Baba ake Ommy Dimpoz alalamika kutengwa na mwanae

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
264,065
1,075,504
28154424_816559445134419_841271122761613312_n.jpg

Pichani mwenye tshet nyekundu ni baba yake mzazi Ommy Dimpoz ambapo Amesema mwanae huyo amemtelekeza miaka Mingi licha ya Dimpoz kusifika kwa kula bata nchi mbalimbali duniani.

Baba Dimpoz ana miaka 64 na ni dereva wa bajaji huko Tabora. Babaji amenunua mwenyewe. Wanaomjua wamesema anashindia mihogo na kachumbari !! .

Mzee Faraji Nyembo akizungumza na Globalpublishers anasema "Ni kama Wema Sepetu anavyohangaika kutafuta mtoto, siku akimpata hata kama hamsaidii chochote atamshukuru tu Mungu hivyo na mimi huwa ninamshukuru Mungu maana nimeshamleta Omary duniani.

Yeye kama mtoto, ndiye anayetakiwa kujua mzazi wake anahitaji nini, yaani ukimuuliza sasa hivi Dimpoz akupe namba yangu, utaona, atakujibu nini maana ninaamini hana.

Nimekuwa nikimpigia, lakini simu yake unaambiwa inatumika, angekuwa anaona umuhimu si angekuwa na namba maalum kwa ajili ya kuwasiliana na mimi baba yake kama mastaa wengine wanavyofanya kuwa na namba kwa ajili ya mashabiki na nyingine ya watu muhimu,” alisema na kuongeza “Mfano nikifa kama leo ni bora huyo Ommy asinizike au kuja Tabora maana watu watampiga na kwanza atasema ni nani wake amefariki dunia maana hivi niko hai hana ushirikiano,” alisema baba huyo

Chanzo: GlobalP
 
Watoto wa kiume wengi mapenzi yao kwa mama tu...
Hata cwez kumlaum Ommy kwa anachokifanya
Kwasababu watu wengi huamin baba anauwezo wa kujikim mahitaji yake mwenyewe bila kupatiwa Msaada
Hao ndio wazazi wapuuzi tu, yeye mzazi ndio anatakiwa atafute mali kwa ajili ya kumuachia mwanae urithi, na sio Omary kumtunza huyo dingi.... Yeye miaka hiyo 64 alikuwa anafanya nini hadi leo ashindie mihogo, si alikuwa anakula bata na vimada? Aache upuuzi wake.
 
Watoto wa kiume wengi mapenzi yao kwa mama tu...
Hata cwez kumlaum Ommy kwa anachokifanya
Kwasababu watu wengi huamin baba anauwezo wa kujikim mahitaji yake mwenyewe bila kupatiwa Msaada
Kama alimterekeza ni sawa lakini kama hakumterekeza haiwezekani ule bata halafu eti uje na utetezi wa kiboya kama huo eti watu wengi uamini baba anaweza kujikimu mahitaji yake mwenyewe.
Yani uwe na maisha mazuri mzazi wako ana miaka 64 anahangaika na bajaj useme anaweza kujitunza mwenyewe huo ni ujinga wa kiwango cha rami
 
View attachment 702913 Pichani mwenye tshet nyekundu ni baba yake mzazi Ommy Dimpoz ambapo Amesema mwanae huyo amemtelekeza miaka Mingi licha ya Dimpoz kusifika kwa kula bata nchi mbalimbali duniani. Baba Dimpoz Ana miaka 64 na ni dereva wa bajaji huko Tabora. Babaji amenunua mwenyewe. Wanaomjua wamesema anashindia mihogo na kachumbari !! . Mzee Faraji Nyembo akizungumza na Globalpublishers anasema "Ni kama Wema Sepetu anavyohangaika kutafuta mtoto, siku akimpata hata kama hamsaidii chochote atamshukuru tu Mungu hivyo na mimi huwa ninamshukuru Mungu maana nimeshamleta Omary duniani. Yeye kama mtoto, ndiye anayetakiwa kujua mzazi wake anahitaji nini, yaani ukimuuliza sasa hivi Dimpoz akupe namba yangu, utaona, atakujibu nini maana ninaamini hana. Nimekuwa nikimpigia, lakini simu yake unaambiwa inatumika, angekuwa anaona umuhimu si angekuwa na namba maalum kwa ajili ya kuwasiliana na mimi baba yake kama mastaa wengine wanavyofanya kuwa na namba kwa ajili ya mashabiki na nyingine ya watu muhimu,” alisema na kuongeza “Mfano nikifa kama leo ni bora huyo Ommy asinizike au kuja Tabora maana watu watampiga na kwanza atasema ni nani wake amefariki dunia maana hivi niko hai hana ushirikiano,” alisema baba huyo

Source: GlobalP
Achezee ujana wake aje asumbue wengine,abebe msalaba wake.
 
