Baada ya Tundu Lissu kuwa-expose waanza kujitaja wenyewe...

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Mbuge wa Viti Maalum (CCM), Sarah Msafiri, amekiri kwenda kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanzania), kufuatilia mkataba wa Kampuni ya M/S Sharrifs Services & General Supply inayohusishwa kufanya biashara yenye utata ya matairi na shirika hilo.

Sarah, alisema alifanya hivyo baada ya kuombwa na mwenye kampuni hiyo, Heri Sharrif, amsaidie kufuatilia mkataba wake Tanesco.

Alidai mbele waandishi wa habari bungeni jana kuwa ameshitushwa na taarifa za kuhusishwa na kampuni hiyo, na inadaiwa aliisimamia malipo yenye utata kutoka Tanesco.

Alidai kuwa hana mahusiano yo yote ya kibiashara na kampuni ya Sharrifs na kwamba siyo mmiliki na wala sio mkurugenzi, na hana hisa wala hajaajiriwa kwa kazi yo yote na Sharrifs.

Lakini alisema: “ninachojua kuhusu kampuni ya Sharrifs ni kupitia mkurugenzi wake Heri ambaye mimi kama mbunge alikuja kwangu kunieleza matatizo yake kwamba aliomba zabuni Tanesco kupitia kampuni yake na wakashinda, wakapewa barua na Tanesco kujulishwa wameshinda kisha wakapewa barua ya kwenda kufanya majadiliano pande mbili yaani Tanesco na Sharrifs.”

Alisema baada ya kukamilisha mchakato huo, walipewa mkataba ambao kimsingi unabeba makubaliano ya mazungumzo waliokaa pande zote mbili.

“Kama mbunge ambaye nina wajibu wa kushughulikia kero za wananchi nilienda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco na kumweleza madai hayo ya Sharrifs, nakumbuka alimwita Mkuu wa Idara ya Manunuzi ambaye alikiri kuifahamu Sharrifs na mkataba wake na mkataba wake alishaushughulikia na kuupeleka kwa mwanasheria wa shirika,” alisema.

Alisema mwanasheria alipoitwa alikwenda na mkataba huo ukiwa umefungwa kwenye bahasha ya kaki na hapo ndipo mkurugenzi mkuu alipomhoji kwanini anakaa na nyaraka ambazo anatakiwa kuziwasilisha sehemu husika.

“Tukiwa wote nilimpigia simu Heri na kumweleza kuwa nipo Tanesco na mkataba wake uko tayari kwa mwanasheria hivyo aje kuuchukua, lakini Heri alinijibu yeye yuko mbali ila kama kuna uwezekano nimchukulie ataupitia nyumbani kwani ni jirani yangu maeneo ninapoishi,” alidai.

Hata hivyo, alidai hakuwa na haja ya kujua walichokubaliana kwenye mkataba kwani kwanza hayamhusu.

Alidai kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake ni mkakati uliowekwa wa kummaliza kisiasa na kuchafua jina lake, mkakati ambao alisema umefanikiwa kwa kiasi fulani.

Aliyataka magazeti yaliyoripoti habari hizo bila kumpa nafasi ya kumsikiliza yamwombe radhi haraka iwezekanavyo na kama yakishindwa basi atayafikisha mahakamani.

Kuibuka kwa Sarah ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyovunjwa na Spika Anne Makinda kumekuja baada ya Kikao cha Bunge la Bajeti 2012/13 kuibua tuhuma mbalimbali zikiwemo za baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo kutuhumiwa kuomba rushwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Tuhuma zingine kwao ni kuwepo kwa makampuni ya mafuta kuhonga wabunge wasipitishe Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni.

Katika kikao hicho, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, wabunge hao walipaswa kutaja maslahi yao kibiashara kwenye shirika hilo.

“Sasa wabunge hawa hawajawahi kufanya hivyo na wameendelea kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na wengine kufanya biashara na Tanesco,” alisema Lissu na kuwataja kuwa ni Munde Tambwe, Sarah Msafiri, Mariam Kisangi wa Viti Maalum, Yusuf Nassir (Korogwe Mjini) na Charles Mwijage Muleba Kaskazini.

Lissu alifafanua kuwa Tambwe na Msafiri wana zabuni ya kuiuzia Tanesco magurudumu na kwamba hawajawahi kutangaza maslahi yao katika jambo hilo kwenye kamati zao.

