MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,084
- 43,477
Umeongea la maana sana mkuu. Mimi pia ni mjasiriamali wa size ya kati na nimegundua unachosema na nina ushahidi mzito kuhusu hilo. Mwaka jana tulikuwa tunamtafta dada wa duka letu mwenye elimu kiasi ya uhasibu/marketing na kiukweli mshahara ulikuwa sio mkubwa yaani laki 3. Kwa waliojitokeza wengi ila akatokea mdada aliyekuwa na talent kubwa kwa jinsi alivyojieleza tukamtajia mshahara ila hakukubaliana nasi tukaona tumwongezee laki maana anaonekana ni jembe pia akakataa. Ila kinachosikitisha hadi leo dada hajapata kazi kwa fikra mgando alizo nazo. Wengine wakipata kazi wanaanza kuleta longolongo
Ukilaza unachangiwa na mtu binafsi, jitihada alizonazo na uwezo wa kutumia ujuzi, maarifa na kuchangamkia fursa.. Mtu hana kazi lakini akiambiwa afanye kazi ya mshahara Laki 3 hataki...eti hawezi kufanya kazi ya mshahara mdogo, siku hizi kuna agency za kuajiri changamka sio lazima uende kwenye ofisi zao wapigie simu waulize post zilizopo emails zao zipo tuma particulars zako..niliwahi kutuma application kwa njia ya simu tena nikiwa kitanda after 10 minutes nilipokea simu kesho yake interview na nilipita japo salary ilikuwa laki 4 na degree yangu bado sikukata tamaa nilifanya kwa juhudi..leo nimepata sehemu nzuri zaidi salary 1.8 million na chenchi..napenda niwatie moyo graduate fanyeni hata kama ni salary ndogo savings zako unaweza fanyia ujasiliamali..wakati nipo kwenye ajira ile ya awali i was selling ladies shoes na nguo ilikuwa si haba napata visent..kingine angalia mienendo yako jinsi unavyoishi na jamii ...tatizo mnataka mishahara mikubwaa wakati kila kitu kwa wakati..hii ni kazi yangu ya nne...ila hizo 3 za awali kweli mshahara ulikuwa kidogo sana. Mwisho acheni uvivu na uzembe na kuweni wabunifu...kilimo na ufugaji nowdays kinalipa pia..