SoC03 Jinsi application ya simu inavyoweza kutatua tatizo la ajira nchini

Stories of Change - 2023 Competition
Jul 18, 2022
24
47
JINSI APPLICATION YA SIMU INAVYOWEZA KUTATUA TATIZO LA AJIRA - CAREER APPLICATION

Utangulizi
Upatikanaji wa ajira umekuwa ni changamoto kubwa kwa mataifa mengi duniani ikiwemo Tanzania. Hii ni kutokana na ongezeko kubwa la watu hususani vijana ambao huhitimu masomo yao huku nafasi za ajira zikiwa haziendani na ongezeko la wahitaji. Hali hii ni tofauti sana na miaka ya nyuma amapo wahitimu kutoka vyuoni walikuwa ni wachache sana na hivyo ilikuwa rahisi mtu kumaliza masomo na kuanza kazi moja kwa moja.

Taarifa kutoka TCU zinaonyesha ongezeko la wahitimu wa vyuo vikuu kwa kila mwaka ni wastani wa wahitimu 50,000 kwa mwaka huku mwaka 2021 pekee walihitimu wanafunzi 54,810. Idadi hii haijumuishi wanafunzi wanaohitimu vyuo vya kati kama vile VETA na NACTE na mafunzo mengine.

Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2022, mwaka 2021 watu wenye umri wa zaidi ya miaka 15 wasiokuwa na ajira walikuwa 2,324,887 sawa na asilimia 9.0. Kwa mujibu wa Benki ya dunia mwaka 2021 kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Tanzania ilikuwa ni 2.74%. Vyanzo vingine vinaeleza kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Tanzania ni zaidi ya 9.3% ikiwa ni kiwango cha juu zaidi ya Kenya, Madagascar na Zimbabwe.

Kuna sababu nyingi zinazopelekea vijana kukosa ajira ikiwa ni pamoja na kukosa taarifa kuhusu fursa za ajira, mfumo wa elimu usioendana na mahitaji ya wakati husika, kukosa ujuzi, mitaji na mafunzo ya biashara na ujasiriamali pamoja na kukosa watu wa kuwasemea - connections. Tatizo la ajira limefikia hatua likaitwa bomu ambalo muda wowote linaweza kulipuka.

Kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali kuhakikisha tatizo la ajira linapangua kama sio kuisha kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia programu mbalimbali za kilimo kama vile Building a Better Tomorrow (BBT), kutoa mafunzo ya kujiajiri vijana kupitia VETA, mikopo kwa wanawake na vijana, n.k. Pamoja na juhudi hizo zinazochukuliwa na serikali na wadau wengine bado kuna haja ya kuendelea kuchukua hatua kuwajibika kwa pamoja katika kupunguza ukubwa wa tatizo la ajira nchini.

MATUMIZI YA SIMU JANJA KUTATUA TATIZO LA AJIRA KUPITIA CAREER APPLICATION - CAREER APP. Miongoni mwa sababu zinazowafanya vijana wakose ajira ni kukosa taarifa za ajira pamoja na connection kati yao na waajiri - mashirika na taasisi mbalimbali nchini na duniani. Kuna taasisi zinaingia gharama kubwa kila wakati kwa ajili ya matangazo ya ajira/kazi na wakati mwingine huhitaji mfanyakazi wa haraka kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa wazi. Kwa sasa tovuti na mitandao ya kijamii wanatoa nafasi za watu kuomba ajira na hakuna Application ambayo ipo mahsusi kuwaunganisha waajiri na waajiriwa watarajiwa yenye taarifa zote za mwajiriwa.

CAREER APPLICATION itamsaidia mhitimu yeyote anayetafuta ajira kusajili taarifa zake zote za kitaaluma, majina yake, anuani zake, ujuzi, uzoefu na mambo mengine. Kupitia taarifa hizi mwajiri atakayehitaji mfanyakazi atakuwa na uwezo wa kuangalia mtu atakayemfaa kulingana na ujuzi anaouhitaji na kwa maana hiyo ataweza kumpigia simu au kumtumia ujumbe kwa njia ya e-mail ambayo aliitumia wakati anajisajili.

Vilevile, kampuni au taasisi husika (mwajiri) anatakiwa kujisajili kwenye mfumo taarifa sahihi ikiwemo anuani za makazi, ofisi na nyingine ili kuepuka suala zima la utapeli. Badala ya kila siku wahitimu kuwa wanaandika barua na kupeleka maofisini, Career App hii itapunguza usumbufu huo na hivyo basi mwajiri na mwajiriwa watapata fursa ya kubadilishana taarifa kupitia Application hii.

