Tatigha
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 1,957
- 2,024
Wanajamii habari
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni miezi michache imepita toka ni hitimu shahada yangu na sasa hivi nafanya biashara zangu,
Kama mnavyojua umri unapokuruhusu kufanya jambo fulani basi sharti ufanye jambo hilo kwa wakati sahihi. Kwa sasa mimi natarajia kuoa ili niwe na msaidizi tujenge familia, na wakati niko chuo mwaka wa kwanza nilibahatika kukutana na msichana mmoja ambaye tulianza uhusiano, kiukweli uhusiano wetu toka tuanze umekua wa mafanikio sana sababu mchumba wangu huyo ndio amechangia kwa kiasi kikubwa mpaka mimi leo hii kumiliki biashara zangu binafsi.
Kwani alikua akinishauri mambo kadha wa kadha ambayo kiukweli yalizaa matunda na sisi kufikia hatua hii tuliyofikia, haya ni baadhi aliyoyafanya mchumba angu kipindi cha nyuma
1.mimi nikiwa first year yeye second year alinishauri na kunipa wazo la kufungua duka la nafaka, huku yeye akitoa nusu mtaji na mimi nikatoa nusu mtaji, tukafanya biashara na sasa iko mbali sana
2.kuna siku alitonya na kuniambia kwao Kuna banda liko wazi halina kazi kwa hiyo tunaweza kufuga kuku wa nyama na yeye atakua anasimamia kila kitu, kwa sababu namuamini nikafanya hivyo na kiukweli amesimamia shoo vizuri Sana mpaka nafurahi.
TATIZO LIKAANZA KUJITOKEZA
Sasa nije kwenye point iliyonifanya niombe ushauri, sasa kuna siku nimekaa na baba yangu nikamueleza juu ya mimi kuoa na mtu ambaye natarajia kumuoa. Kiukweli nilishangaa kuona mzee akinibadilikia akidai ni lazima nioe mkurya mwenzangu ndio yeye ataweza kushiriki katika hiyo harusi bila hivyo nisimjue, mchumba wangu ni mhaya kachanganya na mchaga.
Nilipo muuliza sababu ni nini mpaka nishindwe kuoa mtu wa kabila tofauti na langu, alichonijibu ni kwamba eti anataka akamilishe mila tu na si vinginevyo, yaani yuko radhi mimi nioe mtu ambaye sio sahihi ilimradi tu akamilishe mila, hivi hii ni sawa kweli??
Na mimi ni mtoto wa kwanza katika familia kwa hiyo nimeambiwa mimi ndio mfano kwa wadogo zangu sasa inabidi nioe mkurya mwenzangu, alafu kama nikitaka kumwoa huyo mchumba wangu ninaye mtaka basi nimwoe mke wa pili, na mimi siko tayari kuoa wake wawili.
Na akaniambia nisipo fanya hivyo nitapata shida sana endapo nitalazimisha kufanya navyotaka mimi.
Sasa ningependa kufahamu kwa wale vijana wenzangu wa kikurya ambao wameoa kabila tofauti alafu ni watoto wa kwanza katika familia walipata shida gani?
Hatua nilizochukua baada ya sakata hilo
1.nimeamua niishi na mchumba wangu hivyo hivyo, sihitaji harusi wala cha kwenda kuvalishana Pete kanisani, maana ndoa nimaridhiano baina ya Watu wawili, na sisi tumeridhiana na harusi sio chochote
2.mzee wangu amesema hanitambui mimi sio mwanae, kwa sababu nina kwangu na nina biashara zangu na kuna ndugu wengi tu wako upande wangu wala sioni shida, ila natafuta suluhu taratibu na nina imani muda ukifika atanielewa
Ushauri wenu
Je ni kipi ambacho nakosea hapo ili nijirekebishe? Vipi naweza kupata kweli tatizo kutokana na hii hali? Na ukizingatia binti wa watu nimetoka nae mbali na tumepanga mambo mengi sana, je ni sahihi kweli tuje tutengane eti kisa kutimiza mila?
Nitashukuru San kwa ushauri wenu wana jamvi