Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) cha kwanza kitakachojengwa Wilaya ya Rorya.
Chuo hicho kitajengwa kwa awamu mbili ambapo kwa awamu ya kwanza ni ujenzi wa majengo 9.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amesema "Tunamshukuru Rais kwa kuwa mkombozi wa jamii ya Wanarorya kwani watapata ujuzi na ufundi utakaowasaidia kuajiriwa na kujiajiri, ndio maana nimeongoza mamia ya Wanarorya kushiriki shughuli za maendeleo kwa kuanza kuchimba misingi."
Aidha, DC Chikoka pia amempongeza Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Chege kwa kuendelea kusimamia ahadi zake kwa vitendo.