Ommy Dimpoz: Hata nikiacha muziki nitaishi bila shida yoyote, siyo chawa wa GSM Wala Joho, baba yangu alinitelekeza

lord atkin

Senior Member
Sep 30, 2018
197
683
Msanii Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu mambo mbalimbali, kama vile wapi anapata pesa, ukaribu wake na GSM na aliyekuwa Governor wa Mombasa Hassan Joho na kuhusu kutelekezwa na baba yake mzazi.

Akiongea katika kipindi cha Salama Na Ommy Dimpoz amesema yeye Kwa Sasa yupo vizuri kifedha hivyo hata akiacha muziki ataishi bila shida yoyote Ile. Ommy Dimpoz amesema Kwa Sasa yeye ndiye mwenye tenda ya kushughulika na matangazo yote ya GSM kupitia kampuni yake ya marketing aliyoianzisha ambayo imeajiri wataalamu wa kutosha. Kampuni hiyo inajihusisha na online branding zote za GSM, posters nk.

Ommy Dimpoz amewashauri wasanii wengine kuwa na plan B katika maisha Kwa kutumia influence waliyonayo kufanya biashara zingine badala ya kutegemea muziki peke yake. Pia Ommy Dimpoz amesema yeye siyo chawa wa GSM Wala Joho.

Kuhusu ukaribu wake na Joho Ommy Dimpoz amesema Joho amemsaidia sana kipindi alichokuwa akiumwa Kwa kuwa alibeba gharama karibia zote za matibabu ya south Africa na hospital ya Nairobi. Hivyo ukaribu wao umekuwa ni kama ndugu kwani mtu anayekusaidia katika matatizo hasa ya ugonjwa bond inayokuwepo ni kubwa.

Kuhusu GSM, Ommy Dimpoz amesema ukaribu wao ni wa kibiashara zaidi, Ommy Dimpoz amesema alianza kutangaza bidhaa za GSM kama Balozi kuanzia mwaka 2015, na kwamba Kwa Sasa amefungua kampuni yake ya marketing ambayo ndiyo inayohusika na matangazo yote ya GSM.

Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu Mahusiano hafifu kati yake na baba yake na kusema hali hiyo imesababishwa na ukweli kwamba baba yake alimtelekeza akiwa mdogo hivyo Ommy Dimpoz kulelewa na mama yake mdogo pamoja na bibi yake baada ya mama yake kufariki.

Amenukuliwa akisema "Sina kinyongo naye", Ommy Dimpoz anasema kutekeleza huko kumefanya kukosekana bond kati Yao na si kwamba yeye ana mchukia baba yake. Baba yake Ommy Dimpoz na Mama yake hawakuwahi kuoana, hivyo baba yake alikuwa anaishi na mwanamke mwingine na familia yake.

Kuhusu album

Ommy Dimpoz amesema yupo mbioni kuachia album yake ambayo anaiandaa huku executive producer akiwa pfunk majani.

Hili la watoto kutokuwa na bond nzuri na wazazi Tanzania ni kubwa mno ,ila watu hawajui tu.

Wanaume mnavozaa hakikisheni mnaleaa msifikili kuwa baba ni kuzaa tu, bila malezi na kutengeneza ukaribu zaidi na mtoto basi unajiandalia bomu lako mwenyewe na badae hakuna mtoto atakaye kujali, niamini Mimi ......

Kama mtoto amekuwa Hana ukaribu na wewe usifikili akija kukua atakuja kuwa na feelings zozote na wewe et baba yake ,hata kwa uchawi au Nini yaani hapa mtoto anakuwa Hana chembechembe za huruma na wewe kwani toka utotoni ulishindwa kutengeneza hisia zako juu yake hili swala Mimi naliona hata kwenye familia kabisa. Wazazi wanajisahau watoto wanakua hovyo hovyo tu bila kuwa na malezi ya wazazi, wakishakuwa wakubwa automatic wanajikuta hawana hisia zozote na baba, kwani muda mwingi katika ukuaji wametengwa hawajapata ule upendo,ukaribu na umoja ,unafikili akikua atakujali?

Kuhusu ommy kumtelekeza baba yake Mimi hata sishangai kabisa ,na mtaani wapo wengi sana nawaona .
 
Hili la watoto kutokuwa na bond nzuri na wazazi Tanzania ni kubwa mno ,ila watu hawajui tu ....!

Wanaume mnavozaa hakikisheni mnaleaa msifikili kuwa baba ni kuzaa tu ,bila malezi na kutengeneza ukaribu zaidi na mtoto basi unajiandalia bomu lako mwenyewe na badae hakuna mtoto atakaye kujali ,niamini Mimi ......

Kama mtoto amekuwa Hana ukaribu na wewe usifikili akija kukua atakuja kuwa na feelings zozote na wewe et baba yake ,hata kwa uchawi au Nini yaani hapa mtoto anakuwa Hana chembechembe za huruma na wewe kwani toka utotoni ulishindwa kutengeneza hisia zako juu yake ...hili swala Mimi naliona hata kwenye familia kabisa .....wazazi wanajisahau watoto wanakua hovyo hovyo tu bila kuwa na malezi ya wazazi ,wakishakuwa wakubwa automatic wanajikuta hawana hisia zozote na baba ,kwani muda mwingi katika ukuaji wametengwa hawajapata ule upendo,ukaribu na umoja ,unafikili akikua atakujali ? .....

Kuhusu ommy kumtelekeza baba yake Mimi hata sishangai kabisa ,na mtaani wapo wengi sana nawaona ....
Kuna Ile misemo ya kudanganyana eti baba ni baba tu, au mzazi ni mzazi
 
Umeongea point sana
Sema ndio vile kizazi cha nyoka wajuaji sana
 
Omeongea point nzuri Sana mkuu🙏
 
mkuu umeongea mazuri mengi sana lakini nimeshuhudia wanawake wengi wanakataa kuwaonesha watoto baba zao waliowazaa. Wakizaa tu wanawaficha huko kwa bibi zao kimyaa.
 
Hili la watoto kutokuwa na bond nzuri na wazazi Tanzania ni kubwa mno ,ila watu hawajui tu ....!

Wanaume mnavozaa hakikisheni mnaleaa msifikili kuwa baba ni kuzaa tu ,bila malezi na kutengeneza ukaribu zaidi na mtoto basi unajiandalia bomu lako mwenyewe na badae hakuna mtoto atakaye kujali ,niamini Mimi ......

Kama mtoto amekuwa Hana ukaribu na wewe usifikili akija kukua atakuja kuwa na feelings zozote na wewe et baba yake ,hata kwa uchawi au Nini yaani hapa mtoto anakuwa Hana chembechembe za huruma na wewe kwani toka utotoni ulishindwa kutengeneza hisia zako juu yake ...hili swala Mimi naliona hata kwenye familia kabisa .....wazazi wanajisahau watoto wanakua hovyo hovyo tu bila kuwa na malezi ya wazazi ,wakishakuwa wakubwa automatic wanajikuta hawana hisia zozote na baba ,kwani muda mwingi katika ukuaji wametengwa hawajapata ule upendo,ukaribu na umoja ,unafikili akikua atakujali ? .....

Kuhusu ommy kumtelekeza baba yake Mimi hata sishangai kabisa ,na mtaani wapo wengi sana nawaona ....
Wapo pia ambao wanapata malez mazur tu lkn wakishakuwa wanakuwa hawana bond na baba zao..mm nina mifano hai
 
Back
Top Bottom