Baba Mwenye Nyumba ana maana gani katika hili?

Baba Mwenye Nyumba ana maana gani katika hili?

kitachofuata nikuzushiwa makubwa kutoka kwa huyo baba mbona dunia utaona chungu? Muhimu hama ila aga vizuri
 
Kimbiza mbunye fasta kabla hajai2mbua! Na akishaipiga k2 ugomvi utaanza hapo..!
 
Nilipomaliza chuo, nilipata kazi katika mkoa huu, sikuwa ninamfahamu mtu hata mmoja. Aunty yangu alinitafutia nyumba kwa rafiki zake ambao ni watu wazima, mume na mke. Nyumba ni kubwa ya vyumba vitano vya kulala na sebule mbili. Nilipewa chumba kimoja, kwakweli kunipangisha mim ilikuwa ni kwasababu ya usalama wa nyumba tu, siyo kwa kuwaongezea kipato, kwani watu hawa wana hali nzuri sana ya kimaisha. Muda mwingi huutumia nchi za ughaibuni kwani ndiko watoto wao watatu wanakoishi, hivyo wakiwa safarini ninabaki mimi na dada wa kazi.Wakiwepo wenye nyumba nikiwasalimia 'shikamoo baba na mama' wanaitikia wote wawili 'marahaba binti umeamkaje/umeshindaje'. Akiwepo baba pekeyake nikimuamkia 'shikamoo baba' ananijibu 'salama tu'. Mama ni mshika dini sana na muda mwingi anakuwa kanisani. Baba akiwa pekeyake anakuja kunigongea chumbani na kunikaribisha mvinyo, kwakweli ninakosa raha sana. Nilipohamia hapa, mama mwenyenyumba aliniambia nitumie kila kitu chake, kwakweli amenichukulia kama mototo wake, na aliniusia kuwa nijaribu kuweka pesa, ili na mimi ninunue kiwanja changu kwani kulipa kodi ni kupoteza pesa. Ameniruhusu kuwakarisha wageni wangu kwenye sebule ya pili, ambayo wenyewe hawaitumiii sana. Kwkuwa ndiyo ninaanza maisha, nilihamia hapa na sanduku languo tu, na kitu cha kwanza kununua ilikuwa TV ambayo nimeiweka chumbani kwangu. Nilifanikiwa kigari, cha kunirahisishia usafiri.Kwa kero za baba mwenye nyumba mke wake asipokuwepo, basi nemeamua nikitoka kazini ninampigia simu mama, akiniambia yuko kanisani, basi nitakula nyama choma sehemu wakati ninamsubiri turudi wote nyumbani. Tangu nimeanza kufanya hivyo, siku hizi baba nikimsalimia hanijibu. Jamani, huu mbona ni mtihani wa maisha, wakati nyumba ni kwake, jamani ninaomba ushauri.
Sepa zako kwani huyo baba mwenye nyumba amekuwa kivuli chako i mean huwezi kusepa? hilo li baba lina nyege halina chochote cha maana hapo.
 
Sepa zako kwani huyo baba mwenye nyumba amekuwa kivuli chako i mean huwezi kusepa? hilo li baba lina nyege halina chochote cha maana hapo.

Asante sana kwa ushauri, nimepata nyumba na nitahama katika wiki mbili zijazo, kwani inafanyiwa matengezo ya mwisho. Katika kipinid hiki nimeamua kuchukua likizo na kwenda kukaa na wazazi wangu wakati nikisubiri nyumba ikamilike.
 
Nilipomaliza chuo, nilipata kazi katika mkoa huu, sikuwa ninamfahamu mtu hata mmoja. Aunty yangu alinitafutia nyumba kwa rafiki zake ambao ni watu wazima, mume na mke. Nyumba ni kubwa ya vyumba vitano vya kulala na sebule mbili. Nilipewa chumba kimoja, kwakweli kunipangisha mim ilikuwa ni kwasababu ya usalama wa nyumba tu, siyo kwa kuwaongezea kipato, kwani watu hawa wana hali nzuri sana ya kimaisha. Muda mwingi huutumia nchi za ughaibuni kwani ndiko watoto wao watatu wanakoishi, hivyo wakiwa safarini ninabaki mimi na dada wa kazi.

