Baada ya Tundu Lissu kuwa-expose waanza kujitaja wenyewe...

Hahahahaha...kweli mfa maji...yaani utetezi wa kitoto sanaa, pole mbuge kilaza...walau ungekaa kimya


Tulishapiga keleleeeeeee........!!!!! Viti maalum VIFUTWEEEEEE..... hakuna umaalum wake... They are vilaza, jobless na wanalipwa mishahara minono kama kiti moto, SASA VITI MAALUM KUONA HAWANA KAZI WASHAANZA RUSHWA ZA WAZI KAMA HIZI....

HUYU MBUNGE WAZI WAZI NI RUSHWA KAPEWA NOW ANAJIDEFEND WITH OOOOOOO.....!!! points... kala achunguzwe na hivi viti vifutwe..... hawana kazi....mbaya zaidi wameanza kupokea RUSHWA....
 
Hawa magamba wanachofanya ni kujaribu kusafisha uchafu wao hadharani. Hivyo wanajiongezea aibu zaidi

Kwa upande mwingine Mh. Lissu anasema hivi; Serikali ya CCM ni mtuhumiwa namba wani wa rushwa na ufisadi. Taasisi zake ( hapa TANESCO) ni watuhumiwa namba mbili. Wabunge wa CCM (maana kwa ndio sehemu kubwa ya Bunge na kihistoria ni rubber stamp) ni watuhumiwa namba tatu. Wote ni watuhumiwa na kesi ikiamuliwa kwa haki wote wana makosa/hatia.

Dawa ni moja tu, kuwaondoa CCM madarakani.
 


Kundi linalotaka isijadiliwe ni lile linaloiunga mkono serikali ambalo linaona kuwa kujadiliwa kwake kunaweza kuwatia hatiani viongozi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini, Waziri Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi.


Nipashe! Deliberate Distortion. The opposite is true. Apparently a syndicate has paid for direction of the story.​
 
Kwa akili ya kawaida tu haoni yeye kama mjumbe wa kamati ya Nishati na Madini kwenda kwa Mkurugenzi wa Tanesco kuulizia Mkataba kama uko tayari au vp? Anaweza kuchangia MAAMUZI? Kama MBUNGE halielewi hilo basi kuna matatizo ya KIMAADILI
 
Kwa huo utetezi ashukuru kwa kuzaliwa Tanzania, ingekua amezaliwa nchi zingine kama China angesubiria kitanzi!
 
huyu dada kwa maelezo yake anahusika tena kwa nafasi kubwa !!! ningeshauri apime upepo mwenyewe!!!!
 
Yeye anajiona kaongea point kumbe anajivua nguo pasipo kujijua
 
Utetezi wa kipuuzi kabisa, eti alikuwa anafuatilia kero za wananchi kama mbunge, hakuona matatizo ya maji, barabara, pembejeo, huduma za afya nk aliona kero kubwa ya wanachi ni kwenda kufuatilia mkataba Tanesco, na mimi naomba anisaidie kufuatilia uhamisho wa mwanangu kutoka kantalamba basi
 
Mwanangu Bhikola you don't know what you are saying. Hivyo nakuacha na blanketi lako na mapenzi ya kibubusa. Nimejibu hoja yako kulingana na uzito wake usiokuwepo. Hoja mbovu hujibiwa na majibu mabovu. Nadhani utafaidika sasa.
 

Alidai mbele waandishi wa habari bungeni jana kuwa ameshitushwa na taarifa za kuhusishwa na kampuni hiyo, na inadaiwa aliisimamia malipo yenye utata kutoka Tanesco.
“Tukiwa wote nilimpigia simu Heri na kumweleza kuwa nipo Tanesco na mkataba wake uko tayari kwa mwanasheria hivyo aje kuuchukua, lakini Heri alinijibu yeye yuko mbali ila kama kuna uwezekano nimchukulie ataupitia nyumbani kwani ni jirani yangu maeneo ninapoishi,” alidai.

[SUP]Hapo kwa akili ya kawaida ndio umeona utetezi!?
Mkataba unachukuliwa unaupeleka nyumbani? sio ofisini? na huyo mfanyabiashara hana ofisi? hana wafanyakazi?
Kwa hili hauna jinsi mama una share na huyo mfanyabiashara huu sio utetezi! labda uje ukane wamekunuu vibaya waandishi.[/SUP]

 
He makubwa watoto wa Mkulu wapo kwa Vick ameaadopt au anamsaidia kulea !
Vick si ndio aliimba ule wimbo wa MFALME SULEIMAN !Kwa hiyo mfalme analelewa watoto sio!
vick kamata aliimba kuwa mkulu ni mfalme suleman si unajua wafalme wanavyopenda wanawake wazuri. mali, kila kitu chao sasa vick anatoka na mkulu si unajua matokeo ya kutoka usiku si watoto na hivyo ni mzazi mwenza
ke
 
Dada Sarah, mwogope Mungu, na uwaheshimu wananchi unaowatumikia waliokupa dhamana!

