Baba yangu hataki nioe kabila tofauti na langu

Baba yangu hataki nioe kabila tofauti na langu

Wewe si umeshakua mwanaume, kua na msimamo ndugu, alafu sisi watu wa mara huwa hatuyumbishwi kijana
 
Wanajamii habari
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni miezi michache imepita toka ni hitimu shahada yangu na sasa hivi nafanya biashara zangu,
Kama mnavyojua umri unapokuruhusu kufanya jambo fulani basi sharti ufanye jambo hilo kwa wakati sahihi. Kwa sasa mimi natarajia kuoa ili niwe na msaidizi tujenge familia, na wakati niko chuo mwaka wa kwanza nilibahatika kukutana na msichana mmoja ambaye tulianza uhusiano, kiukweli uhusiano wetu toka tuanze umekua wa mafanikio sana sababu mchumba wangu huyo ndio amechangia kwa kiasi kikubwa mpaka mimi leo hii kumiliki biashara zangu binafsi.
Kwani alikua akinishauri mambo kadha wa kadha ambayo kiukweli yalizaa matunda na sisi kufikia hatua hii tuliyofikia, haya ni baadhi aliyoyafanya mchumba angu kipindi cha nyuma
1.mimi nikiwa first year yeye second year alinishauri na kunipa wazo la kufungua duka la nafaka, huku yeye akitoa nusu mtaji na mimi nikatoa nusu mtaji, tukafanya biashara na sasa iko mbali sana
2.kuna siku alitonya na kuniambia kwao Kuna banda liko wazi halina kazi kwa hiyo tunaweza kufuga kuku wa nyama na yeye atakua anasimamia kila kitu, kwa sababu namuamini nikafanya hivyo na kiukweli amesimamia shoo vizuri Sana mpaka nafurahi.

TATIZO LIKAANZA KUJITOKEZA
Sasa nije kwenye point iliyonifanya niombe ushauri, sasa kuna siku nimekaa na baba yangu nikamueleza juu ya mimi kuoa na mtu ambaye natarajia kumuoa. Kiukweli nilishangaa kuona mzee akinibadilikia akidai ni lazima nioe mkurya mwenzangu ndio yeye ataweza kushiriki katika hiyo harusi bila hivyo nisimjue, mchumba wangu ni mhaya kachanganya na mchaga.
Nilipo muuliza sababu ni nini mpaka nishindwe kuoa mtu wa kabila tofauti na langu, alichonijibu ni kwamba eti anataka akamilishe mila tu na si vinginevyo, yaani yuko radhi mimi nioe mtu ambaye sio sahihi ilimradi tu akamilishe mila, hivi hii ni sawa kweli??
Na mimi ni mtoto wa kwanza katika familia kwa hiyo nimeambiwa mimi ndio mfano kwa wadogo zangu sasa inabidi nioe mkurya mwenzangu, alafu kama nikitaka kumwoa huyo mchumba wangu ninaye mtaka basi nimwoe mke wa pili, na mimi siko tayari kuoa wake wawili.
Na akaniambia nisipo fanya hivyo nitapata shida sana endapo nitalazimisha kufanya navyotaka mimi.
Sasa ningependa kufahamu kwa wale vijana wenzangu wa kikurya ambao wameoa kabila tofauti alafu ni watoto wa kwanza katika familia walipata shida gani?

Hatua nilizochukua baada ya sakata hilo
1.nimeamua niishi na mchumba wangu hivyo hivyo, sihitaji harusi wala cha kwenda kuvalishana Pete kanisani, maana ndoa nimaridhiano baina ya Watu wawili, na sisi tumeridhiana na harusi sio chochote
2.mzee wangu amesema hanitambui mimi sio mwanae, kwa sababu nina kwangu na nina biashara zangu na kuna ndugu wengi tu wako upande wangu wala sioni shida, ila natafuta suluhu taratibu na nina imani muda ukifika atanielewa

Ushauri wenu
Je ni kipi ambacho nakosea hapo ili nijirekebishe? Vipi naweza kupata kweli tatizo kutokana na hii hali? Na ukizingatia binti wa watu nimetoka nae mbali na tumepanga mambo mengi sana, je ni sahihi kweli tuje tutengane eti kisa kutimiza mila?
Nitashukuru San kwa ushauri wenu wana jamvi
Ndugu haya ya wazazi mengine kuyafuatilia ni magum nyinyi kama mnapendana endeleen na mapenzi yenu mana wenyewe mmeshibana kwa kila hali inatosha mkionesha msimamo wenu sasa huyo mzee mwenyewe badae atajirudi na kutambua ni nini kimo ndani yenu. ENDELEZENI MAPENZI YENU MUBASHARA
 
