Nilikuwa na mambo mengi nikakosa muda wa kukujibu hoja zako.
Sawa umesema mambo mengi kuonyesha kwamba Askofu kugombea Ubunge ni dhambi au ni kosa, je unataka kusema Wachungaji na Maaskofu waliopo Bungeni kama Mchungaji Msigwa na wengine wengi wanadhambi gani? au wao wameingia Bungeni bila kuwa na Vyama vya kisiasa? au kosa langu ni kuwa mwanachama wa CCM?
Achacheni mawazo mafupi hakuna mtanzania asie na chama kwa sababu Tanzania haijawahi kuwa na Mgombea binafsi, ila kila anaetaka kugombea lazima asimamishwe na Chama chake.
Vivyo hivyo na hakuna mpiga kura anaeweza kupiga kura kuchagua mtu, lazima uchague mtu aliye ndani ya chama.
Pia kuhusu hoja yangu au mada yetu ilikuwa ni Tamko la TCF. Jukwaa hili la Wakristo Tanzania nilitofautia nao kwa kuwaelekeza Waumini kupiga kura ya hapana katiba inayopendekezwa.
Nadhani huelewi Askofu ni nani na TCF ni akinani. Narudia kusema kama kweli kuna hoja ya msingi kwamba katiba inayopendekezwa ni mbaya sawa nielezeni ni kipengele gani au ibara gani ili nami nisome kisha nifahamu kwamba ipo sababu ya kuikataa, ila sio kusema tu, kwa sababu fulani kakataa nawe kataa au kataza wengine sio sahihi kabisa.