Wakiwepo wenye nyumba nikiwasalimia 'shikamoo baba na mama' wanaitikia wote wawili 'marahaba binti umeamkaje/umeshindaje'. Akiwepo baba pekeyake nikimuamkia 'shikamoo baba' ananijibu 'salama tu'. Mama ni mshika dini sana na muda mwingi anakuwa kanisani. Baba akiwa pekeyake anakuja kunigongea chumbani na kunikaribisha mvinyo, kwakweli ninakosa raha sana.

Nilipohamia hapa, mama mwenyenyumba aliniambia nitumie kila kitu chake, kwakweli amenichukulia kama mototo wake, na aliniusia kuwa nijaribu kuweka pesa, ili na mimi ninunue kiwanja changu kwani kulipa kodi ni kupoteza pesa. Ameniruhusu kuwakarisha wageni wangu kwenye sebule ya pili, ambayo wenyewe hawaitumiii sana. Kwkuwa ndiyo ninaanza maisha, nilihamia hapa na sanduku languo tu, na kitu cha kwanza kununua ilikuwa TV ambayo nimeiweka chumbani kwangu. Nilifanikiwa kigari, cha kunirahisishia usafiri.

Kwa kero za baba mwenye nyumba mke wake asipokuwepo, basi nemeamua nikitoka kazini ninampigia simu mama, akiniambia yuko kanisani, basi nitakula nyama choma sehemu wakati ninamsubiri turudi wote nyumbani. Tangu nimeanza kufanya hivyo, siku hizi baba nikimsalimia hanijibu. Jamani, huu mbona ni mtihani wa maisha, wakati nyumba ni kwake, jamani ninaomba ushauri.

Dadeki,we cheka cheka tu,utaliwa sasa hivi,yangu masikio na macho.,kwanza inaonekana ushaliwa wewe apia kama hujaliwa bado.
 
Dadeki,we cheka cheka tu,utaliwa sasa hivi,yangu masikio na macho.,kwanza inaonekana ushaliwa wewe apia kama hujaliwa bado.

Hapana ndugu yangu, ningefika huko yasingeniumiza mpaka kuja kuomba ushauri hapa jukwaani.
 
jiandae kuhama kabla ya kukupata ya kukupata.
 
jiandae kuhama kabla ya kukupata ya kukupata.

Asante sana ndugu,

Nimepata nyumba ambayo ni mpya, mwenye nyumba ameniambia itakuwa tayari katika siku takribani kumi zijazo. Nimewataarifu wenyeji wangu nia yangu ya kuhama, mama amesikitika sana, lakini imebidi akubali tu, baba anafeel guilty. Kwakweli mazingira baba mwenyenyumba aliyoniwekea yamenifrastruate sana. Nimechukua likizo ya wiki mbili kazini na nitakwenda kuishi na wazazi wangu kwa muda huo. Nikirudi kama nyumba ninayopanga kuhamia haitakuwa tayari, nimejiandaa kukaa kwenye kihoteli cha bei nafuu wakati nikisubiri.

inshallah Mungu atakuongoza.
 
Jamii Forum ni kama familia, nimefurahi sana nilivyopata msaada wa mawazo kutokana na hili. Waingereza wanausemi 'problem shared is problem solved'. Asanteni sana kaka na dada zangu.
 
Jamii Forum ni kama familia, nimefurahi sana nilivyopata msaada wa mawazo kutokana na hili. Waingereza wanausemi 'problem shared is problem solved'. Asanteni sana kaka na dada zangu.

karibu tena mdada..
 
....Usije ukashangaa siku moja simu hiyo baba wa nyumba wako anakutafuta huko huko uliko.....
 
...wanakugeuza msukule sasaivi.... endelea kushangaa
 
Pole ila ungemsumulia tu Aunt yako ajue yaliyokusibu. Sasa umesema kwanini unaondoka naona umesema umewaeleza, nini uliwaeleza.

Ndio hii mibaba mizee ya siku hizi haina aibu wala adabu, yaani nyumba nyingi tu zinamatatizo hayo. Wake wengine wanawajua waume zao na uzee wote hata ndugu zao wa. Kike wanatongozwa.