“Mwijage ni mtaalam mwelekezi wa Kampuni ya Puma Energy iliyopewa tenda na Maswi kuiuzia mafuta Tanesco, hivyo kama mjumbe wa Kamati ya Nishati ana mgongano wa kimaslahi. Nassir na Kisangi hawa wanafanya biashara ya mafuta wanamiliki vituo vya mafuta na wana mgongano,” alisema.

Kuhusu Christopher ole Sendeka, Lissu alidai amekuwa akizipigia debe kampuni tatu zilizonyimwa zabuni ya kuiuzia mafuta Tanesco akiwashawishi wajumbe wa kamati kuwa serikali ilikiuka kanuni kuipa tenda Kampuni ya Puma Energy.

Mwingine aliyetajwa ni Vicky Kamata wa Viti Maalum (CCM) ambaye alidaiwa kuwa na mgongano wa kimaslahi na Maswi.

Baada ya kamati hiyo kuvunjwa, Spika Makinda aliunda Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma hizo.

Julai 28 mwaka huu, Spika Makinda alivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kutokana na baadhi ya wajumbe wake kutuhumiwa kuhongwa na kampuni za mafuta nchini.

Kamati hiyo iliyovunjwa ilikuwa ikiundwa na wajumbe zaidi ya 20 ambao ni pamoja na Mwenyekiti wake, Selemani Zedi na Makamu mwenyekiti, Diana Chilolo, Profesa Kulikoyela Kahigi, Yusufu Haji Khamisi, Mariam Kisangi, Catherine Magige, Dk. Anthony Mbassa, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yusufu Nassir, Christopher Ole Sendeka na Dk. Festus Limbu.

Wengine ni Shafin Sumar, Lucy Mayenga, Josephine Chagulla, Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Masoud, Kisyeri Werema Chambiri, Munde Abdallah, Sara Msafiri, Vicky Kamata na Ali Mbaruk Salim.

Kuvunjwa kwa kamati hiyo kulifuatia Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa, kuomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hilo lijadiliwe na Bunge na kupendekeza kuwa Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe.

Bunge likubali kuivunja na kuiunda upya Kamati ya Nishati na Madini na kamati na baada ya hoja hiyo kuungwa mkono, Spika Makinda alisimama na kukubali hoja hiyo ya Kawawa na kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini.

Spika Makinda alisema ameiagiza Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi.

Baadaye Spika aliunda kamati ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ambayo Mwenyekiti wake ni Ngwilizi. Wajumbe wengine ni John Chiligati (Manyoni-CCM); Gosbert Blandes (Karagwe-CCM); Riziki Omary (Viti Maalum-CUF) na Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema).

Kitendo cha Sarah kuzungumza hadharani na kujitetea kimatafsiriwa kuwa ni kukiuka agizo la Bunge kwamba suala hilo lisijadiliwe na mtu au chombo chochote.

Wiki iliyopita Naibu Spika, Job Ndugai, alisema ripoti Ngwilizi itawasilishwa bungeni iwapo Spika ataridhika taarifa hiyo kutolewa ndani ya Bunge.

Alisema baada ya kukamlika kwa kazi hiyo, baadhi ya wananchi na wanasiasa wameanza kuizungumzia pamoja na vyombo vya habari kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo kinyume cha sheria na kuingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge.

Alisema sheria hiyo inamkataza mtu yoyote kuchambua na kuchapisha taarifa ya kamati kabla ya kuwasilisha bungeni.

“Natoa rai kwa umma kuwa tuache Bunge lifanye kazi yake kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni,” alisema Ndugai.

Ngwilizi naye aliwahi kusema kuzuia kujadili suala hilo hadi ripoti itakapowasilishwa bungeni.
Hadi jana wabunge hawakuelezwa chochote kama ripoti hiyo itawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano uanoendelea.

Hata hivyo, habari ambazo NIPASHE ilizipata, zinaeleza kuwa msimamo bado uko pale pale kwamba suala hilo litaamuliwa na Spika.

Kumekuwepo na taarifa kuwa huenda ripoti hiyo isijadiliwe bungeni kwa ajili ya kulinda heshima ya serikali.

Habari zinadai kuwa uamuzi huo unatokana na kuwepo kwa makundi mawili yanayokinzana. Kundi moja linalotaka ijadiliwe linataka ukweli wa tuhuma hizo ujulikane na haki itendeke kwa waliotuhumiwa.

Kundi linalotaka isijadiliwe ni lile linaloiunga mkono serikali ambalo linaona kuwa kujadiliwa kwake kunaweza kuwatia hatiani viongozi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini, Waziri Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi.

