Baada ya Tundu Lissu kuwa-expose waanza kujitaja wenyewe...

Huyu Sara Msafiri kweli anatumie miguu badala ya kichwa yaani hapa kama ni kujifunga ndo kajimaliza mwenyewe,hapa moja kwa moja kuna issue na akibanwa Itafahamika tu,hapa kunaa kitu si bure huyu Mbunge ati wa viti maaluum!!!
 
Mbuge wa Viti Maalum (CCM), Sarah Msafiri, amekiri kwenda kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanzania), kufuatilia mkataba wa Kampuni ya M/S Sharrifs Services & General Supply inayohusishwa kufanya biashara yenye utata ya matairi na shirika hilo.

Sarah, alisema alifanya hivyo baada ya kuombwa na mwenye kampuni hiyo, Heri Sha



rrif amsaidie kufuatilia mkataba wake Tanesco.

Alidai mbele waandishi wa habari bungeni jana kuwa ameshitushwa na taarifa za kuhusishwa na kampuni hiyo, na inadaiwa aliisimamia malipo yenye utata kutoka Tanesco.

Alidai kuwa hana mahusiano yo yote ya kibiashara na kampuni ya Sharrifs na kwamba siyo mmiliki na wala sio mkurugenzi, na hana hisa wala hajaajiriwa kwa kazi yo yote na Sharrifs.

Lakini alisema: “ninachojua kuhusu kampuni ya Sharrifs ni kupitia mkurugenzi wake Heri ambaye mimi kama mbunge alikuja kwangu kunieleza matatizo yake kwamba aliomba zabuni Tanesco kupitia kampuni yake na wakashinda, wakapewa barua na Tanesco kujulishwa wameshinda kisha wakapewa barua ya kwenda kufanya majadiliano pande mbili yaani Tanesco na Sharrifs.”

Alisema baada ya kukamilisha mchakato huo, walipewa mkataba ambao kimsingi unabeba makubaliano ya mazungumzo waliokaa pande zote mbili.

“Kama mbunge ambaye nina wajibu wa kushughulikia kero za wananchi nilienda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco na kumweleza madai hayo ya Sharrifs, nakumbuka alimwita Mkuu wa Idara ya Manunuzi ambaye alikiri kuifahamu Sharrifs na mkataba wake na mkataba wake alishaushughulikia na kuupeleka kwa mwanasheria wa shirika,” alisema.

Alisema mwanasheria alipoitwa alikwenda na mkataba huo ukiwa umefungwa kwenye bahasha ya kaki na hapo ndipo mkurugenzi mkuu alipomhoji kwanini anakaa na nyaraka ambazo anatakiwa kuziwasilisha sehemu husika.

“Tukiwa wote nilimpigia simu Heri na kumweleza kuwa nipo Tanesco na mkataba wake uko tayari kwa mwanasheria hivyo aje kuuchukua, lakini Heri alinijibu yeye yuko mbali ila kama kuna uwezekano nimchukulie ataupitia nyumbani kwani ni jirani yangu maeneo ninapoishi,” alidai.

Hata hivyo, alidai hakuwa na haja ya kujua walichokubaliana kwenye mkataba kwani kwanza hayamhusu.

Alidai kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake ni mkakati uliowekwa wa kummaliza kisiasa na kuchafua jina lake, mkakati ambao alisema umefanikiwa kwa kiasi fulani.

Aliyataka magazeti yaliyoripoti habari hizo bila kumpa nafasi ya kumsikiliza yamwombe radhi haraka iwezekanavyo na kama yakishindwa basi atayafikisha mahakamani.

Kuibuka kwa Sarah ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyovunjwa na Spika Anne Makinda kumekuja baada ya Kikao cha Bunge la Bajeti 2012/13 kuibua tuhuma mbalimbali zikiwemo za baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo kutuhumiwa kuomba rushwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Tuhuma zingine kwao ni kuwepo kwa makampuni ya mafuta kuhonga wabunge wasipitishe Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni.

Katika kikao hicho, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, wabunge hao walipaswa kutaja maslahi yao kibiashara kwenye shirika hilo.

“Sasa wabunge hawa hawajawahi kufanya hivyo na wameendelea kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na wengine kufanya biashara na Tanesco,” alisema Lissu na kuwataja kuwa ni Munde Tambwe, Sarah Msafiri, Mariam Kisangi wa Viti Maalum, Yusuf Nassir (Korogwe Mjini) na Charles Mwijage Muleba Kaskazini.

Lissu alifafanua kuwa Tambwe na Msafiri wana zabuni ya kuiuzia Tanesco magurudumu na kwamba hawajawahi kutangaza maslahi yao katika jambo hilo kwenye kamati zao.

