Badala ya kubishana majukwaani kudai katiba, kwanini Watanzania wote tusiungane kujadili jinsi ya kutatua tatizo la ajira nchini

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
930
1,000
Kwenu Watanzania wenzangu wa vyama vyote nchini,

Tunayo mengi ya kufanya lakini swala ajira linahitaji kujadiliwa kwa mapana na marefu na Watanzania wote, tusiwaachie wabunge peke yao wanao pokea mishahara kila mwezi.

Hili swala ni vyema likajadiliwa pia na watu wasio na ajira, wafanya biashara, wazee, watoto wa jinsia zote. Hapo ndipo tutakapoweza kupata suluhisho.

Kutegemea mbunge aliyeingia bungeni ili aajiriwe atoe mawazo yanayoweza kutatua tatizo la ajira Nchini ni kupoteza muda na wakati.

Mimi nina amini kuna watu wapo smart mtaani kuliko hata wabunge wetu. Nina hakika watu hawa wakipewa nafasi ya kutoa, hoja zao jinsi ya kutokomeza swala la ukosefu wa ajira Tanzania tutapata suluhisho.

Lakini wana siasa waliojipenyeza siasani baada ya kukosa ajira tusahau.

Watanzania tukae wote pamoja tujadili hili swala ili tutengeneze future za kizazi kijacho.

Hii nchi bado ni changa kuwa na hili tatizo la ukosefu ajira.

Rasilimali tunazo za kutosha, tumekosa watu smart ambao wanaweza kuzibadili rasilimali kuwa fursa.

Nawasilisha.
 
mgaka12

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
445
1,000
Tatizo la Ajara Tanzania linasababishwa na vitu vingi sana ikiwemo elimu yetu inachangia karibu 45%.. lakini tukienda deep down ajira zipo na zinatangazwa kila siku lakini watu awaombi hzo ajira wanasubr ajira za utumishi mfano zipo taasisi na makampuni, mabalozi za kimataifa wanatangaza ajira kutwa mpk zingine zinakuwa reposted kwa kukosa watu zipo nyingi sana mpk wanaamua kuajiri watu wenye vibali ya kufanya kazi Tanzania ambao ni wageni.

Sasa unajiuliza hv wenye madegree wanaolalamika hakuna kazi hawazioni hz ajira? Jibu ni dogo tu watanzania wanataka kufanya kazi ambayo Boss ni Mgogo,Msukuma etc utumishi wakitangaza ajira wanajazana kingine ni waoga wa kucompete au kwenye elimu yetu inamatatizo sehemu, mfano mdogo tu Ubalozi wa US wanatangazaga ajira ambazo haziitaji hata degree watu hawaombi inafikia kipindi wanaomba vibali vya kuajiri US veterans waliopo nchini.

Kingine Tanzania mnaamini kila mwenye degree anatakiwa kuajiriwa ndo maana wasomi wengi wanatafuta Degree kwa njia zozote ukiangalia tatizo la rushwa ya Ngono vyuoni ni kubwa kuliko Rushwa za Ngono sehemu yeyote ukizichanganya kwa pamoja. Sababu ni mtu apate Degree ambayo ukienda kwenye interview kwenye shirika au taasisi ambayo yanayojielewa mpk wanashangaa kinachotoka kichwani ni tofauti kilichoandikwa kwenye cheti.

Serikali inagalie Veta na vyuo vya ufundi tena watoe mpk mikopo watu wakasome vyuo vya ufundi kama ilivyo vyuo vya elimu ya juu kwa sababu mtu akisoma ufundi, mfano Ufundi Simu,Ujenzi,Umeme,Ufundi bomba, etc mtu anamaliza na kujiajiri mwenyewe na kuanza kulipa Deni kuliko kumpa mtu Mkopo ambao akimaliza ajira hakuna. Tatizo Veta yenyewe wanatoa kozi za kipuuzi kama ukonda kwenye magari sasa kozi ya ukonda inafaida gani nani naajiri koda kwa cheti?
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
11,062
2,000
Huwezi kutatua tatizo la ajiro kwa mfumo wa serikali uliopo. Katiba mpya ingeleta ugatuzi wa madaraka na uwahi kwa viongozi vilaza wasio na tija.Ya sasa haitoi hiyo fursa
 
Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
930
1,000
Tatizo la Ajara Tanzania linasababishwa na vitu vingi sana ikiwemo elimu yetu inachangia karibu 45%.. lakini tukienda deep down ajira zipo na zinatangazwa kila siku lakini watu awaombi hzo ajira wanasubr ajira za utumishi mfano zipo taasisi na makampuni...
Haya mawazo mazuri sana
 
comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
3,347
2,000
Kwenu watanzania wenzangu wa vyama vyote nchini:,

Tunayo mengi ya kufanya lakini swala ajira linahitaji kujadiliwa kwa mapama na, marefu na watanzania wote, tusiwaachie wabunge peke yao wanao pokea mishahara kila mwezi...
Kwenye hoja lama hizo CHADEMA huwaoni- hovyoooo
 
Ad majorem

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
529
1,000
Kila mtu ashinde mechi zake. Wanasiasa tunadai Katiba mpya tukiwa na Imani kuwa, itarahisisha shughuli za kisiasa ambayo ndio kazi yetu. Na ninyi vijana msio na kazi, Pambaneni na hali zenu.
 
Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
930
1,000
Kila mtu ashinde mechi zake. Wanasiasa tunadai Katiba mpya tukiwa na Imani kuwa, itarahisisha shughuli za kisiasa ambayo ndio kazi yetu. Na ninyi vijana msio na kazi, Pambaneni na hali zenu.
Swala la ajira sio kwa vijana tu ni kwa watanzania wote wa jinsia zote. We want to create a stable nation.
 
Solomon Ezekiel

New Member
Nov 29, 2020
4
20
Kwenu Watanzania wenzangu wa vyama vyote nchini,

Tunayo mengi ya kufanya lakini swala ajira linahitaji kujadiliwa kwa mapana na marefu na Watanzania wote, tusiwaachie wabunge peke yao wanao pokea mishahara kila mwezi.

Hili swala ni vyema likajadiliwa pia na watu wasio na ajira, wafanya biashara, wazee, watoto wa jinsia zote. Hapo ndipo tutakapoweza kupata suluhisho.

Kutegemea mbunge aliyeingia bungeni ili aajiriwe atoe mawazo yanayoweza kutatua tatizo la ajira Nchini ni kupoteza muda na wakati.

Mimi nina amini kuna watu wapo smart mtaani kuliko hata wabunge wetu. Nina hakika watu hawa wakipewa nafasi ya kutoa, hoja zao jinsi ya kutokomeza swala la ukosefu wa ajira Tanzania tutapata suluhisho.

Lakini wana siasa waliojipenyeza siasani baada ya kukosa ajira tusahau.

Watanzania tukae wote pamoja tujadili hili swala ili tutengeneze future za kizazi kijacho.

Hii nchi bado ni changa kuwa na hili tatizo la ukosefu ajira.

Rasilimali tunazo za kutosha, tumekosa watu smart ambao wanaweza kuzibadili rasilimali kuwa fursa.

Nawasilisha.
That's fact
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom