Mkuu umeongea vizuri sana. Unaona sasa huyo gamba atawezaje kulikana gamba linaloharibu mazingira wakati yeye mwenyewe ni gamba? Kina Pengo magamba wale na kamwe sitegemei waseme ukweli wa mambo bila kukinga chama chao kwa kuwa kuwepo kwa ccm kunawakinga waendelee kufanya maovu kwa ulinzi kamili wa gamba lao. Maaskofu wameshauri mambo mengi kila wakati na wanasema ukweli wanaoujua ambao hata magamba wanajua isipokuwa hawapendi yasemwe hadharani. Sio kila asemaye Bwana Bwana ni kipenzi cha Mungu. Mwaka huu kimenuka ccm, kila kona kuchungu.
Wakuu kila mmoja wetu anaamini Mwenyezi Mungu wake na hii haina UBISHI! Lakini sasa hivi na wala siyo siri watu wanatumia DINI kama biashara tu. Mimi nikienda kanisani siendi kwa sababu ya ASKOFU au MCHUNGAJI fulani, hapana kwani hawa binadamu wamekuwa WALAGHAI MNO! Karibu makanisa mengi unaweza kuyalinganisha na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini! Nikiwa na maana kwamba, baadhi ya vyama vya siasa vilianzishwa kwa nia na malengo mazuri kama zilivyo baadhi ya DINI, lkn cha ajabu watu (VIONGOZI WAANDAMIZI) wanageuza hivi vyombo kama MALI ZAO au MIRADI YAO ya kutafutia UTAJIRI.
Hivyo basi ni kupoteza mda kuanaza kuongelea hawa MAASKOFI NJAA amabo maskini hawajui kuwa jamii imeisha wafahamu kama jamii ilivokwisha wafahamu wanasiasa wenye NJAA.
Wanajanvi angalia nchi za jirani kama KENYA hayo makanisa yanavyofanya USANII na kujipatia hela kwa kuwadanganya WAUMINI, na hiki ndo kitu kinacho anza kujitokeza hapa KWETU. ETI mtu mchungaji nani anapita na kufukuza PEPO, et anapita na kuwaombea watu na wanapona. HUU ni uongo mtupu kabisa.
My take: TUSIWAKUBALI hawa maaskofu njaa na tuwakatae kabisa. Mtu unaweza ukukaa nyumbani ukasali kwa kumuomba MUNGU wako unaye mtambua. Fanya mema kwa mfano wasaidie wenye shida kama una kauwezo fulani na hii ni zaidi ya kuamka ASUBUHI JUMAPILI eti ninakwenda kuombewa na MAASKOFU NJAA. TUWAKATAE KABISA!!!!