Mkuu, umeandika kwa hekima sana! Huyu Diamond, mimi nimeshamuona kama mpumbavu tu, kuna watoto
wa kiume wengine sisi hatuna baba (tunaumia) na kuna wengine walikosana na baba zao sana tu, na huwa wanawasamehe na kuwasaidia. Na kuna wengine walipoteana na baba zao kitambo huwa wanawatafuta
mpaka wanawapata na kama walishafariki huwa wanaumia
sana! Sasa huyu Diamond anamwacha baba yake bila ya msaada hivi ni kosa gani la mzee huyu ambalo halipaswi kusamehewa? Mzee anaishi maisha magumu, Diamond anajidai kutoa
misaada kwa watu baki bila ya kumjali baba
yake sasa ni huruma gani aliyonayo kwa watu baki kuliko
baba yake mzazi ambaye Diamond
bado anatumia jina lake katika majina yake
matatu. Basi kama Diamond hampendi baba yake, aache kabisa kutumia jina la baba yake, atumie jina la ukoo wa mama yake halafu huyu mama Diamond naye ni mtu wa majungu na huyu Diamond hata aende wapi huyo mzee ndio baba yake ni busara akamkumbuka!