“Mwijage ni mtaalam mwelekezi wa Kampuni ya Puma Energy iliyopewa tenda na Maswi kuiuzia mafuta Tanesco, hivyo kama mjumbe wa Kamati ya Nishati ana mgongano wa kimaslahi. Nassir na Kisangi hawa wanafanya biashara ya mafuta wanamiliki vituo vya mafuta na wana mgongano,” alisema.

Kuhusu Christopher ole Sendeka, Lissu alidai amekuwa akizipigia debe kampuni tatu zilizonyimwa zabuni ya kuiuzia mafuta Tanesco akiwashawishi wajumbe wa kamati kuwa serikali ilikiuka kanuni kuipa tenda Kampuni ya Puma Energy.

Mwingine aliyetajwa ni Vicky Kamata wa Viti Maalum (CCM) ambaye alidaiwa kuwa na mgongano wa kimaslahi na Maswi.

Baada ya kamati hiyo kuvunjwa, Spika Makinda aliunda Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma hizo.

Julai 28 mwaka huu, Spika Makinda alivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kutokana na baadhi ya wajumbe wake kutuhumiwa kuhongwa na kampuni za mafuta nchini.

Kamati hiyo iliyovunjwa ilikuwa ikiundwa na wajumbe zaidi ya 20 ambao ni pamoja na Mwenyekiti wake, Selemani Zedi na Makamu mwenyekiti, Diana Chilolo, Profesa Kulikoyela Kahigi, Yusufu Haji Khamisi, Mariam Kisangi, Catherine Magige, Dk. Anthony Mbassa, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yusufu Nassir, Christopher Ole Sendeka na Dk. Festus Limbu.

Wengine ni Shafin Sumar, Lucy Mayenga, Josephine Chagulla, Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Masoud, Kisyeri Werema Chambiri, Munde Abdallah, Sara Msafiri, Vicky Kamata na Ali Mbaruk Salim.

Kuvunjwa kwa kamati hiyo kulifuatia Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa, kuomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hilo lijadiliwe na Bunge na kupendekeza kuwa Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe.

Bunge likubali kuivunja na kuiunda upya Kamati ya Nishati na Madini na kamati na baada ya hoja hiyo kuungwa mkono, Spika Makinda alisimama na kukubali hoja hiyo ya Kawawa na kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini.

Spika Makinda alisema ameiagiza Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi.

Baadaye Spika aliunda kamati ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ambayo Mwenyekiti wake ni Ngwilizi. Wajumbe wengine ni John Chiligati (Manyoni-CCM); Gosbert Blandes (Karagwe-CCM); Riziki Omary (Viti Maalum-CUF) na Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema).

Kitendo cha Sarah kuzungumza hadharani na kujitetea kimatafsiriwa kuwa ni kukiuka agizo la Bunge kwamba suala hilo lisijadiliwe na mtu au chombo chochote.

Wiki iliyopita Naibu Spika, Job Ndugai, alisema ripoti Ngwilizi itawasilishwa bungeni iwapo Spika ataridhika taarifa hiyo kutolewa ndani ya Bunge.

Alisema baada ya kukamlika kwa kazi hiyo, baadhi ya wananchi na wanasiasa wameanza kuizungumzia pamoja na vyombo vya habari kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo kinyume cha sheria na kuingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge.

Alisema sheria hiyo inamkataza mtu yoyote kuchambua na kuchapisha taarifa ya kamati kabla ya kuwasilisha bungeni.

“Natoa rai kwa umma kuwa tuache Bunge lifanye kazi yake kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni,” alisema Ndugai.

Ngwilizi naye aliwahi kusema kuzuia kujadili suala hilo hadi ripoti itakapowasilishwa bungeni.
Hadi jana wabunge hawakuelezwa chochote kama ripoti hiyo itawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano uanoendelea.

Hata hivyo, habari ambazo NIPASHE ilizipata, zinaeleza kuwa msimamo bado uko pale pale kwamba suala hilo litaamuliwa na Spika.

Kumekuwepo na taarifa kuwa huenda ripoti hiyo isijadiliwe bungeni kwa ajili ya kulinda heshima ya serikali.

Habari zinadai kuwa uamuzi huo unatokana na kuwepo kwa makundi mawili yanayokinzana. Kundi moja linalotaka ijadiliwe linataka ukweli wa tuhuma hizo ujulikane na haki itendeke kwa waliotuhumiwa.

Kundi linalotaka isijadiliwe ni lile linaloiunga mkono serikali ambalo linaona kuwa kujadiliwa kwake kunaweza kuwatia hatiani viongozi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini, Waziri Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi.

Vigogo hao wanadaiwa kuipatia Puma zabuni ya kuiizia serikali mafuta mazito ya muendesha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kwa upendeleo na kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.


