Babie Kabae na Udini Clouds Tv

mpya hiyo
 
Yule mshikaji nilikuwa namtazama sana katika vipindi vya dr elie wanachomekea sana sio uongo,ila mm nilikuwa sikereki najua ndo makuzi wamekulia katika dini hiyo nnasikiliza yanayonihusu,ila yeye akichomeka tu wanaanza lawama.
 
Ijumaa saa kumi na moja asubuhi mbona pia kuna kipindi cha uislamu...mleta mada yupo sawa kipindi kinatazamwa na watu mbalimbali na wengine hata dini hawana,so ni vizuri kuepusha kuzungumzia dini..
Hule co msimamo Clouds Tv n msimamo wake mwenyewe kwa faida yake mwenywe. Kila mda na kila saa mtangulize Mola wako na njia/Mapito yko yatakua salama. Hata kwa sisi wakristo tunatakiwa 2mkumbuke Mungu wakat wote. Pia kikubwa ni kujua Mungu n Mmoja. God is one and Only. Mungu wa muslims ndio Mungu wa Christians
 
Kwanini usiseme AMANI KWAKO?
Ni kutawaliwa kifikra tu mkuu, wala tusiwalaumu wanaotumia hiyo salaam coz waafrika tumetawaliwa kuanzia akili hadi makalio.

Mtu anaona uzito kusema "habari ya asubuhi", ambacho ni kiswahili kizuri ila kwake kutumia kiarabu kusalimia ni fahari sana.

Ni sawa na mwingine kusema "good morning", zote ni matokeo ya kutawaliwa kuanzia ubongo hadi makalio.
 
Umetoa maelezo mareeefu ila nilichogundua kwa elimu yangu ndogo, wewe ni mshamba/roho mbaya/mfia dini/una choyo na chuki!!!
Wakatoliki wengi jamaa na marafiki zetu tunasalimiana kwa salam hiyo ya kiarabu tena wakiwa ndani ya eneo la Kanisa na safi tu, tatizo lako haujakulia kwenye viunga vya mjini! Maelezo mareeeefu lkn kinachokuuma ASALAAM ALEIKUM!!!..... haya PAX VOBISCUM
 
Hili ni tatizo katika media nyingi, na ni kinyume na ethics za vyombo vya habari kulingana na mazingira husika ya aina ya nchi.

Kwa mfano huyu baby kabaye angekuwa yupo dubai, hicho anachofanya kisingekuwa kosa hata kwa dakika tatu......ila shida ni kwasababu ni taifa ambalo sheria, tamaduni, mila na desturi zake zinafungamana na dini hiyo anayoipa promotion.

Ila kwa context ya Tanzania ni unethical na socially morally but unacceptable kupromote dini katika local public media ambazo zinasikilizwa na watu wa imani tofauti. Si hapo tu ila pia, dini si shida pekee, kuna wengine kusifia kabila au jamii ya aina fulani kuwa ni superior huo ni ujinga wa aina nyingine ambao ni kosa kuupa airtime, kuna pia kuongea mambo ya kibaguzi juu ya jinsia, rangi, utaifa na mengineyo yenye ishara ya kugawanya watu hayo si ya kuvumilika na hayakubaliki hata kidogo......


Hivyo basi, katika hali ya kawaida haya mambo hayaruhusiwi hata kidogo katika taifa secular kama la Tanzania ambalo jamii inashare different religious and Faith perspectives and views ...
 
CLOUDS hupiga kwaya siku nzima ya JUMAPILI.. waislam hawakuwahi kulalamika! Nadhani mbasumguliwa mnasumbuliwa na SUPERIORITY complex! Hamjaanza leo!
We na we uwe unaelewa mtu kaandika nini.....

Mwenzako anacholalamikia ni kuwa huyu dada ni kama anakuwa anafanya campaign ya dini au kiimani katika kipindi ambacho maudhui yake si ya kiimani.

Hivyo vipindi unavyovisema hata vya imani ya kiislam vipo, na huwa vinakuwapo msimu wa Ramadan na hata siku ya ijumaa ambapo waislaam huwa na ibada.....

Hiyo jumapili ni siku ya ibada kwa Christians na ndio maana gospel huwa zinapigwa karibuni kila channel ya television isipokuwa siku za katikati ya wiki.....

Sasa wewe ni nini hiki unasema.....elewa complain ya mtu na usiichukulie kirahisi au kwa mitazamo ya kukopi na kupest bila kutafakari.
 
Yule mshikaji nilikuwa namtazama sana katika vipindi vya dr elie wanachomekea sana sio uongo,ila mm nilikuwa sikereki najua ndo makuzi wamekulia katika dini hiyo nnasikiliza yanayonihusu,ila yeye akichomeka tu wanaanza lawama.
Kuna watu wa ajabu mkuu,nimeshangaa jambo kama hili mtu analifungulia uzi.
 