Pia, Career App itapunguza mjuano na kuongeza connection za ajira ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Kuna nchi nyingi zilijikita kwenye uzazi wa mpango na kusahau kama kuna uhitaji wa nguvu kazi siku za usoni kwa sasa zimejikuta zina wazee wengi kuliko vijana ambao ni nguvu kazi. Hii ni fursa muhimu sana na ili kuongeza tija na imani kwa Application hii, wizara inayohusika na masuala ya ajira kwa vijana na makundi mengine isimamie zoezi hili ili kuipa thamani na watu waiamini.

Serikali itengeneze Career Application ambayo itakuwa kama database na platform ya vijana kupata fursa za ajira ndani na nje ya nchi. Wakati mwingine taasisi au kampuni huajiri watu wasio sahihi kwa sababu hukosa watu wenye sifa. kwa mantiki hiyo, Application hii ambayo kila mwenye uhitaji wa ajira atalazimika kuwa nayo kwenye simu yake atakuwa na uwezo wa kuweka fani aliyosomea na hivyo hurahisisha upatikanaji wa wataalamu hitajika.

Kwa kawaida serikali inawajibika moja kwa moja kwenye suala la ajira kwa kuwa ina wajibu wa kufanya hivyo. Kwa kuwa serikali haina uwezo wa kumuajiri kila mmoja basi ina wajibu wa kuweka mazingira mazuri ya ajira kwa watu wake kupitia taasisi au wizara husika. Serikali iwatangazie umma na wadau wake wote kwamba Application ipo kwa mtu yeyote au taasisi au shirika litakalohitaji kuajiri basi wanaweza kutumia APPLICATION hii.

Kwa kufanya hivi itakuwa rahisi kuwakutanisha waajiriwa na waajiri kwa wakati mmoja na hivyo hupunguza tatizo la ajira nchini kwa kuwa baadhi ya vijana na wahitimu hukosa fursa ya ajira kwa kukosa connection na taarifa sahihi za ajira mpya.

Ikiwa utavutiwa na andiko hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza neno vote then utakuwa umepiga kura yako.
 
Kuna platform kama upwork, thirdchannel, freelancer, latium etc
Mi nilipata kaz ya mechandiser marekani katika kampuni ya adidas(but sikwenda)
Yeah inawezekana kabisa kikubwa watu wahakikishiwe usalama wao wa kimtandao wasije pigwa. Usisahau kunipigia kura sasa ndugu yangu..
 
JINSI APPLICATION YA SIMU INAVYOWEZA KUTATUA TATIZO LA AJIRA - CAREER APPLICATION

Utangulizi
Upatikanaji wa ajira umekuwa ni changamoto kubwa kwa mataifa mengi duniani ikiwemo Tanzania. Hii ni kutokana na ongezeko kubwa la watu hususani vijana ambao huhitimu masomo yao huku nafasi za ajira zikiwa haziendani na ongezeko la wahitaji. Hali hii ni tofauti sana na miaka ya nyuma amapo wahitimu kutoka vyuoni walikuwa ni wachache sana na hivyo ilikuwa rahisi mtu kumaliza masomo na kuanza kazi moja kwa moja.

Taarifa kutoka TCU zinaonyesha ongezeko la wahitimu wa vyuo vikuu kwa kila mwaka ni wastani wa wahitimu 50,000 kwa mwaka huku mwaka 2021 pekee walihitimu wanafunzi 54,810. Idadi hii haijumuishi wanafunzi wanaohitimu vyuo vya kati kama vile VETA na NACTE na mafunzo mengine. Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2022, mwaka 2021 watu wenye umri wa zaidi ya miaka 15 wasiokuwa na ajira walikuwa 2,324,887 sawa na asilimia 9.0. Kwa mujibu wa Benki ya dunia mwaka 2021 kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Tanzania ilikuwa ni 2.74%. Vyanzo vingine vinaeleza kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Tanzania ni zaidi ya 9.3% ikiwa ni kiwango cha juu zaidi ya Kenya, Madagascar na Zimbabwe.

Kuna sababu nyingi zinazopelekea vijana kukosa ajira ikiwa ni pamoja na kukosa taarifa kuhusu fursa za ajira, mfumo wa elimu usioendana na mahitaji ya wakati husika, kukosa ujuzi, mitaji na mafunzo ya biashara na ujasiriamali pamoja na kukosa watu wa kuwasemea - connections. Tatizo la ajira limefikia hatua likaitwa bomu ambalo muda wowote linaweza kulipuka. Kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali kuhakikisha tatizo la ajira linapangua kama sio kuisha kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia programu mbalimbali za kilimo kama vile Building a Better Tomorrow (BBT), kutoa mafunzo ya kujiajiri vijana kupitia VETA, mikopo kwa wanawake na vijana, n.k. Pamoja na juhudi hizo zinazochukuliwa na serikali na wadau wengine bado kuna haja ya kuendelea kuchukua hatua kuwajibika kwa pamoja katika kupunguza ukubwa wa tatizo la ajira nchini.