Pamoja na kuchemka hata katika hiyo 'story', bado inazidi kuprove kwa Sarah na akina Zitto kuwa Mhando alikuwa kiongozi mbovu maana swali ni kuwa, "Inakuaje Kampuni ishinde tenda na isitaarifiwe kwa muda mrefu na Mkurugenzi Mtendaji awe hana taarifa mpaka kufikia mteja aje kulalamikiwa na Mbunge! Yaani mnatufanya sote majuha? Kama Mhando angekuwa mchapa kazi kwa nini asiwe approachable or accessible easily na hawa ma-suppliers mpaka wafikie kuona kuwa hawana msaada kwake hadi kwenda kulalamika kwa Wabunge?


Hayo yote ni dibaji tu ku disqualify hiyo story ya kitoto ya Mbunge kufikia kujipendekeza kumbebea mkataba mteja anayeomba kusupply mali za mamilioni kama vile uongozi wa kampuni yake ungeshindwa kufika ofisi kuufuata na kupewa maagizo ya kiofisi yanayoendana na mkata huo.

Sarah kinachokusibu ni lile fuko la fedha ulilokuwa unatembeza ili kumtetea Eng. Mhando (alitekuwa wakala wa mafisadi TANESCO) na pia kututaka kupinga bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bila sababu yeyote ya msingi. Pili kumbuka kuwa deals zako zote za kibiashara ulizokuwa unafanya TANESCO sio siku moja tu watu wanazifahamu.

Kumbukumbu zote za kumtembelea Mhando na mawasiliano yenu tunayajua na watumishi wengi sana TANESCO wanakufahamu. Hata yule dada aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Mhando alishafikiwa na alitoa maelezo mazuri mengi ya kukumaliza kabisa ukiachilia mbali wasaidizi wa Mhando waliokuwa masoko na Wabunge wa kike uliwafuata na mazungumzo yako nao n.k. Fanyeni tu madudu yenu lakini msisahahu kuwa waaminifu katika umma na katika vyombo vya usalama wapo na hawatawavumilia hata chembe!

Aliyekushauri kwenda kwenye magazeti (staili ya rafiki yako Zitto) ndiye amekumaliza kabisa maana sasa hata kabla ya yote inatakiwa Spika wa Bunge akusogeze kwenye kamati ya Maadili kukujadili na kukupa adhabu unayostahili si kwa ajili ya sakata linalokuhusu juu ya rushwa na migongano ya kimaslahi bali la kudharau agizo la Spika kupitia kwa Naibu wake KUTOZUNGUMZA TAARIFA HIYO KABLA HAIJAPOKELEWA NA SPIKA. UMEONYESHA DHARAU KUBWA SANA KATIKA MAMLAKA YA BUNGE!:A S angry:

Tundu Lissu, Maswi, Muhongo, Simbachamwene na wengine wote waliopiga kelele juu ya hili sakata linalowahusu akina Sarah na Mhando wote walikuwa sahihi sana.

Baada ya Mhando, wewe Sarah unatakiwa uvuliwe uwanachama kutoka Chama chako ili iwe fundisho kwa Wabunge wanaokiuka maadili ya dhamana walizopewa. Kisha Maj. Gen. Mboma ondolewe haraka sana asiwe mwenyekiti wa Bodi hiyo maana naye ndiye mwenye biashara chafu na TANESCO na wala hana any added advantage katika kuiongoza Bodi kuelekea ufanisi kuliko watanzania maelfu wenye sifa zao tu na wanaoweza kuisimamia Bodi hiyo vyema zaidi kwa manufaa ya Watanzania.
 
Utetezi wake wa kitoto na ametishia kwenda mahakamani lakini kiukweli hawezi kwenda kwani watambana kisheria na ataumbuka haiingii akilini mfanyabiashara anayefanya biashara kubwa kushindwa kuchukua mkataba wake pia nilitegea angezungumzia kitendo cha kulipwa pesa mara ya thamani ya kazi waliyopewa
 
Mbuge wa Viti Maalum (CCM), Sarah Msafiri, amekiri kwenda kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanzania), kufuatilia mkataba wa Kampuni ya M/S Sharrifs Services & General Supply inayohusishwa kufanya biashara yenye utata ya matairi na shirika hilo.

Sarah, alisema alifanya hivyo baada ya kuombwa na mwenye kampuni hiyo, Heri Sharrif, amsaidie kufuatilia mkataba wake Tanesco.

Alidai mbele waandishi wa habari bungeni jana kuwa ameshitushwa na taarifa za kuhusishwa na kampuni hiyo, na inadaiwa aliisimamia malipo yenye utata kutoka Tanesco.

Alidai kuwa hana mahusiano yo yote ya kibiashara na kampuni ya Sharrifs na kwamba siyo mmiliki na wala sio mkurugenzi, na hana hisa wala hajaajiriwa kwa kazi yo yote na Sharrifs.

Lakini alisema: “ninachojua kuhusu kampuni ya Sharrifs ni kupitia mkurugenzi wake Heri ambaye mimi kama mbunge alikuja kwangu kunieleza matatizo yake kwamba aliomba zabuni Tanesco kupitia kampuni yake na wakashinda, wakapewa barua na Tanesco kujulishwa wameshinda kisha wakapewa barua ya kwenda kufanya majadiliano pande mbili yaani Tanesco na Sharrifs.”

Alisema baada ya kukamilisha mchakato huo, walipewa mkataba ambao kimsingi unabeba makubaliano ya mazungumzo waliokaa pande zote mbili.

“Kama mbunge ambaye nina wajibu wa kushughulikia kero za wananchi nilienda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco na kumweleza madai hayo ya Sharrifs, nakumbuka alimwita Mkuu wa Idara ya Manunuzi ambaye alikiri kuifahamu Sharrifs na mkataba wake na mkataba wake alishaushughulikia na kuupeleka kwa mwanasheria wa shirika,” alisema.

Alisema mwanasheria alipoitwa alikwenda na mkataba huo ukiwa umefungwa kwenye bahasha ya kaki na hapo ndipo mkurugenzi mkuu alipomhoji kwanini anakaa na nyaraka ambazo anatakiwa kuziwasilisha sehemu husika.

“Tukiwa wote nilimpigia simu Heri na kumweleza kuwa nipo Tanesco na mkataba wake uko tayari kwa mwanasheria hivyo aje kuuchukua, lakini Heri alinijibu yeye yuko mbali ila kama kuna uwezekano nimchukulie ataupitia nyumbani kwani ni jirani yangu maeneo ninapoishi,” alidai.

Hata hivyo, alidai hakuwa na haja ya kujua walichokubaliana kwenye mkataba kwani kwanza hayamhusu.

Alidai kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake ni mkakati uliowekwa wa kummaliza kisiasa na kuchafua jina lake, mkakati ambao alisema umefanikiwa kwa kiasi fulani.

Aliyataka magazeti yaliyoripoti habari hizo bila kumpa nafasi ya kumsikiliza yamwombe radhi haraka iwezekanavyo na kama yakishindwa basi atayafikisha mahakamani.

Kuibuka kwa Sarah ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyovunjwa na Spika Anne Makinda kumekuja baada ya Kikao cha Bunge la Bajeti 2012/13 kuibua tuhuma mbalimbali zikiwemo za baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo kutuhumiwa kuomba rushwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Tuhuma zingine kwao ni kuwepo kwa makampuni ya mafuta kuhonga wabunge wasipitishe Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni.

Katika kikao hicho, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, wabunge hao walipaswa kutaja maslahi yao kibiashara kwenye shirika hilo.

“Sasa wabunge hawa hawajawahi kufanya hivyo na wameendelea kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na wengine kufanya biashara na Tanesco,” alisema Lissu na kuwataja kuwa ni Munde Tambwe, Sarah Msafiri, Mariam Kisangi wa Viti Maalum, Yusuf Nassir (Korogwe Mjini) na Charles Mwijage Muleba Kaskazini.

Lissu alifafanua kuwa Tambwe na Msafiri wana zabuni ya kuiuzia Tanesco magurudumu na kwamba hawajawahi kutangaza maslahi yao katika jambo hilo kwenye kamati zao.

“Mwijage ni mtaalam mwelekezi wa Kampuni ya Puma Energy iliyopewa tenda na Maswi kuiuzia mafuta Tanesco, hivyo kama mjumbe wa Kamati ya Nishati ana mgongano wa kimaslahi. Nassir na Kisangi hawa wanafanya biashara ya mafuta wanamiliki vituo vya mafuta na wana mgongano,” alisema.

Kuhusu Christopher ole Sendeka, Lissu alidai amekuwa akizipigia debe kampuni tatu zilizonyimwa zabuni ya kuiuzia mafuta Tanesco akiwashawishi wajumbe wa kamati kuwa serikali ilikiuka kanuni kuipa tenda Kampuni ya Puma Energy.

Mwingine aliyetajwa ni Vicky Kamata wa Viti Maalum (CCM) ambaye alidaiwa kuwa na mgongano wa kimaslahi na Maswi.

