Baba yangu hataki nioe kabila tofauti na langu

Sio vizuri kwenda kinyume na matakwa ya wazazi, lakini wazazi wengine wanachofanya siyo kabisa. Sa ukioa mwanamke wa kabila lako faida yake nini??? Watoto wenyewe sisi wa .com hata lugha na mila zetu hatuzijui... Kuumizana kichwa tu kwa kweli.
Mkuu, mi nadhani mkafunge tu ndoa kwa mwenyekiti mpate cheti na anzeni maisha yenu. Huna ata haja ya kuwaambia watu, tafuta shahidi wenu tu na mkaoane. Mzee akibadilisha mawazo huko mbele ndo muibariki ndoa yenu na kuafanya kasherehe.
Yaani mzee wangu sijawahi kumpinga kwa chochote, lakini hili hapana lazima niende against maana ndio maisha yangu hayo
 
oa unayeendana naye sababu kabila haliji kuishi na wewe .. halafu baba yako haji kuishi na wewe kuwa na amani
 
Hivi bado kuna wazazi wa hivi?!

Mkuu endelea kumshawishi atakubali. .sasa hivi anakataa kataa ila ukitilia mkazo mwisho wa siku atakubali

Usioe kabla baba hajakubali
Ndoa inanoga zaidi pande zote mbili zikikubali
 
Wanajamii habari
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni miezi michache imepita toka ni hitimu shahada yangu na sasa hivi nafanya biashara zangu,
Kama mnavyojua umri unapokuruhusu kufanya jambo fulani basi sharti ufanye jambo hilo kwa wakati sahihi. Kwa sasa mimi natarajia kuoa ili niwe na msaidizi tujenge familia, na wakati niko chuo mwaka wa kwanza nilibahatika kukutana na msichana mmoja ambaye tulianza uhusiano, kiukweli uhusiano wetu toka tuanze umekua wa mafanikio sana sababu mchumba wangu huyo ndio amechangia kwa kiasi kikubwa mpaka mimi leo hii kumiliki biashara zangu binafsi.
Kwani alikua akinishauri mambo kadha wa kadha ambayo kiukweli yalizaa matunda na sisi kufikia hatua hii tuliyofikia, haya ni baadhi aliyoyafanya mchumba angu kipindi cha nyuma
1.mimi nikiwa first year yeye second year alinishauri na kunipa wazo la kufungua duka la nafaka, huku yeye akitoa nusu mtaji na mimi nikatoa nusu mtaji, tukafanya biashara na sasa iko mbali sana
2.kuna siku alitonya na kuniambia kwao Kuna banda liko wazi halina kazi kwa hiyo tunaweza kufuga kuku wa nyama na yeye atakua anasimamia kila kitu, kwa sababu namuamini nikafanya hivyo na kiukweli amesimamia shoo vizuri Sana mpaka nafurahi.

TATIZO LIKAANZA KUJITOKEZA
Sasa nije kwenye point iliyonifanya niombe ushauri, sasa kuna siku nimekaa na baba yangu nikamueleza juu ya mimi kuoa na mtu ambaye natarajia kumuoa. Kiukweli nilishangaa kuona mzee akinibadilikia akidai ni lazima nioe mkurya mwenzangu ndio yeye ataweza kushiriki katika hiyo harusi bila hivyo nisimjue, mchumba wangu ni mhaya kachanganya na mchaga.
Nilipo muuliza sababu ni nini mpaka nishindwe kuoa mtu wa kabila tofauti na langu, alichonijibu ni kwamba eti anataka akamilishe mila tu na si vinginevyo, yaani yuko radhi mimi nioe mtu ambaye sio sahihi ilimradi tu akamilishe mila, hivi hii ni sawa kweli??
Na mimi ni mtoto wa kwanza katika familia kwa hiyo nimeambiwa mimi ndio mfano kwa wadogo zangu sasa inabidi nioe mkurya mwenzangu, alafu kama nikitaka kumwoa huyo mchumba wangu ninaye mtaka basi nimwoe mke wa pili, na mimi siko tayari kuoa wake wawili.
Na akaniambia nisipo fanya hivyo nitapata shida sana endapo nitalazimisha kufanya navyotaka mimi.
Sasa ningependa kufahamu kwa wale vijana wenzangu wa kikurya ambao wameoa kabila tofauti alafu ni watoto wa kwanza katika familia walipata shida gani?

Hatua nilizochukua baada ya sakata hilo
1.nimeamua niishi na mchumba wangu hivyo hivyo, sihitaji harusi wala cha kwenda kuvalishana Pete kanisani, maana ndoa nimaridhiano baina ya Watu wawili, na sisi tumeridhiana na harusi sio chochote
2.mzee wangu amesema hanitambui mimi sio mwanae, kwa sababu nina kwangu na nina biashara zangu na kuna ndugu wengi tu wako upande wangu wala sioni shida, ila natafuta suluhu taratibu na nina imani muda ukifika atanielewa

Ushauri wenu
Je ni kipi ambacho nakosea hapo ili nijirekebishe? Vipi naweza kupata kweli tatizo kutokana na hii hali? Na ukizingatia binti wa watu nimetoka nae mbali na tumepanga mambo mengi sana, je ni sahihi kweli tuje tutengane eti kisa kutimiza mila?
Nitashukuru San kwa ushauri wenu wana jamvi
Hakuna ulichokosea mwana umenifurahisha sana kwa kutoyumbishwa na msimamo wa baba yako ndoa ni ya watu wawili yaani wewe na mkeo hata ukioa mkuria mwenzako mkapata matatizo amini usiamini baba yako pia hatakusaidia chochote hivyo umefanya vyema kuishi maisha yako kama yeye alivyoishi maisha yake. Kwenye swala la ndoa fanya taratibu mfunge ndoa kwa mujibu wa imani zenu ni vyema zaidi kuliko kuishi tu hivi.
 
Watoto wa kiume ni jukumu lenu muowe kwenu...wanawake wanaweza olewa na wengine ila mtoto wa kiume linda nyumbani...k ni k tu..na upendo ni upendo tu,wanawake ni wale wale,walau oa kwenu upunguze wasioolewa mungu akupe thawabu...acheni utoto wa eti "nimependa",rubbish...umependa wewe wa kwanza?Ulimbukeni mtupu
 
Ndoa nikitu kingine na uchumba ni kitu kingine ndugu yangu tafakali sana ,lengo la Mzee si mbashara lakini Luna faida nyingi sana za kuoa kwenu na ayoubainika baadae hasa kwa ndoa za kufungwa kanisani kwan mkisha funga ndoa make sasa ufichua makucha yote na kuyaweka waz lakin kabla ya hapo mwanamke unaweza kuishi nae miaka na miaka na usimjue vema .Na hii ndoimepelekea ndoa za wazee wetu kudumu ,kiukweli wezee wetu hawakua na elimu lakin kwenye ndoa walikua na fikila pevu zaid yetu wenye elimu,ukifatilia ndoa zilizo mchanganyiko na zisizo mchanganyiko pana tofauti kubwa sana sikushauli umuache mwenzio hla cha msingi jikabiz kwa bwana yy atafanya njia.Wapo wanandoa wanaishi zaid ya miaka 10 lakin baada ya kufunga ndoa utashangaa ndan ya miaka mi5 wametengana kiujumla swala la ndoa nipana ndomaana hata wachungaji au mashehe ndoa zao nao utakuta zina migogoro mikubwa.Kwa ujumla ukifanya upembuz kwa mapana kuoa kabila yako kuna faida zaidi ya kuoa kabila tofauti,hla aya ubainika safari ya ndoa ikiwa inaendelea.
 
baba yako ana akili sana hata dangote kaoa kwao...

k ni k tu ukija kuwa mkubwa utaelewa.. chukua k ya kwenu... wahaya wanajitahidi sana kwenye hili na ndio maana ndoa zao zinadumu sana
 
Kama inavouma kuchaguliwa mke/mume,tusikubali kuchaguliwa viongozi pia,wawe wa kisiasa ama kidini,kuna raha kwenye kupata unachokitaka,ila si kupewa usichokitaka ili kukamilisha mila na ujinga mwingine unaofanana na huo.

Ila mzee wako angekuelewa maana wewe hauoi mila ila unaoa mke.
 
Wataolewa na watakaopendana nao

Yaelekea mzee wewe ni mdharau kwenu sana....jukumu la msingi la mwanaume ni kuendeleza nyumbani,sasa huu upuuzi wenu wa kujifanya eti mmpenda mahali,dada zenu kwenye kabila lenu waoelewe na nyani?

Kupenda ni very subjective,ni maendekezo,penda kwenu,oa wa kwenu mungu akusaidie..pay homage to your ancestors
 
Wengi wanaochangia nafikiri hawajaoa,hawajui maisha ya ndoa yalivyo:kuna kuumwa ,kufirisika,kugombana,kufa au kufisha,undugu na mambo mengine...mzazi wako anapokuchagulia pa kuoa usifikiri hana akili,anajua maana ameyaona mengi.USHAURI:Kama umepewa option ya kuoa huyo mchumba wako muoe lkn pia muoe na huyo ulieambiwa na baba yako.NB:ukifanya jambo lolote bila idhini ya baba yako hautofanikiwa kwenye hii dunia.kuna watu wengi tu kwenye asili ya kwenu wameoa wake zaidi ya mmoja,alafu simama kiume usipelekeshwe pelekeshwe na mwanamke,hao wanawake sio Ndugu zetu,subiri ukipata matatizo ndio utajua familia yako na ya Mke wako wa wapi wanajali.
 
