Baba yangu hataki nioe kabila tofauti na langu

Dah..... Siku ukimbwaga tu huyo dem wako... mshua anatia timu hapo....anakuwa maza wako....mshua ameyaona madini hapo[emoji12] [emoji12]
Huyo Mzee mi nishamshtukia walevi wenzake anaolewa nao kuna mmojawapo kampandishia kibesi...
Kwamba lazima firstborn wangu amchukue binti yake...yaani just kumwonyesha umwamba tuu!

Mdingi mlevi halafu awe na vinsenti, kwisha habaree yake!
 
Mawazo yaliyochacha?

Mnaendana nani kakwambia?Au kwavile upo delusional na "love" ?Love ikiisha ndio watu wanarudi kwenye senses zao.

Ulikotoka kuna dada wengi wazuri tu,sio wote wabaya,na wanakutegemea uoe mmojawao uendeleze uzao,unapowaacha na kuona hawafai unaenda kuoa mwanamke kama wao ni sign of disrespect kabisa.

Wamekuzaa,wamekuletea mpaka umekua mkaka mzuri,wanategemea atleast uwaoneshe appreciation,uoe kijijini mwenu au kabila lenu...wanawake wazuri wapo,
Waswahili wanasema heri shika moja kuliko kutaka mbili usizokuwa na uhakika Nazo! Halafu hata ukimwacha huyo una uhakika wa kumpata mwingine anayeendanaye? Na a hata akimwacha mchango wake ataupeleka wapi?
 
Mzalishe huyo Dada umalize mchezo, kwani kamwe hawataweza kumkataa mtoto.
 
Mpe Mungu hitaji lako mkabidhi nabako kwa Mungu ayambadilisha siku zinavyokwenda
 
Mimi huwa nafuata kile ninachoamini amini mimi, na sio kile anachoamini au kupenda mtu mwingine, na hiyo ndio principle ya wanaume wote ulimwenguni
Kwa hiyo hiyo fact ya kusema uoe kwenu afu, wanawake wa kwenu wawe huru kuolewa kokote, huo ni unyanyasaji kwetu sisi watoto wa kiume, kwanini uninyime uhuru wa kuchagua mwenza wangu ninae enda kuishi nae mimi
Kwanini uniwekee mipaka ya kutafuta tulizo la moyo wangu?
Hao unaosema walikua wananitumainia Kwani mimi nimezaliwa kwa ajili yao tu?
Dunia ni Pana acha watu waamue kwa mapana pia.
Lakini mura hebu nambie kule kwetu unatokea kijiji gani yawezekana sisi ndugu mura weito

Mimi mchaga mkuu...ila nakusoma Mura

Ila,hawa wanawake ulioishi nao tangu mdogo unawaacha kama vile sio wanawake,hao wengine ndio unaona wanawake zaidi,please onyesha sense of caring vya kwenu,nao ni wanawake kama hao wengine na walikua na matumaini na wewe tangu ukiwa mdogo,wana haki ya kupata upendeleo maalumu walao..

Hebu kuweni na huruma bwana...
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mhaya mchaga hayo si matatizo kbs ndugu yangu
 
Sasa pamoja na hayo hata kama kaongea, Kuna haja gani ya mimi kuoa pale ambapo sijaridhia? Eti kisa tu kuwaridhisha ndugu..

Sijasema uoe mahali ambapo hujaridhia....mzee hajaleta mwanamke specific uoe,kasema chagua kati ya mamia ya wasichana wa kabila lako,utapata atakae endana na wewe 100%.....

Tatizo ni kama amexhagua one specific girl kakuletea,sasa bwana huyu ndio mkeo,huo ni ufala

Ila mzee uende east au west,una jukumu kubwa sana la kuendeleza mwanamke wa kwenu,chukua mmoja na mungu akubariki,usipochukua aisee hata mimi ntakuona traitor!
 
kaa kikao cha ndugu na familia, watu mzee anaowaheshimu muongelee hili jambo, wewe mwenyewe inaionyesha hata kusikiliza. Sometimes mzazi anasema kitu anamaana yake, kama kuna bonds/bondages/chains basi zivunjwe siku hiyo hata mchungaji wa kanisani kwenu akiwepo kwenye kikao itakuwa vema. Kweli kuna mila nyingi, sometimes ni babu mzaa babu ndie alietamka hayo maneno miaka 100 iliyopita ila speaking from experience, my family ilivunja neno la babu wa kale huko na ilikuwa kwa nia njema tu, siku hiyo ilinyesha mvua na radi haijawahi kutokea kijijini hapo, na mvua kwetu inaashiria approval, hakuna aliyekufa, kuumwa, anguka and so forth. jaribu tena na watu wazima wenzake na wana familia. All the best.
 
