Baba mdogo anakula kitimoto hadharani

Huyo kwa jinsi ulivyomuelezea naona keshajisahau! Anachowaza ni kitimoto tuu..
 
Kwani hapo ni kwako?
kama mwenye nyumba anaagizwa alete na analeta wewe ni nani upinge,kumbuka na huyo nae ni baba umuheshimu
 
nishapotezea
 
Yeah dogo anatatizo hilo lkn kwasasa hayupo
 
Hapo inahitaji busara za pande zote mbili, ila kwa huyu Baba Mdogo yeye tayari anakosa busara maana angeweza kufanya hayo mbali huko bila kukera wengine...ukizingati yeye ni Mgeni, vipi kama ingekuwa upo kwake, si ajabu angekulazimisha hata ule.

Ila naamini kwa imani zote kadri unavyopitia majaribu na kuyashinda ndivyo unavyopata thawabu zaidi.
 
Yeah tukiendaga kwao nasi tunafwata sheria zao,
 
Linapo kuja suala haki katika dini hakuna kufurahishana au kuogopana mwambie ukweli hii kitu hapa haitakiwi na ni haramu kwa Imani yangu akasirike asikasirike
 
Hii issue ya kitimoto naona kama mnaibeba tofauti au kimakosa. Kwa nielewavyo Mimi, japo waislam kitimoto ni Haram kwenu, lakin under certain circumstances mnaweza kula. If that's the case, sio kama yakufaa ujisikie vibaya baba ako mdogo kukwambia umpokelee (as long as inakuwa imefungwa vizuri, na hajakwambia ule).

Lakini pia nishawahi kumuuliza Sheikh mmoja kuhusu waislam kula kwenye mahotel ya Kitalii au yanayotoa huduma ya kitimoto, akaniambia vyombo vikishatumika huwa vinaoshwa, so sio tatizo wao kupata huduma sehemu. If that's the case, sioni ajabu baba yako mdogo kutumia vyombo vyenu maana huwa vinaoshwa.

Nina uncle alioa mwanamke wa Kiislam, kila mmoja aliendelea kubaki na dini yake. Yule Aunt alikuwa hatumii kitimoto, ila mara kadhaa nishawahi kushuhudia akimuandalia uncle.

Sijajua kama nitakuwa wrong or what, ila huwa nahisi kuna baadhi ya mapokeo kwenye hizi dini zetu hatujayaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…