Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Daah pengine Joooh yuko zake kwa mama mwenyenyumba wanapiga story.Maana nlisikia wamepatana sisi tunasubiri.

Afu Kumbe mama mwenyenyumba haoni mbali bwana.ile tym jooh anaona anakaziwa macho kumbe mama mwenyenyumba anasikitika haoni mbali..Joooh alikuwa hajui hili ni agustino tu alikuwa anajua.

#ila nawaza tu vipi kama jooohs simu yake imedondoka bahati mbaya na tachi imeharibika inafanya kazi kwenye emoji tu.Wabongo nnavyowaelewa hata story ikihadisiwa kwa emoji wataelewa tu maneno wanaweka wenyewe
 
Daah pengine Joooh yuko zake kwa mama mwenyenyumba wanapiga story.Maana nlisikia wamepatana sisi tunasubiri.

Afu Kumbe mama mwenyenyumba haoni mbali bwana.ile tym jooh anaona anakaziwa macho kumbe mama mwenyenyumba anasikitika haoni mbali..Joooh alikuwa hajui hili ni agustino tu alikuwa anajua.

#ila nawaza tu vipi kama jooohs simu yake imedondoka bahati mbaya na tachi imeharibika inafanya kazi kwenye emoji tu.Wabongo nnavyowaelewa hata story ikihadisiwa kwa emoji wataelewa tu maneno wanaweka wenyewe
dah

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
tapatalk_1575240492055.gif


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaman kwan hamna kwingine mwenye idea ya udirector amalizie script...???

Ila joooh si atuambie tu kama tunakutana tena kwenye hiki kilinge saa 6 usiku tujue tu,mi tangu saa 10 nasoma comments tu story haiji dah...

1-Nataka nijue nani alicheka pale kwenye muembe
2-nguruwe yule aliletwa na nani?
3-mama mwenyenyumba anavuta?je kama havuti, mbona alikuwa hachezi mbali na mfanyabiashara Agustino mzee wa ATM

Joooh tunaapia tutakuwa tunalike saivi jamaa tudondoshee mambo mkali..
 
Hii story ukisoma ukiwa umetuliza akili haswa unaweza jikuta ww msomaji ndo unayedata mana heka heka ni nyingi na haina mapumziko , yani bandua tatizo ongeza tatizo, wacha mtu amiliki chochote kile sitamwonea wivu mana sijui kapitia mangapi ,

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
Hatari sana chief, pale kwenye damu pame nipelekesha acha tu. Nilicheka sana alipofikia stage ya kusema anaubeba mwili bila kujali nani anamuangalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oooky Inaendelea.........

Wakati bado naendelea kuugulia maumivu pale hostel nikacheki muda nikaona inaelekea saa 11 alfajiri nikatoka njee moja kwa moja nikaanza kuitafuta barabara kuu ili niweze kuwahi getto kwa agustino, njiani nilikuwa namawazo mengi kama mtu anaeenda kufata majibu ya HIV test basi nikaanza kupiga tambo kubwa kubwa hadi nikaanza kuona lile getto kwa mbali

Basi njiani nikawa najiuliza hivi nikapiga simu nikutana na kilio nitafanyaje? jee utajiri nitaupata au ndio itakuwa imekula kwangu nimekosa vyote baasi taratibu nikakaribia ile nyumba nikaanza kuusogelea ule mlango nikakuta umefungwa kwa njee basi nikafungua nikaingia ndani lakini niliona kama jamaa yangu agustino atakuwa hajarudi maana kila kitu tulichokiacha pale kuanzia simu ,Walet vilikuwa mezani

Basi nikawasha simu yangu huku nikiwa natetemeka sana nikaanza kutafuta jina la mama yangu ili nimpigiie simu bahati mbaya nilijibiwa mteja unaemtafuta hapatikani, kuna jirani ni msela wangu ikabidi nimpigie ila simu ilikuwa inaita
haipokelewi basi nikajaribu kutafuta baadhi ya ndugu nao wakipiga wanasema simu haipatikani daa nikaanza kuchanganyikiwa.