Baada ya kamati hiyo kuvunjwa, Spika Makinda aliunda Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma hizo.

Julai 28 mwaka huu, Spika Makinda alivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kutokana na baadhi ya wajumbe wake kutuhumiwa kuhongwa na kampuni za mafuta nchini.

Kamati hiyo iliyovunjwa ilikuwa ikiundwa na wajumbe zaidi ya 20 ambao ni pamoja na Mwenyekiti wake, Selemani Zedi na Makamu mwenyekiti, Diana Chilolo, Profesa Kulikoyela Kahigi, Yusufu Haji Khamisi, Mariam Kisangi, Catherine Magige, Dk. Anthony Mbassa, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yusufu Nassir, Christopher Ole Sendeka na Dk. Festus Limbu.

Wengine ni Shafin Sumar, Lucy Mayenga, Josephine Chagulla, Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Masoud, Kisyeri Werema Chambiri, Munde Abdallah, Sara Msafiri, Vicky Kamata na Ali Mbaruk Salim.

Kuvunjwa kwa kamati hiyo kulifuatia Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa, kuomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hilo lijadiliwe na Bunge na kupendekeza kuwa Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe.

Bunge likubali kuivunja na kuiunda upya Kamati ya Nishati na Madini na kamati na baada ya hoja hiyo kuungwa mkono, Spika Makinda alisimama na kukubali hoja hiyo ya Kawawa na kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini.

Spika Makinda alisema ameiagiza Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi.

Baadaye Spika aliunda kamati ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ambayo Mwenyekiti wake ni Ngwilizi. Wajumbe wengine ni John Chiligati (Manyoni-CCM); Gosbert Blandes (Karagwe-CCM); Riziki Omary (Viti Maalum-CUF) na Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema).

Kitendo cha Sarah kuzungumza hadharani na kujitetea kimatafsiriwa kuwa ni kukiuka agizo la Bunge kwamba suala hilo lisijadiliwe na mtu au chombo chochote.

Wiki iliyopita Naibu Spika, Job Ndugai, alisema ripoti Ngwilizi itawasilishwa bungeni iwapo Spika ataridhika taarifa hiyo kutolewa ndani ya Bunge.

Alisema baada ya kukamlika kwa kazi hiyo, baadhi ya wananchi na wanasiasa wameanza kuizungumzia pamoja na vyombo vya habari kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo kinyume cha sheria na kuingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge.

Alisema sheria hiyo inamkataza mtu yoyote kuchambua na kuchapisha taarifa ya kamati kabla ya kuwasilisha bungeni.

“Natoa rai kwa umma kuwa tuache Bunge lifanye kazi yake kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni,” alisema Ndugai.

Ngwilizi naye aliwahi kusema kuzuia kujadili suala hilo hadi ripoti itakapowasilishwa bungeni.
Hadi jana wabunge hawakuelezwa chochote kama ripoti hiyo itawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano uanoendelea.

Hata hivyo, habari ambazo NIPASHE ilizipata, zinaeleza kuwa msimamo bado uko pale pale kwamba suala hilo litaamuliwa na Spika.

Kumekuwepo na taarifa kuwa huenda ripoti hiyo isijadiliwe bungeni kwa ajili ya kulinda heshima ya serikali.

Habari zinadai kuwa uamuzi huo unatokana na kuwepo kwa makundi mawili yanayokinzana. Kundi moja linalotaka ijadiliwe linataka ukweli wa tuhuma hizo ujulikane na haki itendeke kwa waliotuhumiwa.

Kundi linalotaka isijadiliwe ni lile linaloiunga mkono serikali ambalo linaona kuwa kujadiliwa kwake kunaweza kuwatia hatiani viongozi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini, Waziri Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi.

Vigogo hao wanadaiwa kuipatia Puma zabuni ya kuiizia serikali mafuta mazito ya muendesha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kwa upendeleo na kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.



CHANZO: NIPASHE

MY TAKE:
Mbunge kabla ya kutoa statement hi ilibidi aende akasome vizuri sheria ya maadili ya viongozi ya mwaka 1995 angeona kosa lake liko wapi.


Amedanganya umma. Mwanzoni alisema hakuhusika kabisa na akatishia kumfungulia Lissu mashitaka, leo hii anasema alitumwa. Hawa ndo CCM bana. Na bado wananchi wanawapa kura ili wanendelee na madudu yao.
 
aache kujitetea huyo maza....kuna viongozi wengi sana walikua na madili na tanesco ndio maana walikua wanalindana wakati waziri wa nishati alipotaka kuwaumbua...kwanza mkataba mke wa mhando aliokua nao na tanesco vp bado upo au ushasitishwa?
 
Back
Top Bottom