.....anaonekana ni mama huruma sana huyu bibi...lkn akitaka aeleweke ktk heri na jamii masikini ya mtaani,
angeeleza pia ktkt hadhari hiyohiyo ni lini alishawahi kwenda kwa mkurugenzi yeyote wa shirika la umma kupigia debe kikundi cha ushirika wa ujasiriamali cha akina mama​
 
Hii nayo kali mbunge kugeuka kuwa messenger wa kufuata barua?hapo mbadoo tueleze vizuri
 
Lissu is smart guy, uwezo wake ni zaidi ya cabinet nzima ya JK pamoja na VP + Vasco

kaaaaa ama kweli kuna watu wazushi,mwakyembe ni smart mara 100 ya huyo lisu apo hujamgusa magufuli,Muhongo na ....,atawezaje kuizid cabinet,subiri ripot isomwe ndo utajua kitahomsibu na uzushi wake
 
kaaaaa ama kweli kuna watu wazushi,mwakyembe ni smart mara 100 ya huyo lisu apo hujamgusa magufuli,Muhongo na ....,atawezaje kuizid cabinet,subiri ripot isomwe ndo utajua kitahomsibu na uzushi wake
PhD, Prof za CCM? hazina maana, wote hao uliowataja ni wachumia tumbo, Mwakyembe is smart? subiri massacre hitokee kwa huo ukurupukaji wake wa Treni.
Magufuli ni smart? alishindwa nini kuachia ngazi, wakati Pinda alivyomkataza kusimamia sheria?
Muhungo?
 
Oh Tanzania! Yaani mfanyabiashara anamuomba mheshimiwa mbunge amchukulie mkataba wa kazi? Hapana si bure lazima kuna maslahi binafsi. Kwa nini asitume mwakilishi wa kampuni na kwa minajili hiyo kwa nini huyu mheshimika mbunge asiwe sehemu ya kampuni? Tafakari
 
Dada Sarah, mwogope Mungu, na uwaheshimu wananchi unaowatumikia waliokupa dhamana!

Pamoja na kuchemka hata katika hiyo 'story', bado inazidi kuprove kwa Sarah na akina Zitto kuwa Mhando alikuwa kiongozi mbovu maana swali ni kuwa, "Inakuaje Kampuni ishinde tenda na isitaarifiwe kwa muda mrefu na Mkurugenzi Mtendaji awe hana taarifa mpaka kufikia mteja aje kulalamikiwa na Mbunge! Yaani mnatufanya sote majuha? Kama Mhando angekuwa mchapa kazi kwa nini asiwe approachable or accessible easily na hawa ma-suppliers mpaka wafikie kuona kuwa hawana msaada kwake hadi kwenda kulalamika kwa Wabunge?


Hayo yote ni dibaji tu ku disqualify hiyo story ya kitoto ya Mbunge kufikia kujipendekeza kumbebea mkataba mteja anayeomba kusupply mali za mamilioni kama vile uongozi wa kampuni yake ungeshindwa kufika ofisi kuufuata na kupewa maagizo ya kiofisi yanayoendana na mkata huo.

Sarah kinachokusibu ni lile fuko la fedha ulilokuwa unatembeza ili kumtetea Eng. Mhando (alitekuwa wakala wa mafisadi TANESCO) na pia kututaka kupinga bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bila sababu yeyote ya msingi. Pili kumbuka kuwa deals zako zote za kibiashara ulizokuwa unafanya TANESCO sio siku moja tu watu wanazifahamu.

Kumbukumbu zote za kumtembelea Mhando na mawasiliano yenu tunayajua na watumishi wengi sana TANESCO wanakufahamu. Hata yule dada aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Mhando alishafikiwa na alitoa maelezo mazuri mengi ya kukumaliza kabisa ukiachilia mbali wasaidizi wa Mhando waliokuwa masoko na Wabunge wa kike uliwafuata na mazungumzo yako nao n.k. Fanyeni tu madudu yenu lakini msisahahu kuwa waaminifu katika umma na katika vyombo vya usalama wapo na hawatawavumilia hata chembe!

Aliyekushauri kwenda kwenye magazeti (staili ya rafiki yako Zitto) ndiye amekumaliza kabisa maana sasa hata kabla ya yote inatakiwa Spika wa Bunge akusogeze kwenye kamati ya Maadili kukujadili na kukupa adhabu unayostahili si kwa ajili ya sakata linalokuhusu juu ya rushwa na migongano ya kimaslahi bali la kudharau agizo la Spika kupitia kwa Naibu wake KUTOZUNGUMZA TAARIFA HIYO KABLA HAIJAPOKELEWA NA SPIKA. UMEONYESHA DHARAU KUBWA SANA KATIKA MAMLAKA YA BUNGE!:A S angry:

Tundu Lissu, Maswi, Muhongo, Simbachamwene na wengine wote waliopiga kelele juu ya hili sakata linalowahusu akina Sarah na Mhando wote walikuwa sahihi sana.

