Babu Seya na Wanae kusota Jela Maisha!

Babu Seya na Wanae kusota Jela Maisha!

Jibu ni hili. Kama unataka kujuwa ukweli kuwa JK ni nani kwa mademu hapa mjini, jaribu kumtongoza Vicky Kamata kisha njoo kutusumulia hapa JF nini kilikusibu baada ya JK kujuwa hilo, ama Vicky Kamata alikuambia nini wakati unamtongoza? Very simple.
..Hawa watu sio kwamba hawasomi hizo docment tu.. hata wakizisoma hawaamini hayo yalio andikwa. Imani yao ni hiyo tu kuwa Nguza na papii wamaonewa na hawakustahiki kuadhibiwa..lakini hawasemi kwanini hawakustahiki kudhibiwa. Na ukiwauliza wamekosea nini mpaka wakaadhibiwa tofauti na makosa haya yanayosomeka humu. hawana majibu yenye ushahidi hata unao fanana.mm nawasikitikia sana watu wanao amini kama nguza na papii wameonewa.kesi yao imesikilizwa mara 4 tofauti na mahakim na majaji tofauti mote wamewatiwa hatiani sasa tuamini hawa wote walio sikiliza kesi yao wanawachukia achilia mbali mawakili wangapi wamewatetea bado tuu hamuamini kama kama wamepewa adhabu stahiki..basi munao jua ukweli tofauti na ule ulioelezwa mahakama zote jitokezeni mutueleze na kama kweli mutatuaminisha kama ni ukweli tutafuta njia tumuobe mh rais awasamehe.tutakwenda kawa baba askofu pengo na mufti simba tuwaombe wamuombe mh rais awasamehe.leteni ushahidi wa nguza na pii wp wameonewa.
 
yani watu wana ongea kwa hisia wakati documents za hukumu na appeal ziko humu jukwaa la siasa na ziliwekwa hili watu wasome lakini cha kushangaza watu hawasomi wana baki kuongea kwa kutumia hisia.

Uzuri kwenye hizo documents kila kitu kiko wazi kuna facts na evidence za kutosha.

Mkuu nimepitia hizo documents.....Daah ushahidi umewekwa na victims live kabisa....Sijui kwa nini watu hawapendi kusoma?
Watoto 10 waseme Uongo (bila kuchanganyana) mbele ya Mawakili, Mahakama n.k Rehearsal ya aina gani ilihitajika mpaka waweze kukariri??
Watu wanafikiri kundi la watu 10 kubuni uongo na kuutetea mahakamani ni rahisi tu sembuse kwa Watoto??
Watoto wamewatambua watuhumiwa bila Shaka pamoja na kuelezea mazingira ya nyumba/chumba walichokuwa wanafanyiwa ubakaji (ikiwemo kubainisha vitu vilivyopo chumbani kwa usahihi)
Kwa ushahidi uliowekwa Sioni namna akina Babu Seya wangeshinda,hata wangekata rufaa Mara 1000........
KWANZA NIMESHANGAA HUKUMU NYEPESI WALIYOPEWA......
 
Angelawitiwa MWANAO ungekuwa NA HII HURUMA ya KUOMBA Waachiwe HURU???
 
Hao Majaji wamejibu vipi hoja hii?

Kwa upande wao mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP) waliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwasababu sababu zote alizozitoa jana ni sababu ambazo alizitoa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februali mwaka 2010. Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari , basi angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na siyo ombi lake kuja kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu ile ambayo Marando anadai ina dosari. “Hoja za Marando ni za kirufaa, na hoja zake zote anazotaka kuonyesha hukumu ya mahakama hii ina dosari zilishaamriwa na mahakama hii wakati ikisiliza rufaa ya wateja wake mwaka 2010 na tunamtaka Marando aelewe kuwa hakuna maamuzi yasiyonamwisho hivyo sisi tunaomba ombi la Marando linalotaka mahakama hii ifanyiwe mapitio hukumu yake halina msingi”
 
