kwa nilivyomuelewa baba Askofu hoja yake ipo hapa, "hatua zote za maendeleo zina majanga hivyo uwezo wetu upimwe kwa kushughulikia majanga".
hatua za maendeleo ni zipi kazitaja tumenunua ndege, meli mpya ya abiria 2000, na tunajenga strigglers gorge. vitu vyote hivo sio vigeni hapa duniani na vyote vimeshaleta majanga makubwa yaliopelekea vifo vya watu na uharibifu wa mali na miundombinu mbalimbali.
sasa sisi kama watanzania tujiulize; kwasababu vitu hivo vinamajanga tusinunue ndege?,tusinunue meli? tusijenge mabwawa? jibu ni hapana, ila tunapaswa kujiuliza tunajiandaa vipi kushughulikia kuzuia majanga yasitokee na tunakabiliana nayo vipi pindi yanapotokea majanga. tumenunua kivuko je tunazingatia sheria na taratibu za kuendesha kivuko?, idadi ya watu na mizigo tunayopakia ina endana na uwezo wa kivuko?, tunazingatia sheria za usalama wa anga?, tuna vifaa vya uwokozi vya kutosha?.
iyo ndio hoja ya Baba Askofu na sio mihemuko unayosema wewe.