We unampoteza huna lolote unalolijua...

Dada wa watu kateseka nae na wamefanikiwa huyo mwanamke wa kabila lake aje kula vya bure tuu mxiuuuu...

Acha kumpoteza mwenzako,
 
Oa tu ila...asiye sikia la mkuu muda humuadabisha...yaho makabira uliyo taja hapo...mmmmh hata mim naungana na baba yako.
 
Msikilize baba yako , acha kusikiliza watu humu, maana siku ukipata taabu hawatakuja kukusaidia zaidi ya baba yako
 
Watoto wa kiume ni jukumu lenu muowe kwenu...wanawake wanaweza olewa na wengine ila mtoto wa kiume linda nyumbani...k ni k tu..na upendo ni upendo tu,wanawake ni wale wale,walau oa kwenu upunguze wasioolewa mungu akupe thawabu...acheni utoto wa eti "nimependa",rubbish...umependa wewe wa kwanza?Ulimbukeni mtupu
Sasa mkuu mtoto wa watu umempotezea muda wake siku zote hizo, anakujali, anakupenda, ana ushauri wa kujenga juu yako, na mmepanga malengo makubwa tu hapo baadae alafu uje kumtosa kisa kulinda mila zisizo na faida? Hata mungu anaweza akuadhibu
 
Hivi bado kuna wazazi wa hivi?!

Mkuu endelea kumshawishi atakubali. .sasa hivi anakataa kataa ila ukitilia mkazo mwisho wa siku atakubali

Usioe kabla baba hajakubali
Ndoa inanoga zaidi pande zote mbili zikikubali
Nitaufanyia kazi ushauri wako!!
 
Hakuna ulichokosea mwana umenifurahisha sana kwa kutoyumbishwa na msimamo wa baba yako ndoa ni ya watu wawili yaani wewe na mkeo hata ukioa mkuria mwenzako mkapata matatizo amini usiamini baba yako pia hatakusaidia chochote hivyo umefanya vyema kuishi maisha yako kama yeye alivyoishi maisha yake. Kwenye swala la ndoa fanya taratibu mfunge ndoa kwa mujibu wa imani zenu ni vyema zaidi kuliko kuishi tu hivi.
Sawa sawa kiongozi
 
Ndoa nikitu kingine na uchumba ni kitu kingine ndugu yangu tafakali sana ,lengo la Mzee si mbashara lakini Luna faida nyingi sana za kuoa kwenu na ayoubainika baadae hasa kwa ndoa za kufungwa kanisani kwan mkisha funga ndoa make sasa ufichua makucha yote na kuyaweka waz lakin kabla ya hapo mwanamke unaweza kuishi nae miaka na miaka na usimjue vema .Na hii ndoimepelekea ndoa za wazee wetu kudumu ,kiukweli wezee wetu hawakua na elimu lakin kwenye ndoa walikua na fikila pevu zaid yetu wenye elimu,ukifatilia ndoa zilizo mchanganyiko na zisizo mchanganyiko pana tofauti kubwa sana sikushauli umuache mwenzio hla cha msingi jikabiz kwa bwana yy atafanya njia.Wapo wanandoa wanaishi zaid ya miaka 10 lakin baada ya kufunga ndoa utashangaa ndan ya miaka mi5 wametengana kiujumla swala la ndoa nipana ndomaana hata wachungaji au mashehe ndoa zao nao utakuta zina migogoro mikubwa.Kwa ujumla ukifanya upembuz kwa mapana kuoa kabila yako kuna faida zaidi ya kuoa kabila tofauti,hla aya ubainika safari ya ndoa ikiwa inaendelea.
Nitaufanyia kazi ushauri wako mkuu
 
baba yako ana akili sana hata dangote kaoa kwao...

k ni k tu ukija kuwa mkubwa utaelewa.. chukua k ya kwenu... wahaya wanajitahidi sana kwenye hili na ndio maana ndoa zao zinadumu sana
Sasa hivi mkuu hatuangalii hayo, angalia mtu ana kupenda vipi, na ana kujali vipi, kabila halina nafasi
 
Back
Top Bottom