Nianze hivi kwanza; Wakurya au watu wa Musoma/Mara kwa ujumla wake Wahaya ni watani wenu wa JADI, yaani kama Mhehe na Mngoni au Mnyamwezi au Mchagga na Mpare nk; mambo haya ya utani yana historia yake. Wahehe waliingia utani na Wangoni pamoja na Wanyamwezi kwasababu ya vita walizopigana huko miaka au karne kadhaa zilizopita but sina hakika kwanini Wapare na Wachaga ni watani hali kadhalika watu wa Mara utani wao ulianzaje na Wahaya, may be kuna kitu kibaya au kizuri hilo ni Historia unaweza kuitafuta though haina faida yoyote kwa kizazi cha sasa.
1. Ushauri wangu ni hu; endelea na mipango yako kama kawaida, hakuna Radhi yoyote hapo kwa baba/mama kuhusu mambo haya ya kuoa. Mwanamke mwenye sifa za wife material kuna mwingine zaidi ya huyo?????? Hata may be ukimpata mwingine je unataka afanye nini cha zaidi ya hivyo ambayo huyo kafanya? Remember anaweza kutoa (by chance) but still atakua anadandia mafanikio ya mwingine, so nasisitiza KOMAA na huyo huyo dogo.
2. Kuhusu Kanisani (sina hakika na dhehebu lako) hilo ulikosea, kanisani hakuna mwanaume anaye ulizwaga eti "Nani anamtoa John amuoe Jesca)" Bali hua mchungaji/padree hua unauliza hivi, "Ni nani anamtoa JEsca ili aolewe na John?" But again kwa sheria zetu hata kama kwa mfano baba wa binti angegoma kuolewa na wewe still kama binti ana 18+ of age hilo sio shida, wachungaji/mapadree na maaskofu wanajua wala haliwapagi shida, unalisongesha tu. So ushauri wangu kuhusu ndoa hiyo we endelea tu mipango yako hata na mipango yako ya kanisani pia.
 
pole sana, kama bado mpo kwenye haya mambo.
Wanajamii habari
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni miezi michache imepita toka ni hitimu shahada yangu na sasa hivi nafanya biashara zangu,
Kama mnavyojua umri unapokuruhusu kufanya jambo fulani basi sharti ufanye jambo hilo kwa wakati sahihi. Kwa sasa mimi natarajia kuoa ili niwe na msaidizi tujenge familia, na wakati niko chuo mwaka wa kwanza nilibahatika kukutana na msichana mmoja ambaye tulianza uhusiano, kiukweli uhusiano wetu toka tuanze umekua wa mafanikio sana sababu mchumba wangu huyo ndio amechangia kwa kiasi kikubwa mpaka mimi leo hii kumiliki biashara zangu binafsi.
Kwani alikua akinishauri mambo kadha wa kadha ambayo kiukweli yalizaa matunda na sisi kufikia hatua hii tuliyofikia, haya ni baadhi aliyoyafanya mchumba angu kipindi cha nyuma
1.mimi nikiwa first year yeye second year alinishauri na kunipa wazo la kufungua duka la nafaka, huku yeye akitoa nusu mtaji na mimi nikatoa nusu mtaji, tukafanya biashara na sasa iko mbali sana
2.kuna siku alitonya na kuniambia kwao Kuna banda liko wazi halina kazi kwa hiyo tunaweza kufuga kuku wa nyama na yeye atakua anasimamia kila kitu, kwa sababu namuamini nikafanya hivyo na kiukweli amesimamia shoo vizuri Sana mpaka nafurahi.

TATIZO LIKAANZA KUJITOKEZA
Sasa nije kwenye point iliyonifanya niombe ushauri, sasa kuna siku nimekaa na baba yangu nikamueleza juu ya mimi kuoa na mtu ambaye natarajia kumuoa. Kiukweli nilishangaa kuona mzee akinibadilikia akidai ni lazima nioe mkurya mwenzangu ndio yeye ataweza kushiriki katika hiyo harusi bila hivyo nisimjue, mchumba wangu ni mhaya kachanganya na mchaga.
Nilipo muuliza sababu ni nini mpaka nishindwe kuoa mtu wa kabila tofauti na langu, alichonijibu ni kwamba eti anataka akamilishe mila tu na si vinginevyo, yaani yuko radhi mimi nioe mtu ambaye sio sahihi ilimradi tu akamilishe mila, hivi hii ni sawa kweli??
Na mimi ni mtoto wa kwanza katika familia kwa hiyo nimeambiwa mimi ndio mfano kwa wadogo zangu sasa inabidi nioe mkurya mwenzangu, alafu kama nikitaka kumwoa huyo mchumba wangu ninaye mtaka basi nimwoe mke wa pili, na mimi siko tayari kuoa wake wawili.
Na akaniambia nisipo fanya hivyo nitapata shida sana endapo nitalazimisha kufanya navyotaka mimi.
Sasa ningependa kufahamu kwa wale vijana wenzangu wa kikurya ambao wameoa kabila tofauti alafu ni watoto wa kwanza katika familia walipata shida gani?