Hii ni shida sasa, kumbuka amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu. Usitegemee mwanao atakuja kukutanza na kukujali hapo uzeeni. Wazee waliojiandaa na maisha ya uzeeni wala hawana shida... wanatunzwa na kulelewa maana walijipanga. We kula ujana wako usijiwekee akiba utegemee utalishwa na wanao! Mzee mwenye pesa zake nyumba yake itajaa watu na atakufa mikononi mwa watu. Jipangeniiiiiii
 
Kama alimterekeza ni sawa lakini kama hakumterekeza haiwezekani ule bata halafu eti uje na utetezi wa kiboya kama huo eti watu wengi uamini baba anaweza kujikimu mahitaji yake mwenyewe.
Yani uwe na maisha mazuri mzazi wako ana miaka 64 anahangaika na bajaj useme anaweza kujitunza mwenyewe huo ni ujinga wa kiwango cha rami
Hapa mimi kidogo huwa nina mtazamo tofauti, naamini kuwa huyo mzazi anatakiwa akomae na hiyo bajaji yake ampatie Ommy Dimpoz pesa, sio pesa tu, atafute mali zaidi ili ikiwezekana Dimpoz aje kurithi... MZAZI MWENYE BUSARA HUACHA URITHI WA MALI KWA WANAWE! LAKINI MPUMBAVU HUTAPANYA MALI KWA POMBE NA UZINZI KISHA HULALAMIKA KUWA WANAWE HAWAMJALI.
 
Duuh! Kama hamjali kweli sio sawa aisee.

Ila upande wa pili wa shilingi je katika makuzi ya huyo Ommy je Baba alishiriki mpaka kufika alikofika au ndio alihangaika na Mama pekee halafu yeye anakuja na malalamiko baada ya kuona amekuwa mtu mzima ikiwemo na umaarufu alionao.
 
Mzazi ni mzazi regardless alikutenda nini. Hata uwe na justification gani ....ukimtelekeza laana itakutafuna tu one day .... kama unabisha hewala lakini uliza waliokula chumvi kidogo wakupe shuhuda ....mzazi kushindwa kukuachia urithi wowote hiyo itabakia adhabu kwake na pengine ndio anapitia adhabu yenyewe kwa namna nyingine lakini wewe hupaswi kumtelekeza kwa makusudi.
 
Kama alimterekeza ni sawa lakini kama hakumterekeza haiwezekani ule bata halafu eti uje na utetezi wa kiboya kama huo eti watu wengi uamini baba anaweza kujikimu mahitaji yake mwenyewe.
Yani uwe na maisha mazuri mzazi wako ana miaka 64 anahangaika na bajaj useme anaweza kujitunza mwenyewe huo ni ujinga wa kiwango cha rami
Maisha yao kwa ujumla hatuyajui, wala hatujui uyo Ommy kalelewaje

Ila kubali kataa Watanzania wengi kwenye kulea wazazi tunamjali sana mama, baba cyo kiivyo
 
Umenena vyema, mzazi anayetambua wajibu wake kamwe huwezi msikie akilalamika kutaka kutunzwa na wanawe, tena atajisikia aibu kwa nini hajaanda mali na urithi kwa wanawe, ukiona mzazi anataka kutunzwa na wanawe wakati lijitu lizima lina nguvu na kitambi linakula tu mihogo fahamu huyo ni mpuuzi na hajachangia hata kwa vyovyote kwenye maisha ya mwanae, mtu kama Dimpoz kapambana mwenyewe from zero, hakuna sapoti ya mzazi wala nini....
Leo lijitu linataka kutunzwa, pumbavu..
Hii ni shida sasa, kumbuka amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu. Usitegemee mwanao atakuja kukutanza na kukujali hapo uzeeni. Wazee waliojiandaa na maisha ya uzeeni wala hawana shida... wanatunzwa na kulelewa maana walijipanga. We kula ujana wako usijiwekee akiba utegemee utalishwa na wanao! Mzee mwenye pesa zake nyumba yake itajaa watu na atakufa mikononi mwa watu. Jipangeniiiiiii
 
Mzazi ni mzazi regardless alikutenda nini. Hata uwe na justification gani ....ukimtelekeza laana itakutafuna tu one day .... kama unabisha hewala lakini uliza waliokula chumvi kidogo wakupe shuhuda ....mzazi kushindwa kukuachia urithi wowote hiyo itabakia adhabu kwake na pengine ndio anapitia adhabu yenyewe kwa namna nyingine lakini wewe hupaswi kumtelekeza kwa makusudi.

Duuh! Kama hamjali kweli sio sawa aisee.

Ila upande wa pili wa shilingi je katika makuzi ya huyo Ommy je Baba alishiriki mpaka kufika alikofika au ndio alihangaika na Mama pekee halafu yeye anakuja na malalamiko baada ya kuona amekuwa mtu mzima ikiwemo na umaarufu alionao.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom