Baba Mwenye Nyumba ana maana gani katika hili?

Baba Mwenye Nyumba ana maana gani katika hili?

Sasa unachong'ang'ania hapo ni kitu gani hasa? or What are you really trying to justfy?

Kama mwenyewe ulivyosema umepokewa hapo na hao Wazee kwa heshima na hisani ya urafiki wa aunty yako na wenye nyumba. Kwa maneno mengine wenyewe walikuwa hawana mpango wa kupangisha chumba wa upande wa nyumba (kulikuwa hakuna Tangazo kuwa wanapangisha). Hivyo umepokelewa na kupewa treatment kama mtoto. Na pengine hiyo kodi yako unayolipa pengine ndo ku sitiriana tu.

Ni bahati mbaya kuwa sasa uwepo wako kwenye hiyo nyumba una kila dalili za kuelekea kuvuuruga udugu na amani kwenye hiyo familia. Kitendo cha baba mwenye nyumba na Mzee wa familia kutaka muwe ki mapenzi ni 'conflict of interest'. Kwa kuwa na wewe umesha jiweka sawa ki maisha, kuujua mji vema na ku save vijipesa japo vya kupanga sehemu nyingine ni vema kuongozwa na busara badala ya kutaka ku question na neno 'but why"..kumbuka huna haki zozote hapo, ulipokewa kwa hisani tu kama mtoto wa nyumbani kuliko haki ya ki upangaji yaani "renter"

Umekaribishwa kwa wema basi ondoka kwa wema...Kwani utakapokuwa na kwako na unakuja kutembea hapo nyumbani siku moja moja basi hata huyo Mzee atakuwa nafsini mwake anatahayari na hizo shikamoo anazozikataa sasa atakuwa anaziitika kwa "Marahaba" ya nguvu na uchangamfu mwingi. Hata mama mwenye nyumba asisitize vipi wewe hama...kama ana akili basi ataelewa tu ki utu uzima kama kuna jambo. Wala huna haja ya kuleta maneno ya sijui... "paukwa Ooh halafu pakawa" Wee mtu mzima sasa.

Matatizo kama ya kwako ni mengi sana hasa kwa wasichana (japo pia yapo kwa wavulana), Mfano unakuta umemaliza Chuo kama wewe kesi yako hiyo halafu unakwenda kuanza kazi mji fulani unaishi na dada yako na mumewe au aunty yako na mumewe halafu unakuta mume anaanza kukuletea mizengwe ya kutaka "kukudokoa"🙂. Hivyo si bora uanze ustaarabu mwingine bado kungali asubuhi asubuhi kabla hakujakuchwa. Ongozwa na busara yako dada angu vinginevyo sijui utakuwa una save nini katika situation kama hiyo. Piece of mind should be your first priority.

Asante sana, nimekuelewa vizuri mno. Nisingependa kabisa kuweka chuki na hawa wazee, wema walionitendea ni mkubwa mno.

 
Umepata mpaka pesa ya kununua ka gari bado una ng 'ang 'ania hapo hapo? .usijifanye hujui au huelewi baba mwenyenyumba anataka nini kwako. Ni wazi unajua anataka nini, ni wazi huna mkataba wa kuish hapo.kama unatambua usumbufu wa huyo baba, njia pekeee ya kumaliza huo usumbufu ni either umsikilize na utimize anachotaka au uhame ukakae sehemu huru.hakuna namna nyingine ya kuelewa baba wa nyumba anataka nini zaid ya hiyo unayoielewa ndani ya nafsi yako

Ndugu yangu, nilijua nikimuonyesa huyu baba dalili zote za kuwa haitawezekana ata give up, lakini sasa ninaona chuki imeingia, kwakweli ninakosa raha, unakaa kwenye nyumba ya mtu ambae hataki msalimiane!

 
Ndio maisha na majaribu na ww c wa kwanza jifunze cku mtu akija kwako ukamsaidia kuangalia na upande wa mumeo mtarajiwa acjeyafanya nyuma ya pazia kama uliyofanyiwa ww!n kawaida tena wengine wanatongozwa na baba zao wa kambo wengine mpaka shemeji zao hongera kwa maamuz mazur ww endelea na maisha yako hayo ndio yanayotujenga pengine huyi baba acngefanya hayo nyumba ww ucngetafuta maisha kwa raha za hapo ila ss ktk hayo mahudhi pia yamekuwezesha kupiga hatua so mshukuru Mungu kwa yote yeye anajua kila kitu,jiulize ucngekua na kaz au ndio ungekua mfanyakaz wa ndan huna pa kwenda au ndie angekua boc wako ofcn ingekuaje!!!!we nshukuru Mungu sawa dada yangu ndio maisha na ukubwa huo uckii ukibwa jalajala!!!?
 
kiukweli dadaangu nakushauri uhame au jenga nyumba yako, hivi unajisikiaje kupaki gari yako kwenye nyumba ya kupanga, think outside the box.
 
kiukweli dadaangu nakushauri uhame au jenga nyumba yako, hivi unajisikiaje kupaki gari yako kwenye nyumba ya kupanga, think outside the box.