Hatua nilizochukua baada ya sakata hilo
1.nimeamua niishi na mchumba wangu hivyo hivyo, sihitaji harusi wala cha kwenda kuvalishana Pete kanisani, maana ndoa nimaridhiano baina ya Watu wawili, na sisi tumeridhiana na harusi sio chochote
2.mzee wangu amesema hanitambui mimi sio mwanae, kwa sababu nina kwangu na nina biashara zangu na kuna ndugu wengi tu wako upande wangu wala sioni shida, ila natafuta suluhu taratibu na nina imani muda ukifika atanielewa

Ushauri wenu
Je ni kipi ambacho nakosea hapo ili nijirekebishe? Vipi naweza kupata kweli tatizo kutokana na hii hali? Na ukizingatia binti wa watu nimetoka nae mbali na tumepanga mambo mengi sana, je ni sahihi kweli tuje tutengane eti kisa kutimiza mila?
Nitashukuru San kwa ushauri wenu wana jamvi
 
Ahsante mkuu kwa ushauri murua, ila mzee wangu hawezi kukaa kikao mchana akiwa mzima, lazima alewe kwanza na hataki kusikia mambo ya wachungaji, yy anaamini wachungaji ni wachonganishi wa familia, yaani mtu yeyote atayepinga mila basi huyo anamwona kama adui na sio mtu mzuri, ukitaka uende nae sawa basi support kila mila hapo mtaelewana saana
 
Nianze hivi kwanza; Wakurya au watu wa Musoma/Mara kwa ujumla wake Wahaya ni watani wenu wa JADI, yaani kama Mhehe na Mngoni au Mnyamwezi au Mchagga na Mpare nk; mambo haya ya utani yana historia yake. Wahehe waliingia utani na Wangoni pamoja na Wanyamwezi kwasababu ya vita walizopigana huko miaka au karne kadhaa zilizopita but sina hakika kwanini Wapare na Wachaga ni watani hali kadhalika watu wa Mara utani wao ulianzaje na Wahaya, may be kuna kitu kibaya au kizuri hilo ni Historia unaweza kuitafuta though haina faida yoyote kwa kizazi cha sasa.
1. Ushauri wangu ni hu; endelea na mipango yako kama kawaida, hakuna Radhi yoyote hapo kwa baba/mama kuhusu mambo haya ya kuoa. Mwanamke mwenye sifa za wife material kuna mwingine zaidi ya huyo?????? Hata may be ukimpata mwingine je unataka afanye nini cha zaidi ya hivyo ambayo huyo kafanya? Remember anaweza kutoa (by chance) but still atakua anadandia mafanikio ya mwingine, so nasisitiza KOMAA na huyo huyo dogo.
2. Kuhusu Kanisani (sina hakika na dhehebu lako) hilo ulikosea, kanisani hakuna mwanaume anaye ulizwaga eti "Nani anamtoa John amuoe Jesca)" Bali hua mchungaji/padree hua unauliza hivi, "Ni nani anamtoa JEsca ili aolewe na John?" But again kwa sheria zetu hata kama kwa mfano baba wa binti angegoma kuolewa na wewe still kama binti ana 18+ of age hilo sio shida, wachungaji/mapadree na maaskofu wanajua wala haliwapagi shida, unalisongesha tu. So ushauri wangu kuhusu ndoa hiyo we endelea tu mipango yako hata na mipango yako ya kanisani pia.
Nimekupata sana mkuu, ahsante sana
 
Pole sana Mkuu ila ushauri wangu mimi nakuomba sana ufunge ndoa na huyo binti. Umefanya maamuzi sahihi ya kuamua kuishi naye na sasa yakamilishe maamuzi yako sahihi. Na kwa maoni yangu hujafanya kosa lolote lile

