shokoshugi
JF-Expert Member
- Oct 13, 2015
- 333
- 563
'TIKITAKA' ZA DANGOTE AKIELEKEA KENYA!
Unamtambulisha msichana hadharani kuwa ni Bibi Arusi wako mtarajiwa kumbe hujafika hata kwa wazazi wake kujitambulisha! Sasa kaamua kuolewa na 'Mnyilemi Kindamba' wa Uchindile anadai wewe ni 'Kapufi Mwanansao' ambaye ni Mfipa wa Kirando hujui hata kuvua hao samaki!
Dangote naye anatangaza huko kuwa anafikiria kuwekeza kiwanda cha kusafisha mafuta huko Mombasa ambayo ina kina kirefu kuliko Tanga ambayo kina chake ni kifupi hakifai hata kupaki ngalawa au 'boti' za Mpiji!
Ninyi badala ya kujadili dili za nguvu na Kipruto, mkawa mnampenyezea Malkia Nzinga Mbande ili aanze kuwacharaza mijeledi akina 'ntukwe'!
Muiteni Muhehe wa Kiponzelo aje kukanusha hiyo 'ntiiti' maana ni bingwa wa kukanusha!
Badala ya kuajiri watu wenye uelewa na weledi katika timu za majadiliano ya kiuchumi lakini ninyi mnawajaza machawa wa kumsifia Malkia! Mijadala ya kiuchumi ni vita inayopiganwa na watu wenye fikra, siyo sehemu ya kuwapa ulaji machawa waliosaidia kupora uchaguzi wetu!
Kama hao washauri wenu wameshiriki 'mwili na damu' ya Yesu leo, watakuwa na ufahamu wa kujua hiki anachokiongea askofu hapa! Ila mimi naendelea kusoma komenti za kuniwishi Birthday baada ya watu 'Mbudya' kushindwa kunipulizia 'spray mwaka jana! Mimi sio Lema!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 10 Mei 2026; Saa 6:50 mchana