Baba Diamond Ashinda Njaa

Baba Diamond Ashinda Njaa

Diamond msaidie mzee.


Mkuu, umeandika kwa hekima sana! Huyu Diamond, mimi nimeshamuona kama mpumbavu tu, kuna watoto
wa kiume wengine sisi hatuna baba (tunaumia) na kuna wengine walikosana na baba zao sana tu, na huwa wanawasamehe na kuwasaidia. Na kuna wengine walipoteana na baba zao kitambo huwa wanawatafuta
mpaka wanawapata na kama walishafariki huwa wanaumia
sana! Sasa huyu Diamond anamwacha baba yake bila ya msaada hivi ni kosa gani la mzee huyu ambalo halipaswi kusamehewa? Mzee anaishi maisha magumu, Diamond anajidai kutoa
misaada kwa watu baki bila ya kumjali baba
yake sasa ni huruma gani aliyonayo kwa watu baki kuliko
baba yake mzazi ambaye Diamond
bado anatumia jina lake katika majina yake
matatu. Basi kama Diamond hampendi baba yake, aache kabisa kutumia jina la baba yake, atumie jina la ukoo wa mama yake halafu huyu mama Diamond naye ni mtu wa majungu na huyu Diamond hata aende wapi huyo mzee ndio baba yake ni busara akamkumbuka!
 
Ali Kiba okoa jahazi saidia mzee kabla hajavunjika kabisa. Ila huyu mzee hajafanya poa kufuatiliwa na waandishi ni kawaida ila asingetoa ushirikiano wowote kwao ama kuliongelea kama alivyoyafanya Diamond. Na kikubwa hata akisaidiwa hatoridhika kwa tabia hii ataendelea kulalamika tu. Diamond ampe milioni hamsini mbele ya wana Habari kama anavyotaka kisha kila mtu aambae kivyake.
 
udaku mwingine bana...
Huyu Baba hashindi njaa kwa sababu mwanae ana pesa.
Hayo ni maisha na bado anaonekana kijana...
Ashike jembe hata yeye atatoka tu.
Naomba kuuliza, ni jukumu la mtoto kumtunza mzazi wake au ni jukumu la mzazi kumtunza mwanaye aliyemleta hapa duniani kwa raha zake? Tuache fikra mgando, si jukumu la Diamond kumhudumia baba yake ila ni hisani kwa Diamond kumhudumia baba yake. Na hii iwe fundisho kwetu sote, tusiwategemee watoto mwache naye ana vipaumbele vyake.
 
Watu wengi mnacomment bila kusikiliza hiyo clip! Dingi anaongea sense! Yeye alii njaa waandishi ndo wanamfata na dingi kumbe ana nyumba yake! Yeye anaongea ukweli na hana mpango wa kumrudia mama diamond! Inavyoelekea watoto wanataka mzee anyenyekee sana na dingi hataki! Sema kichwa cha habari kimetengeneza kuuza
 
kiukweli maisha ya baba Diamond hayakupaswa kuwa na tofauti hii na ya mwanaye. Ila mi naona ni sahihi yeye kupitia hayo hadi hapo mwanaye atakapomtafuta.
Hili ni fundisho kwa wazazi wote wanaodharau watoto wao au kuwatelekeza.
Pia nijuavyo mimi, unaposababisha mwanao apate shida kwa ajili yako tena makusudi unajikosesha baraka wewe mwenyewe. Mungu akubariki wakati kwa kiburi na makusudi ulisababisha mateso na dhiki kwa mtoto aliyetoka kiunoni mwako?
Ni hiyari ya Diamond kumsaidia babake kama watu wengine au la.
Mimi naongea frm experience. Sikia kwa mwenzio tu. Unapata taabu huku unajua baba yako yupo na hana msaada wowote nawe!!
 
Namwonea huruma huyu mzee kijana. Lakini jambo hili likifafanuliwa kimaandiko na kiimani ni kwamba huenda Diamond asingetelekezwa asingefika hapa alipo, kutelekezwa kuliongeza "Struggle for Existence ".Hivyo kama mimi ningemsaidia tu kwa sababu na yeye ni sehemu ya mafanikio yangu. Sisi huku kwetu huwa tunashukuru mtu akikunyima ulanzi kwa sababu siku hiyo hiyo tunakwenda kupanda vitindi, hivyo baada ya kufanikiwa aliyekunyima ulanzi tunamshukuru na kumsamehe kwa kuwa na yeye ni sehemu ya mafanikio yetu. Diamond msaidie babako machozi hayo anayotoa yatakuharibia future yako. Halafu by the way anahitaji Chakula na malazi tu ambavyo una uwezo navyo.
 
Huyu mzee hata hio kuumwa miguu naona kama anaZuga ili apate huruma.
Hii ni mfano kwa wanaume wanaowakimbia watoto wao!!
You are very right mkuu, watu waache kukimbia majukumu yao halafu wanakuja kujiliza liza kwenye media.

Awafuate wamiliki wa gazeti wamgawie kiasi cha mauzo ya nakala za gazeti.
 
Hili fundisho tunalipata wazazi ambao watoto wetu bado wadogo.
Sio tunadinya halafu tule kona, tudinye na tuwe tayari na majukumu ya matokeo ya Kudinya.
Vinginevyo ndio haya ya mzee Diamond.
Mzee anadhalilika tu ilihali mwanzo alikimbia majukumu.
Mama Diamond alifuata mfumo wa wanawake wa Kijapan....
Kama kuna mwanaume ana mpango wa kutelekeza mimba na mtoto ajifunze kwa huyu Baba Mond.
 
Kama kuna mzazi juha huyu jamaa anashika namba moja...mzazi mwenye kujitambua hawezi kukubali huu upuuzi wa kuhojiwa kwenye gazeti la udaku mambo binafsi yanayohusu familia yake
Huu ni upuuzi na upumbavu wa kiwango cha juu mno
Hivi kalipwa bei gani?
Hivi anajua jamaa wametengeneza bei gani kupitia hiyo habari
Huyu hajitambui na atafakari alipokosea kuliko kuja kulialia kwenye vyombo hovyo vya habari...huku ni kujidhalilisha
Labda kahaidiwa gawio baada ya mauzo. Amechemka sana, yeye anatakiwa kuitisha vikao vya ukoo kulijadili hili kifamilia na sio kutoa headlines za kijuha.
 
Hahahaaa!watu miaka michache ile ilopita walikua wanahustle..Wanaakka asubuhi wanawaza leo tunakula nini?? diamond na mamake wanahangaika japo wapate hela ya unga na dagaa wale wasavaivu hapa mjini..Walikua walikua wanaishi kwenye nyumba ya bibi yao tandale.Cjui kama sio huyo bibi kuwapa makazi wangelala wapi?diamond anaungua na jua kali la dar,Kachafuka mweusii kuuza mitumba wapate hela ya kula na mamake...Huku mzee kakumbatia wanawake wengine ndani ya nyumba yake hana habari..Ni mama diamond alikua na cheni yake ya dhahabu moja aloipebda sana akaenda kuiuza kwa sonara hela akmpa diaomnd aende studio akarekodi wimbo wake wa kwanza..Leo maisha yamebadilika unamuona wa maana!! nenda shamba kalime baba mungu kashakufunza!
 
Obama mwenyewe alisafiri all the way kutoka US mpaka ujaluoni ndani huko ili aone kaburi tu la baba yake kabla hajawa Rais halafu wengine wanakudanganya kijinga jinga tu ooh usimsaidie...look huyu ni damu yako jamaa ni mzazi wako achana na story saidia baba yako..
 
Mkuu, umeandika kwa hekima sana! Huyu Diamond, mimi nimeshamuona kama mpumbavu tu, kuna watoto
wa kiume wengine sisi hatuna baba (tunaumia) na kuna wengine walikosana na baba zao sana tu, na huwa wanawasamehe na kuwasaidia. Na kuna wengine walipoteana na baba zao kitambo huwa wanawatafuta
mpaka wanawapata na kama walishafariki huwa wanaumia
sana! Sasa huyu Diamond anamwacha baba yake bila ya msaada hivi ni kosa gani la mzee huyu ambalo halipaswi kusamehewa? Mzee anaishi maisha magumu, Diamond anajidai kutoa
misaada kwa watu baki bila ya kumjali baba
yake sasa ni huruma gani aliyonayo kwa watu baki kuliko
baba yake mzazi ambaye Diamond
bado anatumia jina lake katika majina yake
matatu. Basi kama Diamond hampendi baba yake, aache kabisa kutumia jina la baba yake, atumie jina la ukoo wa mama yake halafu huyu mama Diamond naye ni mtu wa majungu na huyu Diamond hata aende wapi huyo mzee ndio baba yake ni busara akamkumbuka!

Tazama pia upande wa pili, Zee Zima macheni shingoni na kiduku, Pamba kali katupia halafu anajidai hana hata Buku! Kama alikuwa na haki ya kumpotezea Diamond mpaka kufikia kumpiga hadharani kwa kosa la kwenda kumuomba pesa udogoni (Diamond alizungumza hilo akihojiwa) lakin Maisha yaliendelea kwa nini yeye ahisi lazima asaidiwe na Diamond! Inafaa asaidiwe ila si lazima na tabia yake ya kupewa vi elf kadhaa ahojiwe na Shigongo ili wauze gazeti inazidi kuvuruga uhusiano, Inaonekana hata akiahidiwa pesa huyu tapeli anaweza kumdhuru Mwanae. Ukiweza kupalamia na kutungisha Mimba lazima ujue pia una jukumu la kulea kitokanacho na Shahawa zako! Tupo wengi ambao Wazee wetu Mungu awarehemu walipata shida sana ya Maisha lakini walitulea, hata sisi pamoja na ugumu wa Maisha tulipanda na kushuka kulea watoto wetu ukipata pesa kidogo unanunua dagaa la home yeye enzi hizo mjanja yeye anawahi Mbowe Club.
 
Pamoja na alichomfanyia diamond na mzazi mwenzie enzi hizo, DIAMOND atapaa zaidi endapo atakuwa JASIRI na kumsamehe kisha kumsaidia babake!
Amfungulie mtaji, kwa kumpa pesa tu hajatatua tatizo!
 
Back
Top Bottom