Baba Askofu Dr. Benson Bagonza: Tuheshimu nguvu ya hoja

Msambwata

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2017
Posts
1,307
Reaction score
1,500
ANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.

Tuheshimu Nguvu ya hoja.

1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.

Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?

2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.

Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.

3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.

Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.

4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.

Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.

Belated Happy Birthday Tanzania.

Habari zaidi soma;
Askofu Bagonza akosoa kauli ya 'Aliyepewa mimba asirudi', ahoji makosa ya viongozi yangekuwa mimba, wangekuwa na ngapi?

Rev Bagonza Stresses Need for Economic Recovery Programs

Dr. Bishop Bagonza wa KKKT Karagwe: Watanzania hawafaidi rasilimali za nchi kutokana na dhuruma, rushwa na Ufisadi

Note: Naona maaskofu wameanza kuamka.
 
Hawachelewi kumpima mkojo...

Kiukweli viongozi as dini watachukua sehemu kubwa sn ya lawama kwa ukimya wao huku mambo yakiharibika katiba na sheria as nchi zinachezewa huku viongozi wakuu wakiapa kwaneno na matendo kupeleka maendeleo na kupendelea kwa kwao.

Ntasilitika sana kuja kusikia hao viongozi wakiombea amani badala ya kuombea haki kutamalaki maana haki ndilo tunda la amani
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA WA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE
SOMO LA URAIA: UHURU MIAKA 56.

Tuheshimu Nguvu ya hoja.

1. Hadi Desemba 1961, tulikuwa tunapigania kupata uhuru, siyo serikali. Kwa hiyo kilichopatikana siku hiyo usiku ni "Uhuru", si serikali. Serikali ilikuwapo hata kama hatukuwa tunaipenda.

Wakati wote tunaenda mpaka Umoja wa Mataifa (UNO), serikali ilikuwapo lkn hatukuwa na uhuru. Siku hizi serikali ni muhimu kuliko uhuru. Tujadili kwa nini?

2. Katika utawala wa kikoloni, serikali ndiyo huinyoosha nchi, na nchi ni wananchi. Katika utawala bora, (uongozi), wananchi ndio wanaoinyoosha serikali.

Kunyoosha ni dhana ya kikoloni inayoamini wananchi wana tatizo! Wakoloni walidai wanatunyoosha ili kutuendeleza. Kumnyoosha aliyekupigia kura inahitaji uagane na ustaarabu au kuuweka pembeni kwa makusudi maalum. Tujadili.

3. Uhuru hauna sura wala umbo; ni dhana na tunu kwa taifa. Ktk za nchi za kidemokrasia, uhuru ndicho kitu cha kipekee kinacholindwa kwa nguvu zote.

Ukiona nguvu nyingi (siyo akili), zinatumika kulinda watu badala ya kulinda uhuru, ujue taifa hilo linakaribia mwisho wa kufikiri. Tujadili.

4. Kwa mantiki ya niliyosema juu, utakuta vijana wengi wana kumbukumbu nyingi kuliko ndoto. Kumbukumbu zikiwa nyingi kuliko ndoto ni dalili ya taifa kuwa limesimama. Jana haiwezi kuwa bora kuliko kesho tukawa salama.

Vijana wanahitaji ndoto nyingi kuliko kumbukumbu. Tujadili bila kugombana wala kukashifiana. Utaifa hujengwa kwa fikra pevu. Utaifa na uzalendo haujengwi kwa matofali, zege wala bunduki.

Belated Happy Birthday Tanzania.

Note: Naona maaskofu wameanza kuamka
Tunahitaji watu kama huyu kuiweka Tz katika mstari . Wengine wanaoheshimika huomba hata wakati wa kuapishwa mkuu wa nchi huwezi kusikia chochote .

Baba askofu ubarikiwe kwa kuwa mkweli katika nafsi yako. Nchi inawahitaji.
 
Msambwata Haya maneno yametulia.
Askofu amesema ninachokiamini kuwa wakati umefika kutambua tunachokihitaji ni uhuru wa mawazo.

Kujitoa ktk eneo hili kutatudumaza kifikra. Siyo Sawa kuwategemea wahama kutusemea bali uhuru pia uwepo kwa wasiopenda vyama kuwahoji kwa uhuru wonapotulisha hoha
 
Back
Top Bottom