Baba Diamond Ashinda Njaa

Baba Diamond Ashinda Njaa

Ali mtelekeza mond n mama yke kipindi mond bado mtoto so mama akachukua jukumu la kumlea mond pekee yke, n mond alipokuwa dogo alipokuwa anaenda kumuomba ela baba yke alikuwa ana mtimua n kipigo juu
unajua maana ya baba??
 
Kama kuna mzazi juha huyu jamaa anashika namba moja...mzazi mwenye kujitambua hawezi kukubali huu upuuzi wa kuhojiwa kwenye gazeti la udaku mambo binafsi yanayohusu familia yake
Huu ni upuuzi na upumbavu wa kiwango cha juu mno
Hivi kalipwa bei gani?
Hivi anajua jamaa wametengeneza bei gani kupitia hiyo habari
Huyu hajitambui na atafakari alipokosea kuliko kuja kulialia kwenye vyombo hovyo vya habari...huku ni kujidhalilisha
Halafu mbona hao waandushi hawamuulizi kwanini alitelekeza familia yake ili kubalance habari na kuweza ku-judge nani mkosaji.Naona anatafuta tu huruma ya watu ili Diamond aonekane mbaya na mpuuzi lakini anashindwa kuelewa alipokuwa anatumia hela na wanawake wengine wakina Diamond na mama yake walishinda njaa mara ngapi.
 
Alifanya nini ujana wake na je angekuwa teja hayo malalamiko angeenda tena gazetini au TV kusema na ingekuwa habari Leo?
 
Halafu mbona hao waandushi hawamuulizi kwanini alitelekeza familia yake ili kubalance habari na kuweza ku-judge nani mkosaji.Naona anatafuta tu huruma ya watu ili Diamond aonekane mbaya na mpuuzi lakini anashindwa kuelewa alipokuwa anatumia hela na wanawake wengine wakina Diamond na mama yake walishinda njaa mara ngapi.
Hapo ndio penye shida ukisoma unaona kabisa ni story iliyotengenezwa
 
Mfumo wa wanawake wa kijapan ukoje?
Mkuu wanawake wa Kijep habari zao ndefu.
Ila Kwa ufupi ukimdinya ukampa kitumbo halafu ukakimbia kulea, ujue na mtoto usimuhesabu, na mtoto mwenyewe pia akipata akili wala hakuweki kwenye hesabu kuwa wewe ni baba yake.
Mtoto akiwa mdogo analishwa sumu zote kuwa hana baba, na sumu inapokelewa kiukamilifu na mtoto.
Akipata akili wala hajishughulishi kukutafuta, na ukimuuliza anakujibu kweupe Mbuzi anakula Majani kuwa 'Baba sina, alikimbia wakati nikiwa mdogo, nimelelewa na mama tu'.
Lakini uzuri wa wakimbiaji nao huwa hawageuki nyuma, wakikimbia huwa kimoja, wala huwa hawakumbuki kuwa kuna sehemu walizaa.
Nafanya kazi na vijana 3 wa Kijapan, wote Ma- engineer, wawili wamekimbiwa na baba zao toka wakiwa watoto wadogo kabisa na mmoja alikimbiwa na mama yake akiwa na umri wa miaka 10.
 
Baba sio shahawa au sperms tu..siku hizi zinapatikana hata maabara unaotesha mimba ...

Muulizeni kama yeye sasa ndio ameukata na diamond ni chokoraa mitaani huyo njemba angerudi kuwafata ?

Narejea ubaba sio shahawa...
 
Sijaona UZEE hapo unless siku hizi jina UZEE limepoteza credbility
 
Naomba kuuliza, ni jukumu la mtoto kumtunza mzazi wake au ni jukumu la mzazi kumtunza mwanaye aliyemleta hapa duniani kwa raha zake? Tuache fikra mgando, si jukumu la Diamond kumhudumia baba yake ila ni hisani kwa Diamond kumhudumia baba yake. Na hii iwe fundisho kwetu sote, tusiwategemee watoto mwache naye ana vipaumbele vyake.
Ni jukumu la diamond kumtunza tiffa.
 
Hilo ni fundisho kwa wanaume jamani msikimbie majukumu yenu sasa yeye aliacha kumhudumia why yeye ahudumiwe sasa hivi?
 
MSIKIE BABA DIAMOND AKIFUNGUKA




NA

WAANDISHI WETU, Risasi Jumamosi




DAR ES SALAAM: Wakati mwanaye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mwanaye Tiffah wakiteketeza kiasi cha fedha kinachokadiriwa kufikia shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi.

IMG_3230.jpg


Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma.

Diamond na familia yake hiyo sambamba na madansa wake, waliondoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Frankfurt, Ujerumani ambapo pamoja na kufanya ziara ya kimuziki katika nchi tofauti balani Ulaya, staa huyo aliitumia ziara hiyo kuponda raha.

diamond1.jpg
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ pamoja na mtoto wao Tiffah wakila ‘bata’ Ulaya.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kililiambia gazeti hili mapema wiki hii kuwa, baba Diamond kwa sasa ana maisha magumu na mara nyingi amekuwa akishinda njaa huku baadhi ya majirani wakimpa msaada hali inayowasababisha kushangaa baada ya kusoma kwenye magazeti kwamba mwanaye huyo anatumbua fedha kibao na familia yake, ndugu na marafiki huku mzazi wake huyo akiteseka.

mama-d-ulaya1.jpg


Familia ya Diamond Platnumz ‘wakitumbua’ Ulaya.

“Jamani baba Diamond anateseka! Muoneeni huruma. Alikuja kwangu kuniomba elfu moja lakini bahati mbaya na mimi sikuwa nayo. Mara nyingi amekuwa akishinda njaa. Mbaya zaidi anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu na hana mtu wa kumpeleka hospitali. Njooni mumuone yupo hapa kwake anatia huruma,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kiukweli baba Diamond anasikitisha sana. Tunashindwa kujua tatizo liko wapi kati yake na mwanaye, maana kuna wakati huwa anamsaidia lakini wakati mwingine anampotezea.”

MAPAPARAZI WAMUIBUKIA
Baada ya kuzipata habari hizo, mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa baba Diamond, Magomeni ya Kagera jijini Dar na kumkuta nje ya nyumba yake akiwa ameshika tamaa huku akionesha hali ya kunyong’onyea kama mtu aliyekata tamaa ya maisha.

IMG_3235-001.jpg
Mzee Abdul Juma.

HALI YAKE NI MBAYA
Akizungumza na gazeti hili baada ya salamu, baba Diamond alieleza kwamba bado hali yake ya miguu ni mbaya kwani anatembea kwa kuburuza laiti angekuwa kama zamani angeweza kufanya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato angalau apate fedha kwa ajili ya kula hasa katika kipindi hiki ambacho hana msaada.

3-1-1.jpg


“Niko hapa bado mambo siyo mazuri, miguu inanisumbua kama unavyoona. Nasikia mwanangu (Diamond) ana ziara nje ya nchi na juzi niliona mmeandika ameteketeza milioni 100 na familia yake, namsubiri akirudi huko naamini atanisaidia angalau fedha hata ya kwenda kwenye matibabu na kula kama ataamua maana alishawahi kuniahidi, hali yangu siyo shwari nabangaiza tu hapa,” alisema baba Diamond.

diam.jpg


DIAMOND ASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond aliyeko Ujerumani kwa sasa ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema hana cha kuzungumza kwa sasa.
“No comment kwa sasa, subirini nikirudi tutaliongea hilo kwa kirefu,” alisema Diamond.

ALIOKWENDA NAO ULAYA
Katika gazeti lenye udugu wa damu na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu iliyopita, ukurasa wake wa mbele lilikuwa na kichwa kisemacho; DIAMOND
ATEKETEZA SH. MIL 100 ULAYA.
Katika habari hiyo, Diamond aliandikwa kusafiri na ‘ujumbe’ mrefu wa idadi ya watu 14 ambao wote walikuwa chini yake kwa malazi na chakula. Watu hao ni Zari, mama yake mzazi, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi (mpigapicha), Salam (meneja), mke wa meneja wake mwingine Batu Tale, madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari. Hao walikwea pipa na kufikia Frankfurt, Ujerumani.

BABA DIAMOND AMEFIKAJE HAPA?
Baba Diamond anadaiwa akiwa angali kijana, alitengana na mama Diamond akiwa na mtoto huyo mdogo kwa miaka mingi bila kumpa huduma zozote kitu ambacho kimemsukuma Diamond kuwa na chuki na ashindwe kumpa matunzo mzazi wake huyo baada ya kupata mafanikio.
Hata hivyo, mara kadhaa Diamond amekuwa akimsaidia fedha baba yake huyo lakini si kwa asilimia mia moja kama anavyomtunza mama yake ambaye anaonekana kula raha hususan kipindi hiki ambacho bwana mdogo huyo kutoka Tandale, maisha yamemnyookea.

Gladness Mallya, Erick Evarist na Richard Bukos. Chanzo.GBP

Tafuta pesa we Pimbi(dingi), kama upewi unachotaka, maswala ya kulia lia kausha
 
Mkuu tuko pamoja siku zote sikio halizidi kichwa, mzazi ni mzazi tu haijalishi kakufanyia nini.

Kuna watu wanadhani Diamond ndio wa kwanza, kumbe sivyo haya majaribu yametukuta wengi. Hadithi yako mkuu, kwa ukaribu inataka kufanana na yangu haina haja ya kuiweka hapa...huyu Diamond pesa zinamdanganya, na mama zetu hawa wakati mwingine utengeneza chuki. Ninachoamini huyu Diamond bado ni mtoto ajifunze kuwa yeye sio wa kwanza asimame kwenye nafasi yake kama mtoto na akumbuke maandiko.
Haswaaaa hata Watoto tunawakosea sana wazazi lakini hawatuchukii milele,bado wazaz wanatujali na kutuombea mema,
 
Back
Top Bottom