Basi wakati nimekaa pale nisijue la kufanya mara nikasikia simu yangu inaita asee niliirukia fasta utadhani kinyonga yuko mawindoni kushika nikakuta ni yule jamaa wa kitaa wakati huo simu ilikuwa inanipigia mlio wa batter low kila muda ,baada ya kupokea akaniambia nipige ikabidi nikate nikampigia kisha akaniambia shida nini asubuhi yote hii nikamwabia nenda fasta home unipe mama niongee nae kunajambo nataka kumueleza

Basi baada ya muda kama dakika kadhaa nikaanza kumpigia jamaa simu mfululizo huku nikimuuliza umefika umefika , baada ya muda kidogo ikaingia message kutoka kwa jamaa akaniambia nimefika ila nimekuta kuna tatizo asee nimemaliza kusoma tu ule ujumbe nilikuwa nimekaa kitandani ikabidi nijidondoshe pale chini nianze kujigaragaza huku nikipiga nduru za kufa mtu.

Nimelia weee hadi nikasikia mtu anagonga kwenye ule mlango kwa njee nikaamka kinyoge huku nikifuta machozi nikaenda kufungua mlango.

Nilipofungua nikakutana na mama mwenye nyumba uso kwa uso akaniambia kunataizo nikamwabia ndio ni mambo tu yakifamilia yataisha basi ikabidi nirudi ndani nikahisi joto linaongezeka nikavua suruali nikabaki na boksa na viatu tu miguuni .tshirt nikavua nikalala chali pale sakafuni nikachukua simu nikaanza tena kupiga kwa yule jamaa

Ile imetoa mlio wa kwanza wa pili ikazima nikatoa line nikaweka kwenye simu ya agustino kuwasha hata haikufika kuwaka ikazima jumla jumla hasira zikanipanda nikatamani hata nikate kichwa changu nitoke njee nikipige teke kiruke huko maana mawazo yalikuwa yamenizidi

Wakati nimendelea kuwaza pale chini nikasikia mlangoni kama mtu anagonga kwa njee nikaenda kufungua nikakuta ni agustino nikamwabia ulikuwa wapi toka jana akanimbia nilikuwa kule kule uliponiacha nikienda kwanza ni story ndefu

Basi akaanza kunieleza wakati tumeachana jana usiku yeye akielekea kwenye lile chaka lake kuchimba yale maharage kwa nyuma alianza kuona watu kama wanamfatilia yeye akajua ni yale majaribu yameanza kama yule jamaa aliyokuwa amemwambia alipata hofu kidogo lakini yeye aliendelea na safari yake baada ya kutembea kidogo kugeuka tena akaona wanazidi kumfatilia akasema akaanza kukimbia

Alikimbia sana hadi alipoangalia nyuma akaona hali ni Shwari sasa anasema alipofika kwenye eneo la tukio ndio akaanza kuona vitu vya ajabu kwani alipofika alitafuta mbegu bila mafaniko yoyote anasema alitafuta piga tochi huku na huku lakini hakuona kitu chochote basi akaniambia ikabidi alale pale chini huku akiendelea kutafakari

Baada kama ya dakika moja akashituka na kujikuta yuko pale pale barabarani tulipo achania halafu akawaona wale watu waliokuwa wanamfatilia bado wamesimama kwa mbali ilibidi aanze tena safari ya kuelekea kule ili haweze kuchuma mbegu kwani alijua ile ni ndoto aliniambia alitembea akatembea sana
mpaka kufika pale

Badala ya tafuta mbegu akakuta kunamiili ya watu wawili wako kama walivyozalia wamelala chali halafu majani makubwa ya miharage imeota juu ya vufua vyao akasema yeye alijua ni majaribu ya kijinga ikabidi asogee hivyo hivyo

Wakati anazidi kusogea alisikia kama kuna mtu anapiga hatua kutoka nyuma yake ndipo akaanza kumcharaza viboko vya kufa mtu mgongoni yeye hakujali ndipo akazidi kupiga hatua haraka haraka kuelekea kwenye ile miili huku akiendelea kupigwa bakola basi ile amefika karibu akashika yale majani mkono wa kulia na wakushoto akaanza kuvuta bila mafaniko alivuta sana sana lakini ikashindikana

