Baba Askofu Dr. Benson Bagonza: Tuheshimu nguvu ya hoja

Baba Askofu Dr. Benson Bagonza: Tuheshimu nguvu ya hoja

ANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.

Tuheshimu Nguvu ya hoja.

1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.

Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?

2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.

Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.

3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.

Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.

4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.

Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.

Belated Happy Birthday Tanzania.


Note: Naona maaskofu wameanza kuamka
Hapana,baba Askofu kwa andiko lako hili lazima nirudi kanisani......naam!!! nilikata tamaa kabisa na kanisa nikadhani kuwa kanisa limejaa viongozi wanafiki na waoga , aaa kumbe nilikosea , viongozi wenye busara bado mpo kanisani

Baba kwa neema ya MUNGU jumapili hii tutakuwa wote kwenye ibada.

Kumbe tarehe 9 December tulifurahi si kwa sababu tulipata serikali inayoongozwa na mwafrika mwenzetu , bali tulifurahi kwa kuwa tulipata uhuru!!!!

kumbe uhuru ni mhimu kuliko serikali!!!

Ubarikiwe sana baba Askofu.
 
Kanisa likisema taifa litapona
Siku kanisa litapojitokeza hadharani na kupinga waziwazi ukiukwaji wa haki za binaadamu,taifa kitapona,maana sauti ya kanisa ni nzito sana,Sauti ya kanisa inapenya kwenye masikio ya watawala
Kanisa kama kanisa wajibu wake ni kukemea maovu,kuomba,na kuelekeza njia sahihi ya binaadamu kupita,na njia sahihi ya kupita ni kuishi ndani ya christu yesu baba na mungu kweli,alfa na omega,yeye ni mwanzo na mwisho
Christu yesu alikemea watawala wa rumi bila uoga,na kwa maana hiyo basi,kama kanisa la leo ni kanisa lililojegwa chini ya mwamba,maanake ni kanisa la yesu christo,na Kama ni kanisa la yesu christu lazima liwakemee watawala wanaokiuka haki za binaadamu kuishi kwa kisingizio chochote kile,hata kama ni kisingizio cha maendeleo,huo ndio wajibu wa kanisa la yesu christu mwana wa Nazareth
Kanisa karibu litasema,na kanisa likisema taifa litapona
 
Hapana,baba Askofu kwa andiko lako hili lazima nirudi kanisani......naam!!! nilikata tamaa kabisa na kanisa nikadhani kuwa kanisa limejaa viongozi wanafiki na waoga , aaa kumbe nilikosea , viongozi wenye busara bado mpo kanisani

Baba kwa neema ya MUNGU jumapili hii tutakuwa wote kwenye ibada.

Kumbe tarehe 9 December tulifurahi si kwa sababu tulipata serikali inayoongezwa na mwafrika mwenzetu , bali tulifurahi kwa kuwa tulipata uhuru!!!!

kumbe uhuru ni mhimu kuliko serikali!!!

Ubarikiwe sana baba Askofu.
Mkuu uchwara nyuzi kama hizi hazipendi kabisa
 
“Kumbukumbu zinapokuwa nyingi kuliko ndoto....,” Huu mstari umeniliza! Uko point namba 4 hapo juu.

Kwa kifupi Askofu katumia tafsida. Huu mstari ulitakiwa usomeke hivi....”kumbukumbu za mambo mabaya zinapokuwa nyingi kuliko ndoto....”
Asante sana...ongezea "kuliko ndoto" mbaya.

Kwamba kuna mambo (mabaya) yanafanyika haingii akilini kama ni halisia kiasi cha mtu kuyakumbuka na kuamini ni halisia. Yalipaswa yawe ndoto "mbaya" tu ambapo mtu atakapojiridhisha kama ni ndoto, huishia kuyapuuza na kuendelea na hamsini zake. Lakini dah,,,,,, sio ndoto. Ni halisi.
 