Ila angalia sana na usihata pokea simu zake au kumpigia kumsalimu. Wewe wasiliana na huyo Mama tu, kama ni shida sana basi wasiliana na msichana wake atampa ujumbe.

Ila nakupa hongera kwa msimamo wako, wengi huwa wangeshadandia kuwa na mbaba wangepewa nafasi.
 
Mi sina cha kuongeza zingatia ushauli na tafutata mme umekua sasa
 
chukua tv yako na mabegi yako pakia kwenye hiko kigari chako chapa lapa.
 
Pole ila ungemsumulia tu Aunt yako ajue yaliyokusibu. Sasa umesema kwanini unaondoka naona umesema umewaeleza, nini uliwaeleza.

Ndio hii mibaba mizee ya siku hizi haina aibu wala adabu, yaani nyumba nyingi tu zinamatatizo hayo. Wake wengine wanawajua waume zao na uzee wote hata ndugu zao wa. Kike wanatongozwa.

Ila angalia sana na usihata pokea simu zake au kumpigia kumsalimu. Wewe wasiliana na huyo Mama tu, kama ni shida sana basi wasiliana na msichana wake atampa ujumbe.

Ila nakupa hongera kwa msimamo wako, wengi huwa wangeshadandia kuwa na mbaba wangepewa nafasi.

Asante sana dada yangu Mzurimie,
Kwakweli sikutaka kuwagombanisha aunty yangu na marafiki zake, ukizingatia mama kila akiongea na aunty yangu ananisifia nilivyo mtaratibu na mwenye maadili.

Ilibidi nikae nao wote baba na mama na kuwaeleza kuwa inabidi ni hame, na sababu kubwa ni kuwa nimepata nyumba na nimeipenda, nikiiachia itachukuliwa, hata hivyo sitakaa nao siku zote kwani watoto na wajukuu wao wote wakija likizo watahitaji nyumba yao. Mama alisikitika sana kuwa itakuwa vigumu kwao kupata mtu wanaomuamini kumuacha nyumbani wakati wakiwa safarini.

Hili tatizo nilishidwa kuongea na mtu yeyote yule, kwasababu kwanza hii familia ni ya watu maarufu katika mji huu na huwezi kujua chines whispering, unaongea na kinarudi kwa mwenyewe kimegeuzwa, mnaanza kuwekeana uhasama. Kichwa changu kilikuwa kimejaa mawazo kama baloon na kuja hapa JF kumenisaidia kuyatoa yote.
 
Sasa unachong'ang'ania hapo ni kitu gani hasa? or What are you really trying to justfy?

Kama mwenyewe ulivyosema umepokewa hapo na hao Wazee kwa heshima na hisani ya urafiki wa aunty yako na wenye nyumba. Kwa maneno mengine wenyewe walikuwa hawana mpango wa kupangisha chumba wa upande wa nyumba (kulikuwa hakuna Tangazo kuwa wanapangisha). Hivyo umepokelewa na kupewa treatment kama mtoto. Na pengine hiyo kodi yako unayolipa pengine ndo ku sitiriana tu.

Ni bahati mbaya kuwa sasa uwepo wako kwenye hiyo nyumba una kila dalili za kuelekea kuvuuruga udugu na amani kwenye hiyo familia. Kitendo cha baba mwenye nyumba na Mzee wa familia kutaka muwe ki mapenzi ni 'conflict of interest'. Kwa kuwa na wewe umesha jiweka sawa ki maisha, kuujua mji vema na ku save vijipesa japo vya kupanga sehemu nyingine ni vema kuongozwa na busara badala ya kutaka ku question na neno 'but why"..kumbuka huna haki zozote hapo, ulipokewa kwa hisani tu kama mtoto wa nyumbani kuliko haki ya ki upangaji yaani "renter"

Umekaribishwa kwa wema basi ondoka kwa wema...Kwani utakapokuwa na kwako na unakuja kutembea hapo nyumbani siku moja moja basi hata huyo Mzee atakuwa nafsini mwake anatahayari na hizo shikamoo anazozikataa sasa atakuwa anaziitika kwa "Marahaba" ya nguvu na uchangamfu mwingi. Hata mama mwenye nyumba asisitize vipi wewe hama...kama ana akili basi ataelewa tu ki utu uzima kama kuna jambo. Wala huna haja ya kuleta maneno ya sijui... "paukwa Ooh halafu pakawa" Wee mtu mzima sasa.

Matatizo kama ya kwako ni mengi sana hasa kwa wasichana (japo pia yapo kwa wavulana), Mfano unakuta umemaliza Chuo kama wewe kesi yako hiyo halafu unakwenda kuanza kazi mji fulani unaishi na dada yako na mumewe au aunty yako na mumewe halafu unakuta mume anaanza kukuletea mizengwe ya kutaka "kukudokoa"🙂. Hivyo si bora uanze ustaarabu mwingine bado kungali asubuhi asubuhi kabla hakujakuchwa. Ongozwa na busara yako dada angu vinginevyo sijui utakuwa una save nini katika situation kama hiyo. Piece of mind should be your first priority.
 
Nilipomaliza chuo, nilipata kazi katika mkoa huu, sikuwa ninamfahamu mtu hata mmoja. Aunty yangu alinitafutia nyumba kwa rafiki zake ambao ni watu wazima, mume na mke. Nyumba ni kubwa ya vyumba vitano vya kulala na sebule mbili. Nilipewa chumba kimoja, kwakweli kunipangisha mim ilikuwa ni kwasababu ya usalama wa nyumba tu, siyo kwa kuwaongezea kipato, kwani watu hawa wana hali nzuri sana ya kimaisha. Muda mwingi huutumia nchi za ughaibuni kwani ndiko watoto wao watatu wanakoishi, hivyo wakiwa safarini ninabaki mimi na dada wa kazi.

Wakiwepo wenye nyumba nikiwasalimia 'shikamoo baba na mama' wanaitikia wote wawili 'marahaba binti umeamkaje/umeshindaje'. Akiwepo baba pekeyake nikimuamkia 'shikamoo baba' ananijibu 'salama tu'. Mama ni mshika dini sana na muda mwingi anakuwa kanisani. Baba akiwa pekeyake anakuja kunigongea chumbani na kunikaribisha mvinyo, kwakweli ninakosa raha sana.

Nilipohamia hapa, mama mwenyenyumba aliniambia nitumie kila kitu chake, kwakweli amenichukulia kama mototo wake, na aliniusia kuwa nijaribu kuweka pesa, ili na mimi ninunue kiwanja changu kwani kulipa kodi ni kupoteza pesa. Ameniruhusu kuwakarisha wageni wangu kwenye sebule ya pili, ambayo wenyewe hawaitumiii sana. Kwkuwa ndiyo ninaanza maisha, nilihamia hapa na sanduku languo tu, na kitu cha kwanza kununua ilikuwa TV ambayo nimeiweka chumbani kwangu. Nilifanikiwa kigari, cha kunirahisishia usafiri.

Kwa kero za baba mwenye nyumba mke wake asipokuwepo, basi nemeamua nikitoka kazini ninampigia simu mama, akiniambia yuko kanisani, basi nitakula nyama choma sehemu wakati ninamsubiri turudi wote nyumbani. Tangu nimeanza kufanya hivyo, siku hizi baba nikimsalimia hanijibu. Jamani, huu mbona ni mtihani wa maisha, wakati nyumba ni kwake, jamani ninaomba ushauri.

Umepata mpaka pesa ya kununua ka gari bado una ng 'ang 'ania hapo hapo? .usijifanye hujui au huelewi baba mwenyenyumba anataka nini kwako. Ni wazi unajua anataka nini, ni wazi huna mkataba wa kuish hapo.kama unatambua usumbufu wa huyo baba, njia pekeee ya kumaliza huo usumbufu ni either umsikilize na utimize anachotaka au uhame ukakae sehemu huru.hakuna namna nyingine ya kuelewa baba wa nyumba anataka nini zaid ya hiyo unayoielewa ndani ya nafsi yako
 
Back
Top Bottom