Baba Askofu Dr. Bagonza: Mapenzi ya Mungu na Mapenzi yetu

Baba Askofu Dr. Bagonza: Mapenzi ya Mungu na Mapenzi yetu

Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD), daktari wa Falsafa na Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____________________________
MAPENZI YA MUNGU na MAPENZI YETU.

Siyo kila kifo ni mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anajua kila kifo. Siyo kila ajali ni Mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anaiijua kila ajali.

Tukumbuke alimuacha Mwana wake kuuawa hata kama alikuwa na uwezo wa kuzuia. Alimwacha Mwana wake kusalitiwa hata kama alikuwa na uwezo wa kumkomesha msaliti wake.

Hatua zote za maendeleo zina ukurasa wa majanga. *Dreamliner na Bombadier usiote janga lake. SGR janga lake ni kiama. Stiggler's Gorge ina janga la kuangamiza mamilioni kwa siku moja kingo za bwawa zikipasuka. Meli mpya ya abiria 2000 ni kaburi la halaiki linaloelea majini.*

Uwezo wetu upimwe kwa kushughulikia majanga, si kwa kuchochea majanga. Poleni wafiwa, Ugua pole majeruhi, Tufarijiane Watanzania.

#MyTake:
Falsafa ni somo gumu, halijawahi kueleweka kwa wote. Lakini pamoja na ugumu wake, tuzitafakari falsafa za baba Askofu Bagonza, na tujitahidi kuzielewa. Zina mengi ya msingi.!
Sisi kwa imani yetu tunaamini kila Kifo ni Mapenzi ya Mungu, kama Mungu hakutaka ufe basi huwezi kufa. Vile vile, kila Kifo kina sababu yake. Hakuna Kifo kinachotokea bila kuwepo sababu. Hivyo, hata uzembe wa binadamu ni sehemu ya sababu ya Kifo. Ndiyo maana maandiko yanasema, Kifo ni siri kubwa anayoijua M/mungu pekee. Binadamu angeijua siri hii, basi leo hii tusingekua tunakufa.

Nachelea kuamini kwamba, kauli hii ya Baba Askofu ni ya Kiimani. Kwasababu hakuna imani inayoweza kupinga mapenzi ya Mungu kwenye kila jambo limtokealo binadamu. Yaani hakuna exceptional kwenye kazi ya Mungu. Uhai na Kifo cha Binadamu vyote vinatokana na mapenzi yake.
 
Rudi shule mkuu huwezi kuelewa mambo mazito kama haya ya Baba askofu(phd)
Unaepaswa kurudi shule ni wewe unaeaminishwa kila kitu unakurupuka bila uchambuzi wako mwenyewe na kuanza kutukana kisa kajibiwa baba yako (phd)
 
Hebu acha ubahili wa kutumia akili mkuu, alicho shauri Askofu hapo ni kuwa na taadhari kwa kila mradi wa maendeleo unaofanyika pia kuwe na utararibu wa kukabiliana na side effects zake ,think out of politics unaweza kupata point hapo. Epuka siasa za [emoji122][emoji122][emoji122] kila kitu.
Hapo unapoishi kukitokea bonde la ufa umejiandaaje kukabiliana nalo maana unatakiwa tahadhali kama ulivyojieleza..!
 
Kweli, sasa nmeamini akili ndogo si rahisi kumuelewa bagonza.
Kama ni akili ndogo.. ni zero brain (yaani sufuri )pekee wanaoamini kila kitu kwa kuwa Dr fulani kasema, na ni wale wanaoamini binadamu alitokana na nyani hatua kwa hatua akawa binadamu kamili wakati hao nyani wapo na binadamu wapo.
 
Baada ya kusoma andiko hili na coment zake naanza kuona ile nadharia ya "allegory of the cave" au Asitiria ya Pango ya ndg. Plato alitutolea sisi watanzania. Yaani kuna watu naona kabisa wanavyoshindwa kuuona ukweli kama ulivyo na kuuona ukweli kwa jinsi unavyojidhihirisha machoni pao. Niishie hapa tu kwa leo
 
Back
Top Bottom