Mkuu nahifia anaweza akaitwa kuhojiwa uraia wake
Ndio wale waliosema sasa ni zamu yetu wananchi wakakataa.Hawa sio wale maaskofu wa Lowassa kweli??
......ANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.
Tuheshimu Nguvu ya hoja.
1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.
Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?
2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.
Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.
3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.
Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.
4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.
Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.
Belated Happy Birthday Tanzania.
Note: Naona maaskofu wameanza kuamka
.....Hawa ndio Maskofu tunaowahitaji sio wakina pengo ambao wanashibishwa hawajali hata waumini wao wanavyoteswa na serikali yao ya kiuchwara
......Hawa ndio Madokta sasa, Saaafi kabisa Ngoja Askofu Dr. Munga
Kama ni uhuru wa kucheza mziki na kushangilia mpira ni kweli upo sana.Uhuru upo sana hapa Tanzania, hapa cha kuangalia ni mipaka ya Uhuru. Hata mungu alipompa mwanadamu Uhuru akamwekea amri ili kuweka mipaka ya Uhuru. Sijaona aliyenyimwa Uhuru, ni watu hawajui namna ya kutumia Uhuru hapo ndo linapoanzia hiyo kauli ya kunyimwa Uhuru wanayosema watu
Sasa kama hayohayo ambayo yanaonekana ni makosa yakiwa upande wao kama wanachukulia kuwa si makosa, utakubalije kukosolewa na mtu wa namna hiyo. Vyama ya upinzani vinatakiwa vifanye evaluation, na ccm ifanye monitoring kwa serikali.Kama ni uhuru wa kucheza mziki na kushangilia mpira ni kweli upo sana.
Lakini jaribu kuwaambia watu furahi kuwa hapo wamekosea , ndo utajua hapa kwetu uhuru upo au haupo.
Kwa hiyo ukikosolewa unakasilika unachukua rungu , kwa nini na wewe usimkosoe tu mkosoaji wako?Sasa kama hayohayo ambayo yanaonekana ni makosa yakiwa upande wao kama wanachukulia kuwa si makosa, utakubalije kukosolewa na mtu wa namna hiyo. Vyama ya upinzani vinatakiwa vifanye evaluation, na ccm ifanye monitoring kwa serikali.
Mfano alioutoa wa mwewe, kwamba hata ukimpa vifaranga wengi na kumfungia ama kumnyima uhuru, siku akiupata huo uhuru, hata hao vifaranga atawaacha hapo aruke juu kwa uhuru, pamoja na kwamba mara nyingi akiruka juu, huwa ni vifaranga anatafuta.Sikiliza mkuu, mwanadamu ameubwa na MUNGU na kuzawadia uhuru.
Hivyo kujaribu kupora uhuru wa mwanadamu huko ni kupora zawadi aliyopewa na MUNGU.
Sikiliza , kwa nature ya binadamu ni bora akose vitu vyote vya dunia hii kama nyumba gari na chakula kizuri ,lakini si kukosa uhuru.
Mtu yoyote anayejaribu kupora uhuru wa mwanadamu mwenzake huyu atakuwa anakaribisha janga ambalo hataweza kulituliza badae.
Mungu mwenyewe amempa uhuru mwanadamu wa kumuabudu au kutokumuabudu, na hii haimpi shida kabisa.
Uyo pengo atakua usalama wa taifa tu hakuna kardinal wa ivoHawa ndio Maskofu tunaowahitaji sio wakina pengo ambao wanashibishwa hawajali hata waumini wao wanavyoteswa na serikali yao ya kiuchwara
ANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.
Tuheshimu Nguvu ya hoja.
1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.
Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?
2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.
Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.
3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.
Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.
4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.
Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.
Belated Happy Birthday Tanzania.
Habari zaidi soma;
Askofu Bagonza akosoa kauli ya 'Aliyepewa mimba asirudi', ahoji makosa ya viongozi yangekuwa mimba, wangekuwa na ngapi?
Rev Bagonza Stresses Need for Economic Recovery Programs
Dr. Bishop Bagonza wa KKKT Karagwe: Watanzania hawafaidi rasilimali za nchi kutokana na dhuruma, rushwa na Ufisadi
Note: Naona maaskofu wameanza kuamka.