Baba ake Ommy Dimpoz alalamika kutengwa na mwanae

Maisha yao kwa ujumla hatuyajui, wala hatujui uyo Ommy kalelewaje

Ila kubali kataa Watanzania wengi kwenye kulea wazazi tunamjali sana mama, baba cyo kiivyo
Ndiyo maana nimesema kama alimterekeza ni sawa ila kama hakumterekeza si sawa.
Kumjali mama haimaanishi umuache baba aishi maisha ya ajabu wakati wewe ukisafiri na kula bata ukijisifia umelipa maelfu ya dollar kuingia mighahawa na sehemu za starehe.
Unaweza kumjali mama kwa kumpa zaidi kuliko baba lakini siyo kumuacha kabisa baba kama alikulea aishi maisha hayo wakati uwezo unao.
 
Hao ndio wazazi wapuuzi tu, yeye mzazi ndio anatakiwa atafute mali kwa ajili ya kumuachia mwanae urithi, na sio Omary kumtunza huyo dingi.... Yeye miaka hiyo 64 alikuwa anafanya nini hadi leo ashindie mihogo, si alikuwa anakula bata na vimada? Aache upuuzi wake.
Baba anaumia kuona mastaa Wengine wanawajali wazazi wao lkn mwanae hampigii hata cmu
Nayeye anamuona kwenye TV tu kama watu wengine
 
Duuh! Kama hamjali kweli sio sawa aisee.

Ila upande wa pili wa shilingi je katika makuzi ya huyo Ommy je Baba alishiriki mpaka kufika alikofika au ndio alihangaika na Mama pekee halafu yeye anakuja na malalamiko baada ya kuona amekuwa mtu mzima ikiwemo na umaarufu alionao.
Hii ndo shida ya wazaz wengi (baba) wanatelekeza watoto wao wakisha fanikiwa waanza kelele, binafsi mm n mmoja wapo so naona wanachokifanya diamond na ommy ni sawa tu, nimepitia wakat mgumu sana nabado napambana sidhan kama ntakuja kumtazama mzee wangu vizur
 
Watoto wa kiume wengi mapenzi yao kwa mama tu...
Hata cwez kumlaum Ommy kwa anachokifanya
Kwasababu watu wengi huamin baba anauwezo wa kujikim mahitaji yake mwenyewe bila kupatiwa Msaada
Sasa huyu Omary mama'ake si alishakufaga kwann asihamishie hayo mpnz kwa baba'ake
 
Kama alimterekeza ni sawa lakini kama hakumterekeza haiwezekani ule bata halafu eti uje na utetezi wa kiboya kama huo eti watu wengi uamini baba anaweza kujikimu mahitaji yake mwenyewe.
Yani uwe na maisha mazuri mzazi wako ana miaka 64 anahangaika na bajaj useme anaweza kujitunza mwenyewe huo ni ujinga wa kiwango cha rami
Itakuwa alimtelekeza kama babake mond alivyofanya. Mungu anamnyoosha kabla hajafa
 
Mzazi ni mzazi regardless alikutenda nini. Hata uwe na justification gani ....ukimtelekeza laana itakutafuna tu one day .... kama unabisha hewala lakini uliza waliokula chumvi kidogo wakupe shuhuda ....mzazi kushindwa kukuachia urithi wowote hiyo itabakia adhabu kwake na pengine ndio anapitia adhabu yenyewe kwa namna nyingine lakini wewe hupaswi kumtelekeza kwa makusudi.
Kwani na wewe umetelekeza watoto? Anza kuwakumbuka na uwapelekee matunzo yasikukute ya baba mond na baba dipoz
 
Mchz yuko bize kumpiga "pipe" mama wa mwenzie kumbe kajisahaulisha kumsaidia dingi ake
 
Hii ndo shida ya wazaz wengi (baba) wanatelekeza watoto wao wakisha fanikiwa waanza kelele, binafsi mm n mmoja wapo so naona wanachokifanya diamond na ommy ni sawa tu, nimepitia wakat mgumu sana nabado napambana sidhan kama ntakuja kumtazama mzee wangu vizur
Saa nyingine huwa hakuna jinsi sababu ukiangalia mtu amepigika enzi hata kutoa support ilikuwa hamna eti leo amesimama ndio anakuja. Hapo kumsaidia lazima kujifikiria mara mbili aiseee.

Kama naye alikuwa aina hiyo ya wanaume hata hapaswi kulalama kwa kweli.
 
Akili ya kipuuzi kabisa mzazi wako nilazima umtunze kadiri uwezavyo haijalishi yeye alikutelekeza wewe timiza wajibu wako kufikiria kurithi ni akili ya kipuuzi na nyinyi vijana acheni kuwahukumu wazazi wa kiume hamjui mama zenu waliwafanyia nini wazee hadi kutelekezwa ngoja muwafume hao wakezenu wakichepuka kama mtaweza kuwavumilia
 
Umeongea pumba tu yaan usomeshwe,ulishwe bado mzee aumize kichwa kukutafutia mali ? Kwa lip...usimpe mtt samaki mfundishe l
 
Hahahaha hii mihogo ina kazi hata dokta slaa aliisingizia kwa ugumu wa maisha
Mbona anatudhalilisha wala mihogo wengine? Kwanza sio kushindia mihogo, ni kula mihogo, kama una matatizo na mwanao deal nayo mwenyewe achana na mihogo yetu. We mzee vipi?
 
Hapa tumepata khabari ya upande mmoja kuijibu hii mada panakuwa hapatoshi hatuwezi jua madhira ambayo kijana kayapitia mpaka kufanya hivyo. Pana madingi pasua kichwa jamani makauzu mabandidu almuhimu tujenge mioyo ya kusamehe na kusahau pana fumbo kubwa hapa.
 
Inatosha mwenye akili huwezi lipiza visasi unapaswa kutimiza wajibu wako bila kuangalia mwingine alikufanyia nini
 
Hao ndio wazazi wapuuzi tu, yeye mzazi ndio anatakiwa atafute mali kwa ajili ya kumuachia mwanae urithi, na sio Omary kumtunza huyo dingi.... Yeye miaka hiyo 64 alikuwa anafanya nini hadi leo ashindie mihogo, si alikuwa anakula bata na vimada? Aache upuuzi wake.
Dah Hii kali! Yaani nitafute mali kwa ajili ya kumuachia mtoto urithi. Minajua mzazi wajibu wake ni kumsomeaha mtoto tu, mali zangu ni kwa maiaha yangu,huyo mtoto atatafuta za kwake.
 
Hao ndio wazazi wapuuzi tu, yeye mzazi ndio anatakiwa atafute mali kwa ajili ya kumuachia mwanae urithi, na sio Omary kumtunza huyo dingi.... Yeye miaka hiyo 64 alikuwa anafanya nini hadi leo ashindie mihogo, si alikuwa anakula bata na vimada? Aache upuuzi wake.
Alikuwa anahangaika kumlea huyo Ommy.
Nisivyokuwa na baba roho imeniuma watoto mnaowaongelea vibaya wazazi wenu kumbukeni mzazi ni Mungu wa pili wadunia Waheshimu wazazi wako upate marefu maisha Duniani. Mzazi ni mzazi hata akiwa fukara .unachowafanyia wazazi wako na watoto wako watakuja kukufanyia hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom