Babu Seya na Wanae kusota Jela Maisha!

Babu Seya na Wanae kusota Jela Maisha!

Humu kwenye JF nashindwa kuelewa watu mna agenda za kisiasa au chuki binafsi kwa watu fulani. Nasema hivi kwa sababu inakuwaje wengi sana humu mnaona kwamba Nguza na Mwanae wameonewa hawakubaka wala kulawiti, wakati huo huo wengi mnaamini kwamba Mzee Kapuya kabaka na anastahili kuadhibiwa??!!!

Kwa nini inakuwa hivi?

Hapo nilipoweka BLUE kama sikosei wakati kesi ikiendela wakati ule iligundulika wale watoto hawajaingiliwa lakini sheria ikageuka wakasema hata kuugusisha uume kwenye uke ni kunajisi na hivyo wakaendelea kuwatia hatiani hawa watu, leo Jaji anasema waliwaingilia tuegemee upande upi?

[h=2]Jaji aliyemhukumu Babu Seya ajitetea[/h]


BY MWANDISHI WETU



16th September 2011


email.png

Email



printer.png

Print



comment_bubble.png

Comments








Mihayo.jpg

Mwenyekiti wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji mstaafu, Thomas Mihayo, akionesha vitabu vya ripoti ya Vyombo Habari, wakati alipokuwa akiizindua, Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Machapisho na Utafiti, John Mireny.


Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Thomas Mihayo, jana aliukana uvumi ulioenea kuwa, kiongozi mmoja mkubwa wa serikali aliwashinikiza majaji ili watoe hukumu ya kifungo cha maisha kwa mwanamuziki mashuhuri nchini, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na watoto wake.
"Hakika si kweli…Niliupitia mwenendo wa kesi hiyo na kubaini kwamba kilichokuwa kinasemwa mitaani kilikuwa ni uvumi usiokuwa na chembe ya ukweli," alisema Jaji Mihayo alipokuwa akizindua rasmi Ripoti ya Ufuatiliaji wa Vyombo vya Habari vya magazeti (Julai 2010-Juni 2011) ya Baraza la Habari la Tanzania (MCT) jana jijini Dar es Salaam.
"Na cha kushangaza, vyombo vya habari vilikuwa vikiutangaza uvumi huu," aliwaambia waandishi wa habari.
Jaji Mihayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT, alisema aliusoma kwa kina mwenendo wa kesi ya kulawiti dhidi ya Babu Seya na wanawe kama ulivyoandaliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kabla ya kutoa hukumu ya mwisho.
Alisema kwa kuwa Mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kuamua kuhusiana na shauri hilo, ilipokea ukweli wa mwanzo wa shauri hilo na ikauwasilisha Mahakama Kuu.
"Kwa kweli ni mimi ndiye nilikuwa mwenyekiti wa kesi hiyo kama Jaji wa Mahakama Kuu na ndiye niliyetoa hukumu ya mwisho (ya kumhukumu Babu Seya na wanaye kifungo cha maisha)," alisema.
Alisema wakati akizisoma nyaraka na mwenendo wa kesi toka katika mahakama hiyo ya chini (Mahakama ya Kisutu), aligundua kwamba kilichokuwa kikisemwa na watu mitaani ulikuwa ni uvumi tu.
"Si kweli kwamba kulikuwa na ofisa mmoja mkubwa katika duru za serikali ambaye alitoa shinikizo kwa Majaji lililowafanya wafikie kwenye tamati hiyo ya kumhukumu Babu Seya na wanaye kifungo cha maisha," alisema.
Jaji Mihayo alisema alitenga muda wa kuongea na watoto wasichana waliodaiwa kubakwa na Babu Seya na wanawe na akagundua kwamba watoto hao walikuwa wamelawitiwa na kwamba tendo hilo lilikuwa limefanywa kwa kipindi cha miezi kadhaa.
Alisema aliwasikiliza watoto hao na akapata picha kamili ya kilichoendelea katika matukio hayo na pia aligundua kwamba wazazi wa watoto hao hawakuwa wanajua mwenendo wa watoto wao.
Alifafanua kwamba baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vikitoa ripoti isiyo sahihi ya kesi hiyo na akasema kwamba kama waandishi wangefanya uandishi wa kiuchunguzi, wangeweza kupata ukweli wa tukio hilo.
"Kibaya ni kwamba waandishi hawakulichunguza tukio hilo kiundani, vinginevyo wangeweza kupata ukweli wenyewe," alisema Jaji Mihayo.
Alisema uandishi wa kiuchunguzi unakosekana Tanzania na akawaomba wanachama wa vyombo vya habari nchini kusoma hiyo ripoti mpya ya ufuatiliaji wa vyombo vya habari vya magazeti iliyozinduliwa na MCT kwa nia ya kubaini mapungufu yao katika eneo la kuripoti habari za uchunguzi na kuyasahihisha.
Pamoja na hayo, Jaji Mihayo, aliipongeza MCT kwa kufuatilia kwa kina mwenendo wa kitaalamu wa wataalamu wa vyombo vya habari na kuja na ripoti pana na ya kina inayojumuisha masomo mengi…uhuru wa vyombo vya habari, masuala ya kijinsia, walemavu, maadili ya waandishi wa habari, mchakato wa mapitio ya katiba na kadhalika.
"Ninawaasa wataalamu wa vyombo vya habari kuwasaidia watu wanaoishi vijijini, walemavu na wale walio katika makundi ya pembezoni ili waweze kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato wa mapitio ya katiba," alisema. Hivi sasa Babu Seya na mwanaye mmoja, wanatumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kuwalawiti watoto wanafunzi wa kike.
Hata hivyo, washtakiwa wawili waliachiwa huru na Mahakama ya Rufani.
Kwa upande wake, John Mirenyi ambaye ni Meneja wa MCT anayeshughulika na uchapaji, utafiti na nyaraka, alisema kimsingi ufuatiliaji wa vyombo vya habari ni tathmini ya weledi na ufanisi wa maadili wa vyombo hivyo.
Alisema matokeo ya ufuatiliaji huo yatashirikisha wadau wa nje kwa lengo la kuchambua uzito wa ufanisi na mapungufu yake toka kwenye jicho la wataalamu wenyewe



​
 
Umeongea la maana Zogwale, hata mimi naungana na wewe. Naamini wengi humu jf kinachowafanya waongee hoja zisizo na mashiko ni kwa sababu wanawaonea huruma hawa mabwana. Kimsingi hata mm nawaonea huruma sana na niungane na wewe kuwatakia msamaha hawa jamaa kwani watakuwa wamejifunza, naamini hivyo. Kilichobaki ni RAIS pekee anayeweza kutia mkono wake wa huruma ili wasamehewe, japo kuna wajinga humu wanampaka matope. Usiwasikilize wapuuzi wasiojua sheria, badala yake ONA HURUMA na MUNGU kesho atakuhurumia wewe pia ktk yale ulomkosea.

Ni kweli tupu mkuu wangu, unajua hujafa hujaumbika!!! Huu msemo una siri kubwa sana. Kila binadamu anakutana na masahibu kwa aina yake, yasipokupata wewe yatampata mzazi, ndugu, mtoto au hata mjukuu. Kwa mantiki hii tusipende sana kushabikia makosa kwa kuwa hujui kesho na kesho kutwa wewe unaweza hata ukiwa kazini ukapakaziwa kosa la uhaini au uhujumu uchumi na ikakupelekea ukae jela maisha na huku hukulitenda kosa lile. Pia yawezekana kosa likawa la kweli ila pia kuna kuomba rehema za Mungu na kupata msamaha. Ninachoomba hata ni kwamba hata kama watafungwa basi iwe ni ile adhabu ya miaka 30 ya wabakaji wengine wote ambao walibaka minor au hata wakubwa. Rais wa nchi yetu tunaamini ni mtu wa huruma, basi amhurumie huyu mzee apate miaka 30 na mwanawe na itapungua kwa kuwa walishatumikia kadhaa. Hata kama huu mzee seya atafia huko kabla ya 30 but tuna hakika mwanaye atatoka hata na miaka 40s or 50s. Hii nayo ni adhabu tosha na itakuwa fundisho kwa wengine.
 