Asante sana dada yangu kwa ushauri mzuri. Matatizo ya baba yalianza kwenye lift, kukiwa na mvua au ndiyo nimechelewa basi atajitolea kunidrop kazini, lakini maongezi aliyokuwa ananiambia kwenye gari sikuwa ninayapenda. Kwa akili fupi nilidhani kuwa na usafiri wangu kungenifanya niwe more independent, kumbe nilikuwa ninajaribu kuziba ufa huku ukuta ukizidi kuinama!
 
Unapenda sana kwa sadala au unapenda sana kitonga au kwa lugha rahisi unapenda mtelemko na utakuponza
 
unafikiri utaendelea kukaa hapo milele?!!

Watu wengine wa ajabu kweli, na shukuru anakugasi manake inaonekana ungejisahau kabisa, au unataka wadau wakushauri umpe nyapu ili upewe nyumba???

Samahani mjomba " nyapu" ndo nini???


Sent from my EyePhone
 
Pole sana..ni mkoa gani huo?

Ndugu nilileta hii subject ili nipate msaada, sasa nikiandika mkoa gani huoni kama nitakuwa nimewaexpose wasamaria wangu na kuyaweka maisha yangu hatarini? Nilichohitaji ilikuwa ushauri ambao nimeupata, mengine yatakuwa ni irrelevant.
 
Hamia mtaa wa saba(7).Ukiamua kuendelea kuishi hapo fanya haya:
-Mweleze mama mwenye nyumba mkanda mzima.
-Muulize mdingi akuweke wazi anachotaka.Akikueleza anachotaka uamuzi ni wako,na elewa kila uamuzi una POSITIVE or NEGATIVE OUTCOME.
 
Yaani mpaka umenunua gari? Uamuzi ni wako na uwezo unao, 1.mpe anachotaka au 2.hamia kwingine
 
Nilipomaliza chuo, nilipata kazi katika mkoa huu, sikuwa ninamfahamu mtu hata mmoja. Aunty yangu alinitafutia nyumba kwa rafiki zake ambao ni watu wazima, mume na mke. Nyumba ni kubwa ya vyumba vitano vya kulala na sebule mbili. Nilipewa chumba kimoja, kwakweli kunipangisha mim ilikuwa ni kwasababu ya usalama wa nyumba tu, siyo kwa kuwaongezea kipato, kwani watu hawa wana hali nzuri sana ya kimaisha. Muda mwingi huutumia nchi za ughaibuni kwani ndiko watoto wao watatu wanakoishi, hivyo wakiwa safarini ninabaki mimi na dada wa kazi.

Wakiwepo wenye nyumba nikiwasalimia 'shikamoo baba na mama' wanaitikia wote wawili 'marahaba binti umeamkaje/umeshindaje'. Akiwepo baba pekeyake nikimuamkia 'shikamoo baba' ananijibu 'salama tu'. Mama ni mshika dini sana na muda mwingi anakuwa kanisani. Baba akiwa pekeyake anakuja kunigongea chumbani na kunikaribisha mvinyo, kwakweli ninakosa raha sana.

Nilipohamia hapa, mama mwenyenyumba aliniambia nitumie kila kitu chake, kwakweli amenichukulia kama mototo wake, na aliniusia kuwa nijaribu kuweka pesa, ili na mimi ninunue kiwanja changu kwani kulipa kodi ni kupoteza pesa. Ameniruhusu kuwakarisha wageni wangu kwenye sebule ya pili, ambayo wenyewe hawaitumiii sana. Kwkuwa ndiyo ninaanza maisha, nilihamia hapa na sanduku languo tu, na kitu cha kwanza kununua ilikuwa TV ambayo nimeiweka chumbani kwangu. Nilifanikiwa kigari, cha kunirahisishia usafiri.

Kwa kero za baba mwenye nyumba mke wake asipokuwepo, basi nemeamua nikitoka kazini ninampigia simu mama, akiniambia yuko kanisani, basi nitakula nyama choma sehemu wakati ninamsubiri turudi wote nyumbani. Tangu nimeanza kufanya hivyo, siku hizi baba nikimsalimia hanijibu. Jamani, huu mbona ni mtihani wa maisha, wakati nyumba ni kwake, jamani ninaomba ushauri.
Ni kawaida , Vya Dezo sikuzote havikosi string attached
 
Back
Top Bottom