nadhani watanzania wanaongozwa kwa hisia na mahaba binafsi na wasanii hawa kutoka na mvuto wao katika tansia ya muziki kwani ukichunguza nusu au asilimia karibu 70 wanaosema wameonewa watolewe gerezani mosi hawajawahi kudhuria au kusoma ile kesi ya awali pale kisutu 2.hawajawahi hata kupitia nakala ya huhumu au hata kufuatilia sababu za kufungwa kwao pale 3.hawajawahi kusoma kupitia au hata kuoona nakala ya hukumu ya jaji mihayo pale hight court ambayo ilikazia hukumu ya mahakama ya kisutu wala kusikia kwa mtu aliyeisoma zaidi ya vichwa vya habari vya magazeti na post za kishabiki zenye maono binafsi 4. hawajui sababu zilizowatoa wale 2 francis chichi nguza na nguza mbangu pale nahakama ya rufaa. wanegi tunazungumza opinion na ushabiki labda niwajuze hakuna mtu yoyote wala chuo chochote duniani kinachoweza kuwafunza watoto 9 kati ya 12 watoe ushahidi ulinyooka wakiwa cross examined na mawakili zaidi ya 3 wazoefu lazima wangepishana tu maelezo yao yanekuwa collarobareted na ripoti ya daktari na wazazi wao yupo mtoto mmoja ukiskiliza story yake wewe ukiwa mzazi unaweza ukakosa usingizi so nawashauri tuache kutia mahaba kwenye hizi mambo mimi nimezishudia nyingi sana sema hii ni maarufu sana ndo maana iko hivi naamini wengi humu mnajua zipo kesi za kubaka mnasema kabisa kama bora afungwe mmbakaji huyo pasipo kusikiliza facts za upande wa pili lakini kesi hii mnatanguliza hukumu zenu kabla ya kujua facts nashangaa sana.mkisoma gazeti la majira la juzi kuna watoto wa 4 mbeya wamebakwa na mchungaji wa pentekoste kigoma this year kuna sheikh amefungwa kwa kesi kama hiyo sasa ndo itakuwa watu wa dunia kama sisi acheni mapenzi acheni kuamini watu kwa watoto wenu kuna hatari kubwa sana
 
Kwa upande wao mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP) waliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwasababu sababu zote alizozitoa jana ni sababu ambazo alizitoa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februali mwaka 2010. Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari , basi angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na siyo ombi lake kuja kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu ile ambayo Marando anadai ina dosari. "Hoja za Marando ni za kirufaa, na hoja zake zote anazotaka kuonyesha hukumu ya mahakama hii ina dosari zilishaamriwa na mahakama hii wakati ikisiliza rufaa ya wateja wake mwaka 2010 na tunamtaka Marando aelewe kuwa hakuna maamuzi yasiyonamwisho hivyo sisi tunaomba ombi la Marando linalotaka mahakama hii ifanyiwe mapitio hukumu yake halina msingi"

Point yao ilikuwa na msingi zaidi, kwa hiyo marando alikuwa anategemea hao majaji wangekula matapishi yao?
 
May the following verses be a comfort for Nguza, his son and all well wishers:

Greatly have they afflicted me from my youth, let Nguza Viking and his son now say,
YET they have not prevailed against me!
The plowers plowed upon my back; they made long their furrows.
But the Lord is righteous;
he has cut the cords of the wicked.
May all who afflicted Nguza and Papii
be put to shame and turned backward in a broad day light!
Let them be like the grass on the housetops,
which withers before it grows up,
with which the reaper does not fill his hand
nor the binder of sheaves his arms,
nor do those who pass by say,
The blessing of the Lord be upon you!
We bless you in the name of the Lord!”
 
