Baba Askofu Dr. Bagonza: Mapenzi ya Mungu na Mapenzi yetu

Baba Askofu Dr. Bagonza: Mapenzi ya Mungu na Mapenzi yetu

Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD), daktari wa Falsafa na Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____________________________
MAPENZI YA MUNGU na MAPENZI YETU.

Siyo kila kifo ni mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anajua kila kifo. Siyo kila ajali ni Mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anaiijua kila ajali.

Tukumbuke alimuacha Mwana wake kuuawa hata kama alikuwa na uwezo wa kuzuia. Alimwacha Mwana wake kusalitiwa hata kama alikuwa na uwezo wa kumkomesha msaliti wake.

Hatua zote za maendeleo zina ukurasa wa majanga. *Dreamliner na Bombadier usiote janga lake. SGR janga lake ni kiama. Stiggler's Gorge ina janga la kuangamiza mamilioni kwa siku moja kingo za bwawa zikipasuka. Meli mpya ya abiria 2000 ni kaburi la halaiki linaloelea majini.*

Uwezo wetu upimwe kwa kushughulikia majanga, si kwa kuchochea majanga. Poleni wafiwa, Ugua pole majeruhi, Tufarijiane Watanzania.

#MyTake:
Falsafa ni somo gumu, halijawahi kueleweka kwa wote. Lakini pamoja na ugumu wake, tuzitafakari falsafa za baba Askofu Bagonza, na tujitahidi kuzielewa. Zina mengi ya msingi.!
maneno haya mujarab ya Baba Askofu kwa huyu Nebukadneza wetu hamna tofauti na kutwanga maji kwenye kinu tu!!
 
Hapo hakuna critical argument bali kuna emotional argument.Hizo huwa sizijadili.
kwa nilivyomuelewa baba Askofu hoja yake ipo hapa, "hatua zote za maendeleo zina majanga hivyo uwezo wetu upimwe kwa kushughulikia majanga".
hatua za maendeleo ni zipi kazitaja tumenunua ndege, meli mpya ya abiria 2000, na tunajenga strigglers gorge. vitu vyote hivo sio vigeni hapa duniani na vyote vimeshaleta majanga makubwa yaliopelekea vifo vya watu na uharibifu wa mali na miundombinu mbalimbali.
sasa sisi kama watanzania tujiulize; kwasababu vitu hivo vinamajanga tusinunue ndege?,tusinunue meli? tusijenge mabwawa? jibu ni hapana, ila tunapaswa kujiuliza tunajiandaa vipi kushughulikia kuzuia majanga yasitokee na tunakabiliana nayo vipi pindi yanapotokea majanga. tumenunua kivuko je tunazingatia sheria na taratibu za kuendesha kivuko?, idadi ya watu na mizigo tunayopakia ina endana na uwezo wa kivuko?, tunazingatia sheria za usalama wa anga?, tuna vifaa vya uwokozi vya kutosha?.
iyo ndio hoja ya Baba Askofu na sio mihemuko unayosema wewe.
 
Dah.. Chadema ni wajinga sana walahi!

Kila andiko wao huona kwa upande wa siasa basi! Tena likiwa limetolewa na mkosoaji wa Magufuli.

Kwa akili za wana chadema wanaona askofu kasema tusijenge mabwawa, tusinunue meli wala ndege kwa sababu zina majanga!

Ni heli unyimwe kipato kuliko akili za kutafakari!
 
Huyo anafanya siasa tu..kwa nini agusie miradi ya maendeleo ambayo chadema wanaipinga..?mbona mabasi yanapata ajali..boda boda na vingine..hata magari binafsi..mwanadamu huwa akikaa hafikirii mabaya..kwenye ndege kuna miamvuli ya kujiokoa lakini hata siku moja husikii ndege imepata ajali na kuna watu wawili walijiokoa kama ambavyo tunaagizwa kufanya tukiingia kwenye ndege ( hii ni kwa waliowahi kupanda)..inapotokea ajali watu hughafirika na unaweza usione hata hilo boya hususani kwa ajali ya mara moja na haraka...lakini ukiangalia hii ajali ilikuwa inaepukika..ni suala la uzembe na rushwa kwa wasimamizi wa kivuko..

What a shame?

Mbona....mbona.....mbona....mbona.....

Kwa mbona hizi, maana yake hili ni la kawaida, siyo?

Kwani kivuko ni Bodaboda bibie??

Acheni watu waseme. Kuna shida, kuna makosa ktk yote haya. Chutameni, ficheni aibu yenu!!
 
Siku hizi matukio yamekuwa kiki za kisiasa.Mea culpa
Matukio ya ajari kama hizi za kizembe huwezi kuzitofautisha na siasa hata siku moja!! Siasa ni kila kitu, kwani wasimamizi wa kivuko hiki wanatekereza ilani ya chama kinachoongoza nchi!! Wanaposhindwa kusimamia majukumu yao na kupelekea vifo vingi kiasi hiki lazima serikali ndio ya kulaumiwa!! Vifaa vya uokozi vinakosekana ni jukumu la nani kuvinunua?? Hakuna waokoaji wenye ujuzi nani wa kulaumiwa?? Miaka yote ajari kibao za majini zinatokea lakini hatuna la kujifunza tu?? Na ndio maana kwa nchi za watu hadi kufikia sasa kuna watu wangekuwa wameshajiuzuru/kufukuzwa kazi. Unakuja na hoja eti captain kwanza hakusafiri lazima akamatwe!! Kama alikuwa off, au ana udhuru?? Eti alikuwa anaendesha day worker? Yaani ukienda huko visiwani ndio utajua ni kudra za mwenyezi mungu tu,. SERIKALI HAIWEZI KWEPA LAWAMA KWENYE HILI.
 
Uwezo wa baadhi ya waTanganyika kufifiri ni mdogo sana....achilia mbali kuelewa.
 
Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD), daktari wa Falsafa na Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____________________________
MAPENZI YA MUNGU na MAPENZI YETU.

Siyo kila kifo ni mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anajua kila kifo. Siyo kila ajali ni Mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anaiijua kila ajali.

Tukumbuke alimuacha Mwana wake kuuawa hata kama alikuwa na uwezo wa kuzuia. Alimwacha Mwana wake kusalitiwa hata kama alikuwa na uwezo wa kumkomesha msaliti wake.

Hatua zote za maendeleo zina ukurasa wa majanga. *Dreamliner na Bombadier usiote janga lake. SGR janga lake ni kiama. Stiggler's Gorge ina janga la kuangamiza mamilioni kwa siku moja kingo za bwawa zikipasuka. Meli mpya ya abiria 2000 ni kaburi la halaiki linaloelea majini.*

Uwezo wetu upimwe kwa kushughulikia majanga, si kwa kuchochea majanga. Poleni wafiwa, Ugua pole majeruhi, Tufarijiane Watanzania.

#MyTake:
Falsafa ni somo gumu, halijawahi kueleweka kwa wote. Lakini pamoja na ugumu wake, tuzitafakari falsafa za baba Askofu Bagonza, na tujitahidi kuzielewa. Zina mengi ya msingi.!

Kesho tumkute uhamiaji
 
Mwanasiasa aliyejificha kwenye dini.Afanye moja aeleweke.
Kwanini mnapata tabu mtu anapoeleza ukweli? Siyo kila anayeeleza ukweli ni mwanasiasa. Siasa ina maslahi kwa wanaoifanya kama kazi. Hili alilosema baba askofu ina manufaa gani kwake?
 
Back
Top Bottom