Mwanamziki mkongwe nchini Nguza Viking aka Babu Seya na mwanaye Papii Kocha, wataendelea na kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufani nchini kuitupilia mbali rufaa yao iliyosikilizwa leo


Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara lakini wakagonga mwamba. Hukumu hii ya rufaa ndiyo ya mwisho kusikilizwa.



 
Kitu ambacho nashindwa kuelewa nikwamba nasikia huyu binti wa kubakwa na Kapuya eti alikuwa shahidi kwenye kesi ya Babu Seya. Binafsi nahisi huyu Babu Seya kaonewa.

Kama babu seya kaonewa inakuwaje kapuya iwe hakuonewa??? wana jf tuwe great thinkers sio wanasiasa jamani
 
Kama walitenda hiyo ni stahili yao,na kama wamesingiziwa bac malipo mazuri yanawasubir akhera!
 
Ni kweli tupu mkuu wangu, unajua hujafa hujaumbika!!! Huu msemo una siri kubwa sana. Kila binadamu anakutana na masahibu kwa aina yake, yasipokupata wewe yatampata mzazi, ndugu, mtoto au hata mjukuu. Kwa mantiki hii tusipende sana kushabikia makosa kwa kuwa hujui kesho na kesho kutwa wewe unaweza hata ukiwa kazini ukapakaziwa kosa la uhaini au uhujumu uchumi na ikakupelekea ukae jela maisha na huku hukulitenda kosa lile. Pia yawezekana kosa likawa la kweli ila pia kuna kuomba rehema za Mungu na kupata msamaha. Ninachoomba hata ni kwamba hata kama watafungwa basi iwe ni ile adhabu ya miaka 30 ya wabakaji wengine wote ambao walibaka minor au hata wakubwa. Rais wa nchi yetu tunaamini ni mtu wa huruma, basi amhurumie huyu mzee apate miaka 30 na mwanawe na itapungua kwa kuwa walishatumikia kadhaa. Hata kama huu mzee seya atafia huko kabla ya 30 but tuna hakika mwanaye atatoka hata na miaka 40s or 50s. Hii nayo ni adhabu tosha na itakuwa fundisho kwa wengine.

Nakubaliana na wewe 100%. Tena katika marais nilopata kuwaona wenye HURUMA, hekima na busara ni rais wetu wa sasa. Awahurumie hawa mabwana, wameshajifunza kama walikosea
 
Dahh!!! rufaa ya mwisho kusikilizwa..... pole zao jamani... Labda wanaweza pewa msamaha unaotolewaga na rais.
 
Duh kaka mkubwa hana huruma kabisa. Napata wasiwasi,nahisi babu seya alikuwa hadi 0712 haiwezekana jamaa akawa na hasira hivyo.
 
Kapuya anapeta Huku akisambaza ukimwi Huku kova akisema ni suala binafsi lakini la wakina babu seya ni kosa la jinai
 
Hivi unapomfunga mtu kifungo cha maisha, nia huwa ni kuachieve nini?
 
"Walipakaziwa kesi wamenajisi watoto wakafungwa bila hatia hukumu za kipilato."
 
Mwanamziki mkongwe nchini Nguza Viking aka Babu Seya na mwanaye Papii Kocha, wataendelea na kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufani nchini kuitupilia mbali rufaa yao iliyosikilizwa leo


Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara lakini wakagonga mwamba. Hukumu hii ya rufaa ndiyo ya mwisho kusikilizwa.



Wakuu hawa wanaolia nani zao sasa make najua hawa watenda kosa siyo watanzania wao wamewajulia wapi mpaka machozi yote hayo yatoke.
 
Kweli nimekubali vya wakubwa usiguse, Ila msichoke kumuomba Mungu kwani inawezekana 2015 mkatoka baada ya hawamu ya shetani kutawala kuisha.
 
Back
Top Bottom