Baada ya Mhando, wewe Sarah unatakiwa uvuliwe uwanachama kutoka Chama chako ili iwe fundisho kwa Wabunge wanaokiuka maadili ya dhamana walizopewa. Kisha Maj. Gen. Mboma ondolewe haraka sana asiwe mwenyekiti wa Bodi hiyo maana naye ndiye mwenye biashara chafu na TANESCO na wala hana any added advantage katika kuiongoza Bodi kuelekea ufanisi kuliko watanzania maelfu wenye sifa zao tu na wanaoweza kuisimamia Bodi hiyo vyema zaidi kwa manufaa ya Watanzania.

Babykailama: Hapo penye kijani CCM haina dhamira wala ujasiri wa kuwaachisha uanachama wanachama au wabunge wala rushwa!!! Wataanzia wapi? Ni nani msafi ndani ya CCM? Hebu tujiulize ni kwa nini dhana ya kujivua gamba imekwama?? Nadhani ni kutokana na kuwa kila mwana CCM anajua kuwa hakuna aliye msafi hivyo hakuna mwenye haki ya kukemea rushwa!!! Ni jambo la ajabu mno chama maarufu kiasi hiki kuvunja katiba ya chama na katiba ya nchi na bado kung'ang'ania madaraka. What a shame!!!!!
 
Hili nalo ni tatizo..!! Tanzania, my motherland.. I love you so much..!
 
Bi Sarah angetusaidia hata mifano miwili ya ziada ya wananchi wengine aliowahi 'kufuatilia' matatizo yao kwa ukaribu huo. Ngoja na mie nimuombe mbunge wangu anipitishie barua yangu muhimi nyumbani, manake tunaishi jirani tu....ila sijui atakubali!
 
ccm ni kama akina msanja ukiashangaa hapa kesho unaona ni afadhari ya jana kweli mwaka huu tutaona ukilazi wahawa jamaa
 
Alichojieleza ruth msafiri amenikoroga na kujichanganya,
1. Amesema hausiki na hiyo kampuni bali aliombwa tu, aeleze kuna nini hapo katikati mpaka mwenye kampuni amuombe yeye?. Je kuombwa kwake hakutokani na ushawishi alionao yeye?.

2.amesema alipoitwa mwanasheria wa tanesco alikuja na bahasha ambayo baadae aliombwa aichukue muhusika ataikuta nyumbani, anasema hajui kkilichoandikwa ndani ya bahasha kwa kuwa hayamuhusu, kama yalikuwa hayamuhusu alifika vipi tanesco?.

3. Ninini kimemsibu mpaka jana kuibuka na kutoa habari za kujitetea?, imekuaje aje kujitetea siku moja baada ya taharifa ya kufukuzwa muhando?.
 
kaaaaa ama kweli kuna watu wazushi,mwakyembe ni smart mara 100 ya huyo lisu apo hujamgusa magufuli,Muhongo na ....,atawezaje kuizid cabinet,subiri ripot isomwe ndo utajua kitahomsibu na uzushi wake
*Mkuu wewe bado upo usingizini, toka lini kada wa CCM akawa smart. Haijarishi una degree ngapi ukiwa mwanaCCM wa leo ujue wewe ni zezeta tu.

*Mtu smart hawezi kuwa mwoga na mnafiki.
Mwakyembe, Magufuli, Muhongo, Sitta nk ni waoga na wanafiki wakubwa.

*Ndani ya CCM ya leo kigogo mmoja tu ndio ana dalili ndogo za kuwa smart naye ni EDWARD LOWASSA kwa kuwa sio mwoga sana wala sio mnafiki sana, yeye ni fisadi anajua hivyo na anasonga mbele kwa staili yake hiyo hiyo na hakuna anayemweza ndani ya CCM. Wengine wengi waliobaki ndani ya CCM ni kama mazezeta tu, yako pale kuburutwa na kulalamika vichochoroni.
 
Amezaa na mkubwa.

It's not secret Kiona na ndio sababu ya kuhongwa ubunge wa kuteuliwa.. Serikali ya kishkaji tu hii, no serious minds kila anayepata cheo anatazama wapi aingize serikali mkataba feki...
 
Last edited by a moderator:
mambo mengine hayahitaji hata elimu ya chekechea kubaini ukweli hapa maslahi lazima yatakuwepo anajaribu kuukimbia ukweli tu, ngoja tusubiri maamuzi ya madam spika na yeye kama hata amua kuilinda serikali isiaibike
 
Back
Top Bottom