hakuna ukweli familia ikabaka kuanzia baba mpaka watoto wa chini kabisaa, hizi ni hukumu za kipirato zinazoamuliwa na walio juu ya sheria, chuki binafsi za mapenzi zinazofanywa na wakuu wasio na huruma hata chembe, mwanadamu anageuka kuwa mungu mtu anaamuru fulani afungwe maisha na inakuwa hivyo, dhambi mbaya sana hii kuzima ndoto za mwenzako, na kumpa mateso ya maisha, kama walibaka yule mwalimu aliyekuwa anasemekana alikuwa anapewa hela ya kuwapa wale watoto ili waende kwa babu seya yu wapi mbona aliachiwa huru? Mwlimu huyu alikuwa akifundisha pale mbuyuni, inauma sana ukweli tunaujuwa na hawa mahakimu wenye kutekeleza amri za mabwana zao wanaowapa nafasi hizi wamekuwa ni watu wanaotoa hukumu kwa maagizo, shame on u stupid judges, taaluma yenu iko wapi kama mnafanyishwa kazi kwa remort? Kweli usije ukala cha mkubwa. Inauma sana

ukweli unaujua unawaacha wandugu wanaumia jela maisha? Hakika nawe hutaachwa kuhesabiwa dhambi za mateso za hawa ndugu kama kweli hawakutenda
 
Mheshimiwa Rais Kikwete tunaomba utumie busara zako, wasamehe watu hawa kwa msamaha maalum. Hakika inawezekana walitenda kosa ila wameshaonja adhabu yake. Wasamehe, wahame nchi warudi kwao maisha. Hakika ninafikiri kuwasamehe au angalao wafungwe 30 years ili hata mwanae aweze kutoka baadaye. Oneni huruma sana. Sishabikii ubakaji ila pia tuone huruma, tuwafunge kifungo cha wabakakaji, hata hiyo 30 years inatosha kuwashikisha adabu.

Mimi kama mwanamke nimejiingiza kwenye kiatu cha mwanamke mwenzangu aliyelawitiwa wanawe,
maombi yangu kwa rais ni kuwa,kama kweli walilawiti watoto mheshimiwa rais naomba wafungwe maisha au ikibidi wanyongelewe mbali ili iwe fundisho kwa mashetani wenzao.
Msiba kwa jirani.
 
Ndugu kwanza ondoa neno kubaka katika kesi hii ya akina Babu Seya wao wameshitakiwa kwa kuwanajisi yaani KUGUSISHA UUME KWENYE UKE wa wale watoto pasipo kuingiza lakini cha ajabu kifungo cha maisha na wale wanaobaka na kuuingiza kabisa uume wanahukumiwa kifungo kisichozidi miaka 30. na cha ajabu katika eneo lile inasemekana wale watoto wamehamishwa eneo hilo tangu kutolewa kwa ile hukumu na haijulikana wamepelekwa wapi, nahisi inawezekana wengine wamepelekwa kusoma nje ya nchi.
Acha kuropoka wewe.....akigusishwa wa kwako ndio utafurahia wakipewa kifungo cha miaka 3 na utaendelea kumwacha asome hapo hapo akili yake ikae vizuri kisaikologia... Lile ni donda moyoni mwa mtoto usipo kuwa makini maisha yake yote........
 
Anaweza kutoka akawa huru, lakini si chini ya jua hili linalowaka katika anga hili. asubili jua katika anga jingine
 
wazee huwa wanasema mke wa mtu sumu tatizo babu seya alijifanya maziwa kilichotokea ni kisasi atapata unafuu wa kesi yake labda mbaya wake afe.
porojo hizi tushazichoka, mnatapatapa. Mahakama ilitenda na imetenda haki......nitafurahi kama watafia jela...."baba na mwana wanaimba segerea"
 
ukweli unaujua unawaacha wandugu wanaumia jela maisha? Hakika nawe hutaachwa kuhesabiwa dhambi za mateso za hawa ndugu kama kweli hawakutenda

ha ha ha ha we ni kiboko !! katika wote niliofuatilia uzi wao
 
Atamuachia thru msamaha wa Rais 2005 akiwa anang'atuka, tutashauriana awekwe kwenye proposal list.....
 
hii kesi kila mtu anasema yake ila kama kweli walionewa kwa nini hata siku moja hawajawahi kusema hadharani ama na wenzao huko jela kuwa sababu ya sisi kuhukumiwa kwa sababu ya fulani....period
 
hii kesi kila mtu anasema yake ila kama kweli walionewa kwa nini hata siku moja hawajawahi kusema hadharani ama na wenzao huko jela kuwa sababu ya sisi kuhukumiwa kwa sababu ya fulani....period

Time will tell!
 
Back
Top Bottom