Ila kaka unaushauri wa kibwege duuuu yaani sijui wawapi wewe lazima ni mkurya wachaga hawana akili za kijinga hizi
kaa kikao cha ndugu na familia, watu mzee anaowaheshimu muongelee hili jambo, wewe mwenyewe inaionyesha hata kusikiliza. Sometimes mzazi anasema kitu anamaana yake, kama kuna bonds/bondages/chains basi zivunjwe siku hiyo hata mchungaji wa kanisani kwenu akiwepo kwenye kikao itakuwa vema. Kweli kuna mila nyingi, sometimes ni babu mzaa babu ndie alietamka hayo maneno miaka 100 iliyopita ila speaking from experience, my family ilivunja neno la babu wa kale huko na ilikuwa kwa nia njema tu, siku hiyo ilinyesha mvua na radi haijawahi kutokea kijijini hapo, na mvua kwetu inaashiria approval, hakuna aliyekufa, kuumwa, anguka and so forth. jaribu tena na watu wazima wenzake na wana familia. All the best.
 
Pole sana kaka lakini jaribu kuelewesha ata ndugu wa karibu waweze mueleza mzee wako coz mapnzi bora hujengwa na nyie wawili wala xi wazazi
 
Na mimi nakushauri either uoe mwanamke ambaye mko naye dini moja kama si kabila lako, ila kama ni tofauti ya hapo basi oa kabila lako
 
Sasa mbona we ndo unaonekana unamatatizo,we MTU gani haongei na wew mpaka alewe .sasa iyo inayokukataza ni akili ya pombe wala sio yeye We nenda kabaliki ndoa yako uishi na mkeo kwa aman
 
Baada ya kusoma comments za wadau nimeina bado nchi hii kuna wimbi kubwa tu la ubaguzi hususan wa kikabila ktk ndoa yaan watu wazima na akili zao timamu bado wanapalilia kuoana kwa misingi ya kikabila?, kwani kwenye ndoa mtakuwa na kazi ya kufanya matambiko?, nchi hii tunataka haya mambo yaishe ndio maana Aman inatawala kwa sababu ya mwingiliano wa ndoa baina ya makabila. Kwa hiyo acheni watu waoane as long as wamependana na kuelewana regardless ya tofauti ya makabila. Mzazi anayetaka mwanae aoe ama aolewe na mtu wa kabila lake binafsi namuona ana mawazo mgando na hajaelimika vinginevyo labda apinge ndoa kwa kigezo kingine ila sio kabila.
 
Watu wa namna kama yako huwatokea hasa vijana wanaotaka kuoa wakati bado wanategemea wazazi wako. Yani unaonesha mpaka sasa wazazi wako hawaamini kama unaweza jisimamia mwenyewe. Wanakuwa na hofu kuwa unaweza oa mwanamke wa ajabu uje uwaletee tabu wao.
 
Ndugu haya ya wazazi mengine kuyafuatilia ni magum nyinyi kama mnapendana endeleen na mapenzi yenu mana wenyewe mmeshibana kwa kila hali inatosha mkionesha msimamo wenu sasa huyo mzee mwenyewe badae atajirudi na kutambua ni nini kimo ndani yenu. ENDELEZENI MAPENZI YENU MUBASHARA
Shukrani kiongozi
 
Pole sana kaka lakini jaribu kuelewesha ata ndugu wa karibu waweze mueleza mzee wako coz mapnzi bora hujengwa na nyie wawili wala xi wazazi
Nitafanya hivyo kiongozi
 
Sasa mbona we ndo unaonekana unamatatizo,we MTU gani haongei na wew mpaka alewe .sasa iyo inayokukataza ni akili ya pombe wala sio yeye We nenda kabaliki ndoa yako uishi na mkeo kwa aman
Mimi sina tatizo mkuu, sema tu napenda amani
 
Baada ya kusoma comments za wadau nimeina bado nchi hii kuna wimbi kubwa tu la ubaguzi hususan wa kikabila ktk ndoa yaan watu wazima na akili zao timamu bado wanapalilia kuoana kwa misingi ya kikabila?, kwani kwenye ndoa mtakuwa na kazi ya kufanya matambiko?, nchi hii tunataka haya mambo yaishe ndio maana Aman inatawala kwa sababu ya mwingiliano wa ndoa baina ya makabila. Kwa hiyo acheni watu waoane as long as wamependana na kuelewana regardless ya tofauti ya makabila. Mzazi anayetaka mwanae aoe ama aolewe na mtu wa kabila lake binafsi namuona ana mawazo mgando na hajaelimika vinginevyo labda apinge ndoa kwa kigezo kingine ila sio kabila.
Mkuu tuna safari ndefu sana, sisi kama watanzania
 
Watu wa namna kama yako huwatokea hasa vijana wanaotaka kuoa wakati bado wanategemea wazazi wako. Yani unaonesha mpaka sasa wazazi wako hawaamini kama unaweza jisimamia mwenyewe. Wanakuwa na hofu kuwa unaweza oa mwanamke wa ajabu uje uwaletee tabu wao.
Mimi siwategemei kwa chochote zaidi ya ushauri wao kama wazazi
 
Back
Top Bottom