MATUMIZI YA SIMU JANJA KUTATUA TATIZO LA AJIRA KUPITIA CAREER APPLICATION - CAREER APP. Miongoni mwa sababu zinazowafanya vijana wakose ajira ni kukosa taarifa za ajira pamoja na connection kati yao na waajiri - mashirika na taasisi mbalimbali nchini na duniani. Kuna taasisi zinaingia gharama kubwa kila wakati kwa ajili ya matangazo ya ajira/kazi na wakati mwingine huhitaji mfanyakazi wa haraka kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa wazi. Kwa sasa tovuti na mitandao ya kijamii wanatoa nafasi za watu kuomba ajira na hakuna Application ambayo ipo mahsusi kuwaunganisha waajiri na waajiriwa watarajiwa yenye taarifa zote za mwajiriwa.

CAREER APPLICATION itamsaidia mhitimu yeyote anayetafuta ajira kusajili taarifa zake zote za kitaaluma, majina yake, anuani zake, ujuzi, uzoefu na mambo mengine. Kupitia taarifa hizi mwajiri atakayehitaji mfanyakazi atakuwa na uwezo wa kuangalia mtu atakayemfaa kulingana na ujuzi anaouhitaji na kwa maana hiyo ataweza kumpigia simu au kumtumia ujumbe kwa njia ya e-mail ambayo aliitumia wakati anajisajili. Vilevile, kampuni au taasisi husika (mwajiri) anatakiwa kujisajili kwenye mfumo taarifa sahihi ikiwemo anuani za makazi, ofisi na nyingine ili kuepuka suala zima la utapeli. Badala ya kila siku wahitimu kuwa wanaandika barua na kupeleka maofisini, Career App hii itapunguza usumbufu huo na hivyo basi mwajiri na mwajiriwa watapata fursa ya kubadilishana taarifa kupitia Application hii.

Pia, Career App itapunguza mjuano na kuongeza connection za ajira ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Kuna nchi nyingi zilijikita kwenye uzazi wa mpango na kusahau kama kuna uhitaji wa nguvu kazi siku za usoni kwa sasa zimejikuta zina wazee wengi kuliko vijana ambao ni nguvu kazi. Hii ni fursa muhimu sana na ili kuongeza tija na imani kwa Application hii, wizara inayohusika na masuala ya ajira kwa vijana na makundi mengine isimamie zoezi hili ili kuipa thamani na watu waiamini. Serikali itengeneze Career Application ambayo itakuwa kama database na platform ya vijana kupata fursa za ajira ndani na nje ya nchi. Wakati mwingine taasisi au kampuni huajiri watu wasio sahihi kwa sababu hukosa watu wenye sifa. kwa mantiki hiyo, Application hii ambayo kila mwenye uhitaji wa ajira atalazimika kuwa nayo kwenye simu yake atakuwa na uwezo wa kuweka fani aliyosomea na hivyo hurahisisha upatikanaji wa wataalamu hitajika.

Kwa kawaida serikali inawajibika moja kwa moja kwenye suala la ajira kwa kuwa ina wajibu wa kufanya hivyo. Kwa kuwa serikali haina uwezo wa kumuajiri kila mmoja basi ina wajibu wa kuweka mazingira mazuri ya ajira kwa watu wake kupitia taasisi au wizara husika. Serikali iwatangazie umma na wadau wake wote kwamba Application ipo kwa mtu yeyote au taasisi au shirika litakalohitaji kuajiri basi wanaweza kutumia APPLICATION hii.
Kwa kufanya hivi itakuwa rahisi kuwakutanisha waajiriwa na waajiri kwa wakati mmoja na hivyo hupunguza tatizo la ajira nchini kwa kuwa baadhi ya vijana na wahitimu hukosa fursa ya ajira kwa kukosa connection na taarifa sahihi za ajira mpya.

Ikiwa utavutiwa na andiko hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza neno vote then utakuwa umepiga kura yako.
Karibu na hapa Thread 'Lugha ya Taifa(Kiswahili Sanifu) hatarini kuanguka' SoC03 - Lugha ya Taifa(Kiswahili Sanifu) hatarini kuanguka
 
Back
Top Bottom