isitoshe siku hizi utamaduni wa kuwaachia wazee wajukuu wawalee ni kama unakufa, kheri hiyo kidogo inawaondolea upweke ndani ya nyumba
 
mimi mtu anayezaa zaidi ya watoto 3 katika dunia ya sasa mi huwa simuelewi.
Zamani watu walikuwa wakizaa watoto wengi kwa sababu elimu na njia za uzazi wa mpango kulikuwa hakuna, sasa hivi zipo tele, mtoto pia alikuwa akitumika kama rasilimali ya kulima shamba na kuchunga mifugo, saa hivi mtoto anatakiwa alishwe, avalishwe na asomeshwe na utengeneze future nzuri kwa kuwekeza sio waje kutembea juani wakisaka ajira
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu Watanzania;

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili.

Siku ya sherehe ya mwaka mpya nilikuwatana na dada mmoja anaitwa Veronica (hili sio jina lake halisi) ambaye nilimaliza naye shule ya msingi mwaka 1999.

Huyu dada nilikwisha kutana naye mwezi kama wa August maeneo ya Banana Ukonga huku Dar. Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana miaka takribani 15 tulipiga story nyingi sana za zamani.

Sasa nilipokutana naye tena Ijumaa ya tarehe 01 January 2020 huku Kivule ninapokaa (kwa maana aliniambia anakaa Kata moja na mimi) nilimuona anaongozana na binti mdogo wa miaka kama 9 hivi.

Tena huyo binti wamefanana kweli kweli. Basi tulipoonana tulisalimiana tena kwa furaha sana. Baada ya story kadhaa nikamuuliza, huyu ndio mtoto wako wa kwanza? Akakataa. Akasema hapana, huyu sio mtoto wangu.

Huyu ni mdogo wangu wa mwisho. Mtoto wangu ameenda kwa baba yake kusalimia atarudi shule zikifunguliwa. Sema ndio rafiki yake mkubwa sana huyu (mdogo wake wa mwisho) kwa maana wamepishana mwaka mmoja tu.

Mimi sikuwa na jambo lingine la kumwambia zaidi tu ya kumpa hongera lakini nikawa ninajisemea tu kimoyomoyo "ina maana haya masuala ya mtoto na mama kuzaa kwa pamoja bado yanaendelea katika karne hii ya 21?"

Hii issue nilikuwa ninaiona tu kwa wazee wa zamani ambapo unakuta mtu unakutambulisha "huyu ndio baba yangu mdogo/shangazi yangu tumbo moja na baba" au "huyu ndio mama yangu mdogo tumbo moja na mama" lakini ukijaribu kuwatazama actually wanalingana umri au wamepishana mwaka mmoja tu.

Mimi ni moja kati ya watu wanaokerwa sana na lugha za hawa dada/mama zetu manesi lakini linapokuja suala la kukemea wamama/wababa wanaoendeleza utamaduni huu wa hovyo mimi ninawaunga mkono sana.

Kuna mtoto wa shangazi yangu mmoja yeye ni nurse huko Geita anakwambia mama mtu mzima wa design hii akija kujifungua (wanawafahamu sana kwa maana vijijini watu ni wachache) huwa wanawachamba kwa maneno na lugha chafu mbele ya waume zao.

Kuna mama mmoja aliwahi kufariki mwaka 2006 alipokuwa anajifungua wakati bado tunakaa kule Keko. Sasa wakati wa mazishi watu wamekusanyika na wageni wanataka kujua chanzo cha kifo chake ikawa sasa ni aibu kusema kuwa amelufa kwa sababu ya "complications" za uzazi ilhali binti yake mkubwa ana mtoto wa miaka 2 tayari.

Mimi binafsi ninaona sio jambo la hekima wala busara kwa mama/baba kuendelea kuzaa watoto wengine wadogo ilhali wale "first born" wamekwisha kuwa wababa/wamama wanaokaribia ku-reproduce.

Sio vizuri mama kuonekana ana tumbo kubwa la ujauzito pindi wale "first borns" wanapokuwa wamepevuka akili.

"HAPPY NEW YEAR 2021"

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Inategemea na mazingira na familia yako ikoje.
Ndugu Marehemu Mengi alipoona hana wajukuu akaaamua kutafuta wajukuu yeye mwenyewe. They are now 6/ 7 years old.
 
Sio jambo zuri kuzaa ikiwa mtoto wako tayari kaisha pevuka, ila kuna muda inabidi iwe hivyo
Mfano:- mtu nimezaa nikiwa na miaka 18 (ilikuwa bahati mbaya na sikutaka abortion) baada ya hapo nikasema sasa nahitaji kurekebisha makosa, nikaamua kutulia kuanza kuandaa life langu kwanza (nikarudi school) ndio nije nizae tena hapo nakuja kusema sasa nahitaji mtoto wa pili nina miaka 35 mtoto wa kwanza kaisha vunja ungo tayari. Unazania nini kitatokea kwa kizazi hiki
 
Back
Top Bottom