Baba Askofu Dr. Benson Bagonza: Tuheshimu nguvu ya hoja

Kwakweli binafsi ,ninekuwa mzito mnoo kwenda kanisani kwasababu ya ukimya wa viongozi wale walioushambulia utawala wa kidemokrasia wa kikwete,na kuunyamazia huu utawala wa kidkteta uchwara ....
Naona sasa nguvu za kurudi kanisani zitaanza kurejea hawa viongozi wa kiroho wakiacha unafiki wa kuunyamazia utawala huu...
 
“Kumbukumbu zinapokuwa nyingi kuliko ndoto....,” Huu mstari umeniliza! Uko point namba 4 hapo juu.

Kwa kifupi Askofu katumia tafsida. Huu mstari ulitakiwa usomeke hivi....”kumbukumbu za mambo mabaya zinapokuwa nyingi kuliko ndoto....”
Nimerudia mara kadhaa kusoma hii point namba 4, akili kubwa sana imetumika hapa, kama ni ngumi basi hii point iko katika uzito wa juu
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.

Tuheshimu Nguvu ya hoja.

1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.

Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?

2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.

Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.

3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.

Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.

4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.

Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.

Belated Happy Birthday Tanzania.

Note: Naona maaskofu wameanza kuamka
Baba Askofu....where have you been baba?

wewe baba ni zaidi ya kilo-Mruma (Mruma x 1000)!
 
Duh! Huyu askofu, ni great thinker! Wala siyo kuamka tu. Kwanza watu wanapokuwa kimya, haina maana kuwa hawajali au hawana chakusema, bali ni uvumilivu, hekima na busara.

Lakini kuna point inafikia, ambapo wenye busara wanatambuwa kuwa “hata mawe yataongea”.
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.

Tuheshimu Nguvu ya hoja.

1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.

Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?

2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.

Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.

3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.

Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.

4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.

Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.

Belated Happy Birthday Tanzania.

Note: Naona maaskofu wameanza kuamka
Yani very short and clear, yet precisely on the point! Nimependa sanaaa haya maneno na ujumbe ulioyabeba!
 
Askofu ameongea kwa busara sana
Sana mkuu! Quite unbelievable! Kumbe wale wasiyoongea ndo huwa wana nondo za ukweli kabisa. This is the best.

Ndo maana ninaamini uminyaji wa demokrasia ni hatari sana! Kwasababu kuna watu wenye akili sana ambao hawana habari na siasa, lakini mambo kama yanayoendelea sasa nchini, yanaweza kusababisha watu wa aina hiyo wakaingiza nguvu na maarifa na akili zao kwenye siasa kwa nia ya kukomesha ukandamizaji. Hii posti kwangu hadi usawa huu ni ya mwaka!
 
Maaskofu mwaka huu mmeamua, sijui Askofu mwenzenu yye huwa anawaza nini au anaogopa kuhojiwa uraia wake
_Pengo la utotoni_
 
Back
Top Bottom