Vigogo hao wanadaiwa kuipatia Puma zabuni ya kuiizia serikali mafuta mazito ya muendesha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kwa upendeleo na kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.



CHANZO: NIPASHE

MY TAKE:
Mbunge kabla ya kutoa statement hi ilibidi aende akasome vizuri sheria ya maadili ya viongozi ya mwaka 1995 angeona kosa lake liko wapi.

 
Yaani ningekuwa mie ndio mshauri wake huyo Sarah.. nicingemshauri kuita waandishi wa habari na kutoa "a cooked story" kama ile ambayo mwisho wa ciku ataiamini yeye tu.. Watanzania wengi wanauelewa ukweli sasa..
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Mbona kajikanyaga sana huyo mama.yaani hapo kaweka mambo hadharani.

hapo ndio ujuwe kuwa amekamatwa wewe ukiwa kama mjumbe wa kamati ya nishati na madini ambayo ni kama unasimamia maslahi ya serikali halafu wakati huo huo ukiwakilisha maslahi ya kampuni binafsi(conflict of interest) ni kosa kisheria
kisheria angetakiwa ayaeleze hayo kwanza kwa spika ambapo spika asingemteua kuwa ktk kamati hiyo kwa kuofia mgogano wa maslahi
 
politiki Hivi hajaachia ngazi tu ya huo ubunge viti maalum. Au ni maalum kwa rushwa? Aibu zake mfa maji haachi kutapatapa. shame on her na hao wanaopanga hizo kamati niulize walikuwa hawafahamu kuwa hawa wajumbe wengi wanabiashara zao ambazo zitakiuka maadili? Ripoti iwekwe wazi watakaombuka waumbuke. Ndio tatizo la hii sirikali kulindana tumechoma sie.
 
Last edited by a moderator:
Aibu zao wataeleza yote bila kuulizwa. minitu mingine inatia aibu hao wajumbe waacjie ubunge wote.
 
Wabunge watokanao na upendeleo au viti vya chup... hawana wa kuwakilisha zaidi ya matumbo yao. Tumepiga kelele tuondoe hivi viti lakini wakubwa hawataki kwa vile wanaweka watu wao hasa vimada na mambo mengine. Sasa mnaona? Kwenye kutoa maoni ya katiba tuazimie kupiga marufuku viti hivi vya aibu.
 
Jamani mnalaumu bure tu, hakujua kama ni kosa, wabunge wa Chama Cha Mapenzi(CCM) ni vilaza sana aisee
 
Sarah, unadhalau ya hatari, huo utetezi usio na kichwa wala miguu kawaambie familia yako
 
Mgongano wa masilahi ya vick kamata sababu ni nyama na ana watoto wa mkulu. Na mkulu pamoja na mwanae wanamiliki kampun ya mafuta so nadhan wamemweke na Vick ili kulinda maslahi ya watoto wadogo wa mkulu ambao anao Vick
 
Mgongano wa masilahi ya vick kamata sababu ni nyama na ana watoto wa mkulu. Na mkulu pamoja na mwanae wanamiliki kampun ya mafuta so nadhan wamemweke na Vick ili kulinda maslahi ya watoto wadogo wa mkulu ambao anao Vick
He makubwa watoto wa Mkulu wapo kwa Vick ameaadopt au anamsaidia kulea !
Vick si ndio aliimba ule wimbo wa MFALME SULEIMAN !Kwa hiyo mfalme analelewa watoto sio!
 
Hahahahaha...kweli mfa maji...yaani utetezi wa kitoto sanaa, pole mbuge kilaza...walau ungekaa kimya
 
Wabunge watokanao na upendeleo au viti vya chup... hawana wa kuwakilisha zaidi ya matumbo yao. Tumepiga kelele tuondoe hivi viti lakini wakubwa hawataki kwa vile wanaweka watu wao hasa vimada na mambo mengine. Sasa mnaona? Kwenye kutoa maoni ya katiba tuazimie kupiga marufuku viti hivi vya aibu.

dah mkuu naona umetokelezea na hoja nzitonzito! hapo nilipo bold hapo nafikiri hapajakaa vizuri, hata kama unapinga nafikiri ni busara kupinga kwa hoja zenye mashiko kuliko kashfa. nina mashaka na thinking yako katika jukwaa hili. ni mtazamo tu lakini, tusijenge chuki mkuu
 
Back
Top Bottom