Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,639
- 220,421
Nilipomaliza chuo, nilipata kazi katika mkoa huu, sikuwa ninamfahamu mtu hata mmoja. Aunty yangu alinitafutia nyumba kwa rafiki zake ambao ni watu wazima, mume na mke. Nyumba ni kubwa ya vyumba vitano vya kulala na sebule mbili. Nilipewa chumba kimoja, kwakweli kunipangisha mim ilikuwa ni kwasababu ya usalama wa nyumba tu, siyo kwa kuwaongezea kipato, kwani watu hawa wana hali nzuri sana ya kimaisha. Muda mwingi huutumia nchi za ughaibuni kwani ndiko watoto wao watatu wanakoishi, hivyo wakiwa safarini ninabaki mimi na dada wa kazi.
Wakiwepo wenye nyumba nikiwasalimia 'shikamoo baba na mama' wanaitikia wote wawili 'marahaba binti umeamkaje/umeshindaje'. Akiwepo baba pekeyake nikimuamkia 'shikamoo baba' ananijibu 'salama tu'. Mama ni mshika dini sana na muda mwingi anakuwa kanisani. Baba akiwa pekeyake anakuja kunigongea chumbani na kunikaribisha mvinyo, kwakweli ninakosa raha sana.
Nilipohamia hapa, mama mwenyenyumba aliniambia nitumie kila kitu chake, kwakweli amenichukulia kama mototo wake, na aliniusia kuwa nijaribu kuweka pesa, ili na mimi ninunue kiwanja changu kwani kulipa kodi ni kupoteza pesa. Ameniruhusu kuwakarisha wageni wangu kwenye sebule ya pili, ambayo wenyewe hawaitumiii sana. Kwkuwa ndiyo ninaanza maisha, nilihamia hapa na sanduku languo tu, na kitu cha kwanza kununua ilikuwa TV ambayo nimeiweka chumbani kwangu. Nilifanikiwa kigari, cha kunirahisishia usafiri.
Kwa kero za baba mwenye nyumba mke wake asipokuwepo, basi nemeamua nikitoka kazini ninampigia simu mama, akiniambia yuko kanisani, basi nitakula nyama choma sehemu wakati ninamsubiri turudi wote nyumbani. Tangu nimeanza kufanya hivyo, siku hizi baba nikimsalimia hanijibu. Jamani, huu mbona ni mtihani wa maisha, wakati nyumba ni kwake, jamani ninaomba ushauri.