Wakati huo ananiambia anazidi pigwa viboko ikabidi azidi kukomaa ile bado anaendele alishangaa kuona macho ya wale watu yanafunguka kuangalia vizuri anaona ni wazazi wake wakati huo hajafanikiwa kutoa zile mbegu basi kwa mshituko alioupata ikabidi akimbie kurudi getto alifanikiwa kufika ikabidi alale lakini cha ajabu kumekucha yuko ile ile sehemu aliyokuwa anafanyia tukio ndio ikabidi aanze tena safari upya kuja hapa nikamwabia lakini unauhakika kwamba wazazi wako ni wazima? Akaniambia hajui ikabidi na mimi nimueleze yalio nikuta

Nikamwabia tupeleke simi zipate moto halafu tupeleleze tujue maana mimi nilikuwa najua mama yangu tayari yamesha mkuta ya kumkuta basi tulitoka pale getto nikamwabia agustino mimi sasa hizo habari za mganga sizitaki kwa kweli
bora tutafute njia nyingine tuone tunafanyaje ikabidi anikubalie kwa shingo upande.

Baada ya kuacha simu kibandani ikabidi twende kwenye kimgahawa wakati tunakula kunajamaa alikuwa yuko pembeni yetu amechoka kweli anapiga story kwa kilugha ila tukaona kama anamtaja jina mama mwenye nyumba halafu wanatukodolea macho sisi ila hatukuelewa kitu chochote tuliondoka tukarudi getto ile tumefungua mlango tukakuta matone ya damu kama kuku ka katwa kichwa halafu akaachwa anaruka ruka mule ndani

Ikabidi agustino atoke njee akamuita mama mwenye nyumba yule mama kufika anasema eti haoni kiti na sisi kutaza vizuri tunaona nyumba iko safi

Wakati tunaendelea kujadiliana ile inama inuka kuangalia chemba nikaona kiganja cha mkono wa mtoto mdogo asee nikamwabia agustino tazama pale chini ananiambia wapi nambwambia angalia mkono ule anasema haoni ikabidi nizame ndani ya kitanda kwanda kushika chaa ajabu kile kimkono kikapotea

Nikamwabia bro leo nikitoka kuchukua simu sirudi tena getto hapa narudi zangu hosteli,nikamwabia tafuta chumba sehemu nyingine hatukumaliza muda mwingi tukarudi kufata simu kupiga kwa jamaa yangu akaniambia eti mama yako jana usiku saa saba alivamiwa na wezi akapigwa nusu afe yuko hospital kalazwa asee nikisikitika sana nilijua mimi ndio chanzo.

Hapo ndio nikajua kumbe walozi wengi wanaweza tengeneza tatizo wanavyotaka hata kusingizia mtu mauaji kichawi ili tu watimize malengo yao ,Agustino alipiga kwao lakini baba yake akamwabia leo nimekuota ndotoni pia leo leo umenipigia simu.

Nadhani ni mzazi alishindwa mwambia mwanae kuwa nimekuota vibaya siku hiyo hiyo nilienda pale nikachukua kila kilichochangu nikasepa kurudi shuleni, Agustino yale mauza uza yalimshinda ikabidi ahame ile nyumba ya yule mama wa kisukuma ilikuja kupigwa moto na raia wenye hasira kali wakimtuhumu kuwa anafuga watu ambao ni mabubu hawaongei

Kisha nikasikia story raia wanasema eti alikuwa anatumia viganja vya mikono ya watu kuwafanya raia ma bubu hata zile damu mule getto ilikuwa inatokana na miili ya vichanga .Kile kiganja akichukua sijui anafanya nini akikupiga nacho kofi hutoweza kuongea tena labda uzaliwe upya

Sasa wakati nimerudi naendelea na masomo agustino yeye aliendelea kusoma huku akiwa anapiga zile mishe zake za kusafirisha bangi kwa urafiki na mambo tuliyokua tumepitia nilikuwa nae bega kwa bega kumsindikiza kupeleka mzigo kwa wauzaji hata mzigo ukifika nilikuwa naenda kumpokea

Lakini siku za agustino kumbe zilikuwa zinahesabika tu mungu wangu..wahuni walikuwa wanamlia gepu kwamba anaharibu biashara yao huku yeye ni dogo tu wakuja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari sana chief, pale kwenye damu pame nipelekesha acha tu. Nilicheka sana alipofikia stage ya kusema anaubeba mwili bila kujali nani anamuangalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hujawahi pitia jambo gumu huwezi elewa yaani
Kuna muda wa kujilipua liwalo na liwe mana unakuwa mfu anayetembea wacha tu

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Back
Top Bottom