Bado, gharama za harusi jamani, tafadhali

Bado, gharama za harusi jamani, tafadhali

Naomba usubiri, bado tunapambana, ikikaa vizuri utapata. Vipi una shughuli, au unajaribu kutaka kufahamu kuwa gharama ni ndogo mno za eneo hilo...

Tunayo ya kwetu tarehe 22.11.2014 mc nimeambiwa 350,000 na picha na video laki 400,000 ni hasara mkuu
 
Mpwa, ndio maana kila siku uko single, kumbe unaepuka haya

Ha ha ha..baada ya kukuonja nilimuacha mamsap wangu, afu ukakataa nikitangaza nia kwako...! Binamu nyama ya hamu ujue..!
 
Hii harusi nikisoma bajeti na mahitaji kama ya arusha vile
 
gharama zote zako au umeshirikisha wadau
 
Wakuu nilitoka kidogo, hata hapa nipo katika gari nimeingia tu kupitia simu. Naomba baadae nitoe ufafanuzi nikiwa katika kompyuta, poleni kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
 
Fanyia sherehe nyumbani kama kuna nafasi, utaokoa pesa nyingi tu.
Ikiwa lazima muende ukumbini, basi watu 50-80 wanatosha. Na ubook tables tu kwenye hoteli, chakula na vinywaji ndio gharama ya kukodi ukumbi. Yaani unabadili utaratibu kabisa wa typical wedding receiption. La tafuta bar inakosa wateja ndio ufanye ukumbi, owner watafurahi maana wataona umewaletea wateja.

Mawazo yako ni mazuri, kuna jamaa yangu kafunga harusi kwa misifa sasa hivi ana madeni mwili mzima na pesa hana, angetumia akili kidogo tu angeanza maisha ya ndoa bila stress za kutokuwa na pesa ndani.
 
Keki kama sijaiona hapo,halafu kuna haya ya kuzingatia:
Ukishaamua kufanya sherehe tena na Brass Band ipo basi ujue lazima cost itaenda juu.
1.Kama ni mapambo ukumbini wengi wanaanza laki 4
2.Music na MC nayo almost laki 4
3.Vinywaji sherehe nyingi wengi wanakunywa bia hata kama hapendi bia watakunywa Grand malt kitu ambacho inarudi kwenye gharama ya bia.
4.Magari kama hutatafuta ya marafiki zako ukae ukijua hizo bei zitapanda.
5.Still picha na moving pamoja huwa inarange laki 3 mpaka 4 na nusu bila projector.
Hii sherehe ukienda ukumbini lazima gharama ile kwako otherwise punguza watu au kafanyie mazingira ambayo hizo kumbi au bar wateja wamepungua basi anaweza kukupa kwa gharama ndogo.
Halafu hapo ukumbini kama vinywaji bei ni ghali,nunua hapo vichache hasa vile vya kopo vingine kanunue mtaani kwenye bei rahisi.Hapo Bar nunua vichache vya sample tu.
 
1. Chakula: watu 150
x 7000 (kwa kila sahani) = 1,050,000 .00
2. Vinywaji: Bia At least watu 50 watatumia bia x 3 @ x 2300Tshs =
345,000.00
Soda Watu 100 watakunywa soda x 3@ x 600Tshs =
180,000.00
3. Suti ya bwana harusi 150 000Tshs. x 1
= 150,000.00
4. Gauni la bibi harusi kukodi 150,000 Tshs x 1
= 150,000.00
5.Suti ya best man 150,000 x 1
= 150,000.00
6. Gauni la best woman 100,000 x 1
= 100,000.00
7.Kushona suti za watoto wasimamizi 4 x 25,000 =
50,000.00
8. Usafiri A. Gari ya bibi harusi 1 x 50,000
= 50,000.00
B.Gari ya bwana harusi 1x 50,000
= 50,000.00
C. Gari costa 2 kwa ajili ya ndugu x 60,000
= 120,000.00
9. Gharama ya Ukumbi 1 x 500,000
= 500,000.00
10. Gharama za upambaji 1 x 250,000
= 250,000.00
11. Gharama za kurekodi 1 x 200,000
= 200,000.00
12. Gharama za Shampeni 2 x 200,000
= 400,000.00
13. Gharama za guest 60,000
= 60,000.00
14. Mc na Muziki 200,000
= 200,000.00
15. Vipodozi bibi harusi 150,000
= 150,000.00
16. Blass Band 200,000
= 200,000.00

= 4,355,000.00


NDUGU WASHAURI WANGU, NI MIMI NILIYEOMBA USHAURI JUU YA UWEZEKANO WA
KUFANYA HARUSI YA TSHS. 2000,000 HAPA DAR ES SALAAM. MLINIONYESHA KUWA
HAKUNA KINACHOSHINDIKANA, ILA NI AINA GANI YA HARUSI NILIHITAJI NI SUALA
AMBALO MLINIACHIA.

NIMEENDELEA KUPAMBANA WAKUU, MWANAMKE HATAKI KUNIACHIA, NIMEKUBALI
KUPAMBANA.

BADO NARUDI KWENU WAKUU,HEBU KAGUENI VIFAA
NILIVYOTAJA HAPO JUU, NINI KIMEPUNGUA, JE HARUSI HAPO NIMEKAMILISHA.
NIBORESHE NINI, WAZEE KARIBUNI.
NATANGULIZA SHUKRANI


hapana garama kubwa bi harusi kama ana uwezo yeye na best wake ajitegemee. pole ukimaliza harusi nitafte tuvunje kamati.
 
Ndugu yangu umenigusa sana, ni kitu kinasumbua kichwa mpaka sasa kuna kitu najaribu kufanya. Nitawajuza kama nikifanikiwa kupitia hapa JF, yaani nafahamu kuna watu wanangoja hilo sana ili wapate hela.

Achana kabisa na mambo ya kamati
Washenzi sana wengi wao
Ndo hufanya sehemu ya kupiga hela hii
 
hapo bado garama za kuwarudisha wazaz/ndugu mkoan.
Je gest unakaa siku 1 tu
mara nyingi wanywaji wa bia ni wengi kuliko soda, nilitegemea wa bia wawe 100, wa soda 50.
 
Hizo cost naona kama hazina uhalisia kwa jiji la Dar....mfano ukumbi now days, Gari la maharusi,gharama ya suti, upambaji, gauni la bib harusi, MC

Pia cjana Cake hapo....gharama hizo unatafuta stress my frnd.
 
Tunayo ya kwetu tarehe 22.11.2014 mc nimeambiwa 350,000 na picha na video laki 400,000 ni hasara mkuu

Ndugu, unaweza endelea tu, utapoteza muda bure. huyu bwana ameniweka clear kwamba mc na mziki wake na shampeni 3 ingawa nita endelea bargaining ndio hiyo 350000. Endelea tu na utaratibu almost no difference
 
Back
Top Bottom