Wanajamii habari
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni miezi michache imepita toka ni hitimu shahada yangu na sasa hivi nafanya biashara zangu,
Kama mnavyojua umri unapokuruhusu kufanya jambo fulani basi sharti ufanye jambo hilo kwa wakati sahihi. Kwa sasa mimi natarajia kuoa ili niwe na msaidizi tujenge familia, na wakati niko chuo mwaka wa kwanza nilibahatika kukutana na msichana mmoja ambaye tulianza uhusiano, kiukweli uhusiano wetu toka tuanze umekua wa mafanikio sana sababu mchumba wangu huyo ndio amechangia kwa kiasi kikubwa mpaka mimi leo hii kumiliki biashara zangu binafsi.
Kwani alikua akinishauri mambo kadha wa kadha ambayo kiukweli yalizaa matunda na sisi kufikia hatua hii tuliyofikia, haya ni baadhi aliyoyafanya mchumba angu kipindi cha nyuma
1.mimi nikiwa first year yeye second year alinishauri na kunipa wazo la kufungua duka la nafaka, huku yeye akitoa nusu mtaji na mimi nikatoa nusu mtaji, tukafanya biashara na sasa iko mbali sana
2.kuna siku alitonya na kuniambia kwao Kuna banda liko wazi halina kazi kwa hiyo tunaweza kufuga kuku wa nyama na yeye atakua anasimamia kila kitu, kwa sababu namuamini nikafanya hivyo na kiukweli amesimamia shoo vizuri Sana mpaka nafurahi.

TATIZO LIKAANZA KUJITOKEZA
Sasa nije kwenye point iliyonifanya niombe ushauri, sasa kuna siku nimekaa na baba yangu nikamueleza juu ya mimi kuoa na mtu ambaye natarajia kumuoa. Kiukweli nilishangaa kuona mzee akinibadilikia akidai ni lazima nioe mkurya mwenzangu ndio yeye ataweza kushiriki katika hiyo harusi bila hivyo nisimjue, mchumba wangu ni mhaya kachanganya na mchaga.
Nilipo muuliza sababu ni nini mpaka nishindwe kuoa mtu wa kabila tofauti na langu, alichonijibu ni kwamba eti anataka akamilishe mila tu na si vinginevyo, yaani yuko radhi mimi nioe mtu ambaye sio sahihi ilimradi tu akamilishe mila, hivi hii ni sawa kweli??
Na mimi ni mtoto wa kwanza katika familia kwa hiyo nimeambiwa mimi ndio mfano kwa wadogo zangu sasa inabidi nioe mkurya mwenzangu, alafu kama nikitaka kumwoa huyo mchumba wangu ninaye mtaka basi nimwoe mke wa pili, na mimi siko tayari kuoa wake wawili.
Na akaniambia nisipo fanya hivyo nitapata shida sana endapo nitalazimisha kufanya navyotaka mimi.
Sasa ningependa kufahamu kwa wale vijana wenzangu wa kikurya ambao wameoa kabila tofauti alafu ni watoto wa kwanza katika familia walipata shida gani?

Hatua nilizochukua baada ya sakata hilo
1.nimeamua niishi na mchumba wangu hivyo hivyo, sihitaji harusi wala cha kwenda kuvalishana Pete kanisani, maana ndoa nimaridhiano baina ya Watu wawili, na sisi tumeridhiana na harusi sio chochote
2.mzee wangu amesema hanitambui mimi sio mwanae, kwa sababu nina kwangu na nina biashara zangu na kuna ndugu wengi tu wako upande wangu wala sioni shida, ila natafuta suluhu taratibu na nina imani muda ukifika atanielewa

Ushauri wenu
Je ni kipi ambacho nakosea hapo ili nijirekebishe? Vipi naweza kupata kweli tatizo kutokana na hii hali? Na ukizingatia binti wa watu nimetoka nae mbali na tumepanga mambo mengi sana, je ni sahihi kweli tuje tutengane eti kisa kutimiza mila?
Nitashukuru San kwa ushauri wenu wana jamvi
 
Pole sana Mkuu ila ushauri wangu mimi nakuomba sana ufunge ndoa na huyo binti. Umefanya maamuzi sahihi ya kuamua kuishi naye na sasa yakamilishe maamuzi yako sahihi. Na kwa maoni yangu hujafanya kosa lolote lile
Ahsante kwa kunitia moyo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mshua ni mgumu kuelewa sana na hataki kuzungumza na mimi akiwa mzima, ni mpaka alewe ndio anakua tayari kuzungumza na mimi, hivi unafikiri unaweza kumuelewesha mlevi akuelewe, mbona ndugu wengine ambao hawatumii kilevi wamenielewa ila tatizo ni yeye tu
Kumbe mpaka anywe
Kwahiyo unataka kuweka suluhu na mlevi
Mwache aendelee kunywa siku akiacha atakukuta umeoa tayari
Acha kucheza na mlevi katika mambo ya msingi kama ndoa
Assume baba ako alikufa ulipozaliwa
 
Hahahaaa umenichekesha
 
Back
Top Bottom