Babu Seya na Wanae kusota Jela Maisha!

Babu Seya na Wanae kusota Jela Maisha!

Bubu Msemaovyo

Platinum Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,552
Bila shaka kuna members wa JF wapo Mahakama ya Rufaa wakifuatilia hukumu hii ambayo Watanzania wengi wanaisubiri kwa hamu kubwa kusikia Babu Seya, Papii Kocha wako huru,


I am +VEly thinking of these men to be FREE. Praise the Lord.

Amen.

--------------
Mahakama ya Rufaa Tanzania imetupilia mbali rufaa ya Mwanamuziki Nguza Viking maarufu Babu Seya na mwanae Johnson Nguza na imewahukumu kuendelea kutumikia kifungo cha maisha kwa makosa ya kubaka na kulawiti RADIO1 STEREO

Mahakama kuu imetupilia mbali hoja zote zilizokua zikipinga hukumu dhidi ya mwanamziki Nguli Babu na mwanae na kuamuru aendelee kutumikia kifungo cha maisha jela kama ilivokuwa imeamriwa awali na mahakama hiyo.

Hukumu hiyo imekuwa mwiba mchungu wenye Sumu kwa mashabiki wa wanamziki hao waliokuwa wanategemea wasanii hao wataachiwa huru au kuwapunguzia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Source : TBC

Mwanamziki mkongwe nchini Nguza Viking aka Babu Seya na mwanaye Papii Kocha, wataendelea na kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufani nchini kuitupilia mbali rufaa yao iliyosikilizwa leo


Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara lakini wakagonga mwamba. Hukumu hii ya rufaa ndiyo ya mwisho kusikilizwa.



 
jk ameenda nje ya nchi ili akitoka asisikie,kwa sababu itamuuma sana.
 
surely,i pray them.hata mimi mwenyewe naombea watoke,wawe huru.pia ningependa kujua kuhusu wale watoto wanaodaiwa kufanyiwa unyambilisi,nadhani kwa sasa wameshakuwa watu wazima,wanaweza kusema kama ni kweli si kweli walifanyiwa hivyo
 
naamini watapewa kifungo cha miezi 3 au mwaka mmoja jela .



Naomba mungu adhabu yao isizidi hapo.
 
Kweli siamini kabisa baba na mwanawe wanaweza kufanya ubakaji kwa pamoja. Hiyo wanaweza wanyama tu lakini sio binadamu.
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Penye ukweli uongo ujitenga ngoja tusubiri na tuone.
 
AkyaMungu hii nchi imelaaniwa......kwa nini wanatesa watoto wa watu lakin? ol z well, tunaamin watatoka tu
 
Wabakaji hao wafungwe maishaaaa,angekuwa mCCM mngekuwa na maneno menf kisa msaniii mnaanza bwabwaja
 
Endeleeni kuomba kwani hukumu imetolewa na rufaa imetupwa so watakua kule segerema maisha yao yote
 
Mahakama ya Rufaa Tanzania imetupilia mbali rufaa ya Mwanamuziki Nguza Viking maarufu Babu Seya na mwanae Johnson Nguza na imewahukumu kuendelea kutumikia kifungo cha maisha kwa makosa ya kubaka na kulawiti RADIO1 STEREO
 
Back
Top Bottom