Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,202
- 99,941
Baba, si ulisema tuna majirani wema sana? Na kwamba nyumba yetu ina utulivu, tena wewe na wanao yaani kaka zangu na dada zangu tunapendana sana? Mbona sasa huyu Jirani yetu baba Kagoma juzi alitufokea na tena akatufokea sana tu, huu ni ujirani gani?
Namkumbuka Mama nanihii juzi alivyotoka kuuza vitumbua vyake kule ughaibuni kaja akataka kutudhulumu dishi letu la maji na maji yake akidai dishi lote na maji yake ni vya kwake?
Huyu Babu yake Musa-Vani juzi niliwakuta kilabuni yeye, yule mtoto wa Kunyata na jirani mwingine wakikuteta tena wakisema wanataka waanzishe mto wao wenyewe, ati wasiwe na wanashirikiana na sisi, baba naona kama vile maadaui wanaongezeka kuliko marafiki.
Leo wakati natoka shule nikapitia kule kwa Mwalimu wa Kizungu, nikamkuta anaangalia Luninga huku taarifa lukuki zikitamalaki kuwa eti, kaka zangu na dada zangu nusura wadunfane leo walipokuwa kwenye darasa lao la tuisheni kule Arusha, Baba; nionavyo mimi maadui wanaongezeka kuliko marafiki.
Nilipokuwa pale chini ya mti wakati nasubiri kuchota maji nikajiliwa na wazo la kuwahesabu hawa waliokuwa marafiki, ndugu na jamaa zetu ambao baba wewe mwenyewe pamoja na akina babu mlidiriki kuwakaribisha hadi chumbani kule ambako hawakuruhusiwa kuingia, mmmhhh baba sikuamini kuwa haha pale Kaunga eti nao wana watoto wa baba yao mdogo anaitwa Mama wa 23 eti nao pia hawatutaki!!!
Baba, nakuomba sana aamka usingizini tutengeneze njia zetu, kama tutashindwa kabisa kupatana na majirani hawa basi heri tunoe mapanga yetu kungali na muda wa kufanya hivyo.
Waslaam Kitinda mimba wako, safarini Shinyanga