Chief kweli Karne hii bado unakereka kukutana na watu wenye wametokana na mazingira tofauti ya kimaisha?

Hivi mnatambua kwamba hata sheria ya kimaumbile inatutaka tujiangalie sisi binafsi kwanza kabla ya mwingine/wengine? Dunia inazidi kuwa kama kijiji na wala Tanzania sio Mars ni lazima tukutane na watu wa aina nyingi tena wengine ukatamani ujitie kitanzi kuliko kukutana nao lakini Kanuni ya maisha na sheria ya Ulimwengu inatulazimisha tujitambue sisi ili tuwaelewe wengine!!
 
Mwambie google hasante, na nimekufundisha sasa waelimishe na wezako ulichokiona cha maana nilichokueleza kama unaona ni upuuzi potezea. Tusije kuleta ligi kwenye jambo lakitoto lisilona maana , mstaarabu ni yule asiyemkera jirani yake. Mimi msukuma siwezi kumsalimia muha kisukuma. Mwisho.
 
Kila mtu angekumbatia lugha yake kwa kiwango hicho basi hata hichi kiswahili pengine kisingepatikana.
 
Pengine bi mdada anastress za maisha ndio maana anajikuta anajua sanq Dini na kuihubiri kwa fujo....

Ila kiuhalisia hata mafundisho ya dini yanatutaka kutokupenda kulikopitiliza imani zetu kuliko tunavyompenda sana MUNGU.

Ukiona mtu anajikuta ni mshika dini au anajikuta hiyo imani yake anaijua kuliko kitu chochote, me nakwambia we fanya utafiti utagundua madhaifu yake na hastahili hata kuwa mfagia kanisa au msikiti.
 
Mkuu, sijakereka ila nimesema haya ni matokeo ya kutawaliwa kifikra. Hivi ukiwa China, Korea, Japan, Urusi nk utawasikia wao kwa wao wakisalimiana "good morning"?

Tumetawaliwa na waarabu na wazungu ndio maana tunajikuta tuko hivi.
 
Kwani tofauti ya dini na Mungu ipi?
 
Mkuu, sijakereka ila nimesema haya ni matokeo ya kutawaliwa kifikra. Hivi ukiwa China, Korea, Japan, Urusi nk utawasikia wao kwa wao wakisalimiana "good morning"?

Tumetawaliwa na waarabu na wazungu ndio maana tunajikuta tuko hivi.
Ungejua kikorea ungeweza kuona athari waliyowatawala kwenye kikorea.
 
Hivi hapa tatizo ni Baby Kabaye kuongelea dini? Au tatizo ni dini ya kiislamu? Maana mwisho wa siku kazungumziwa Mungu au sio? Sasa ni lini imeanza kuwa dhambi au kinyume na sheria kumzungumzia Mungu?

Aisee Mungu ni mmoja na hakwepeki katika uhai wala kifo wala hatupungukiwi na chochote tukisikia anazungumziwa, sana sana tunaongeza kitu katika uelewa wetu! Tujifunze kukubali kwamba kuna binadamu wako tofauti na sisi, hata iweje hakuna siku wote tutakua sawa hapa duniani (sijui wakati/baada ya kifo)!!
 
Mkuu, sijakereka ila nimesema haya ni matokeo ya kutawaliwa kifikra. Hivi ukiwa China, Korea, Japan, Urusi nk utawasikia wao kwa wao wakisalimiana "good morning"?

Tumetawaliwa na waarabu na wazungu ndio maana tunajikuta tuko hivi.

Hapana Chief sio kutawaliwa kifikra, hapa unatakiwa ukumbuke ya kwamba kila mmoja ana msingi wake wa maisha!

Wote ni mashahidi wa jinsi Tanzania yetu hisivyokua na msimamo wowote katika suala Zima la utamaduni na chimbuko letu na matokeo yake ni wananchi wasiojua upi hasa ni Utamaduni wao!
Hebu fikiria makabila zaidi ya 20 halafu uyafanyie muingiliano ule wa Mwalimu Nyerere (kipindi cha ujamaa makabila kuoana tofauti na kioo kuchanganywa) unategemea utapata kitu gani?
Matokeo yake kizazi cha 2000 na kuendelea ni kizazi kinachofatiliza tamaduni na machimbuko ya Mataifa mengine kwa asilimia kubwa lakini pia tuzingatie kwamba kwa sasa dunia inazidi kukaribiana (kuwa kijiji) na binaadam kote duniani wanapigana kutafuta ni wapi walipotoka (kizazi kinaamka) matokeo yake dunia miaka 100 ijayo si ajabu ikazungumza Lugha moja kwa asilimia 70!

*Mtazamo wangu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…