Kuna maneno kaandika leo na Uzi uliletwa humu..bahati mbaya Mods wameufuta. So sad..
Baba Askofu Dr. Bagonza ni level zingine
Cc: OKW BOBAN SUNZU
Baba Askofu Dr. Bagonza ni level zingine
Cc: OKW BOBAN SUNZU
Nilitamani niyaoneKuna maneno kaandika leo na Uzi uliletwa humu..bahati mbaya Mods wameufuta. So sad..
Baba Askofu Dr. Bagonza ni level zingine
Cc: OKW BOBAN SUNZU
Yule aliyehojiwa ni Niwemugizi wa jimbo la NgaraKama huyu askofu ndiye aliyehojiwa na uhamiaji basi sina cha kusema
Be blessed baba askofu.
Wameanza kukereka, lakini wamegawanyika, wapo watakuja na kusema sio MSIMAMO WA KANISAANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.
Tuheshimu Nguvu ya hoja.
1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.
Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?
2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.
Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.
3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.
Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.
4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.
Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.
Belated Happy Birthday Tanzania.
Habari zaidi soma;
Askofu Bagonza akosoa kauli ya 'Aliyepewa mimba asirudi', ahoji makosa ya viongozi yangekuwa mimba, wangekuwa na ngapi?
Rev Bagonza Stresses Need for Economic Recovery Programs
Dr. Bishop Bagonza wa KKKT Karagwe: Watanzania hawafaidi rasilimali za nchi kutokana na dhuruma, rushwa na Ufisadi
Note: Naona maaskofu wameanza kuamka.
Mpaka comment no. 27 sijaona Mlumumba hata mmoja.
Mkuu nahifia anaweza akaitwa kuhojiwa uraia wake
Sana mkuu! Quite unbelievable! Kumbe wale wasiyoongea ndo huwa wana nondo za ukweli kabisa. This is the best.
Ndo maana ninaamini uminyaji wa demokrasia ni hatari sana! Kwasababu kuna watu wenye akili sana ambao hawana habari na siasa, lakini mambo kama yanayoendelea sasa nchini, yanaweza kusababisha watu wa aina hiyo wakaingiza nguvu na maarifa na akili zao kwenye siasa kwa nia ya kukomesha ukandamizaji. Hii posti kwangu hadi usawa huu ni ya mwaka!
hii nimeiona leo,,,, huyu askofu ni nondo aisee ,,,wale wenye hoja za uchama siwaoni humu