Msambwata Haya maneno yametulia.
Askofu amesema ninachokiamini kuwa wakati umefika kutambua tunachokihitaji ni uhuru wa mawazo.

Kujitoa ktk eneo hili kutatudumaza kifikra. Siyo Sawa kuwategemea wahama kutusemea bali uhuru pia uwepo kwa wasiopenda vyama kuwahoji kwa uhuru wonapotulisha hoha
Uhuru wa mawazo unasaidia nn kama wazo halichukuliwi
 
Aliyo yaongea kuhusu uhuru ni kweli taifa lolote lina hitaji sana uhuru kuliko kitu chochote nnacho shangaa tulipo pata uhuru ghafla tulianza kutumia tena sheria zile zile za mkoloni pia baadh ya vyombo vya usalama aka police wakati wa mkoloni jeshi hili lilikua linaitwa police force na cha kushangaza bado linaitwa hivyo hivyo badala ya kuitwa police service now jeshi hili linahitaji maboresho liwe na little sense ya demokrasia na sio maguvu kila saa lakini kwa vile lina service upande wao they don't care.
 
Uhuru wa mawazo unasaidia nn kama wazo halichukuliwi
Sikiliza mkuu, mwanadamu ameubwa na MUNGU na kuzawadia uhuru.

Hivyo kujaribu kupora uhuru wa mwanadamu huko ni kupora zawadi aliyopewa na MUNGU.

Sikiliza , kwa nature ya binadamu ni bora akose vitu vyote vya dunia hii kama nyumba gari na chakula kizuri ,lakini si kukosa uhuru.

Mtu yoyote anayejaribu kupora uhuru wa mwanadamu mwenzake huyu atakuwa anakaribisha janga ambalo hataweza kulituliza badae.

Mungu mwenyewe amempa uhuru mwanadamu wa kumuabudu au kutokumuabudu, na hii haimpi shida kabisa.
 
Huyu askofu ni mtz kweli achunguzwe harafu apimwe mkojo, ni mchochezi haijawa kutokuea akamatwe
 
Safi sana, hawa wawili wamelianzisha, next week wataanza wachungaji. Afu Post kama hz znazosisitiza kuhusu kurumbana kwa hoja, huwezi kuwaona wale vijana wenye akili za kijani.
Nikushangae tu wewe na wenzio wa uoande ule mnavyoshabikia hoja za Askofu pasipo kuzichambua kwa kina. Ni aibu kuyatafsiri maneno ya kifalsafa na kiumini, kisiasa.

Aliyoyasema Askofu ni tahadhari kwa viongozi wa vyama vya siasa, hasa upinzani, ambao matukio ndiyo imekuwa agenda kuu, na siyo Sera za kudumisha Uhuru wetu.
 
Sikiliza mkuu, mwanadamu ameubwa na MUNGU na kuzawadia uhuru.

Hivyo kujaribu kupora uhuru wa mwanadamu huko ni kupora zawadi aliyopewa na MUNGU.

Sikiliza , kwa nature ya binadamu ni bora akose vitu vyote vya dunia hii kama nyumba gari na chakula kizuri ,lakini si kukosa uhuru.

Mtu yoyote anayejaribu kupora uhuru wa mwanadamu mwenzake huyu atakuwa anakaribisha janga ambalo hataweza kulituliza badae.

Mungu mwenyewe amempa uhuru mwanadamu wa kumuabudu au kutokumuabudu, na hii haimpi shida kabisa.
Uhuru upo sana hapa Tanzania, hapa cha kuangalia ni mipaka ya Uhuru. Hata mungu alipompa mwanadamu Uhuru akamwekea amri ili kuweka mipaka ya Uhuru. Sijaona aliyenyimwa Uhuru, ni watu hawajui namna ya kutumia Uhuru hapo ndo linapoanzia hiyo kauli ya kunyimwa Uhuru wanayosema watu
 
Back
Top Bottom