Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Oooky Inaendelea........

Bado nilikuwa pale getto nikitafakari nisijue nini cha kufanya ikabidi nichote kikombe kingine cha maji ili ni mwagie tena lakini hata nilipoweza fanya hivyo haikusaidia kitu chochote zaidi ya yale maji kuzidi loanisha mashuka.

Basi mimi kwa mawazo yangu nikajua huyu jamaa itakuwa tayari amesha fariki na kwa mazingira yale na ukaribu ule tuliokuwa nae ingeonekana msala wote unaniangukia mimi nikawaza nikimbie nikasema naweza sababisha tatizo lingine wanaweza sema jamaa kaua halafu kakimbia

Pia ni nani atanielewa hata kama nikieleza mbele ya vyombo vya sheria eti tuliweza fanya mambo yote yale tukiwa pamoja nani atanielewa yaani mawazo mengi yaliniijia kichwani nisijue nini cha kufanya. Pia nikiangalia na zile damu kwenye shuka na chini ya uvungu ndio nikasema hapa nimekwisha hii ni kesi ya mauwaji kabisa.

Nilichokifanya nilimbeba agustino nikamuweka chini halafu nikatoa tshirt aliokuwa ameivaa ya rangi ya blue kisha nikamvua viatu alikuwa na viatu vikubwa vya wafanyakazi wa migodini kisha nikatoa yale mashuka yote kwenye kitanda yaliyokuwa yametapakaa damu.

Ndipo nikaangalia vizuri hadi kwenye cover la godoro kulikuwa kuna michirizo ya damu iliyokuwa imepenyeza kwenye shuka hadi kufika kwenye godoro basi nikayaweka kwenye ndoo halafu pia nikaweka na ile tshirt yake nikaanza kusugua cover la godoro kwa dodoki la kuogea

Kisha nikamchukua agustino nikamrudisha kwenye kitanda baadae nikaanza kupiga deki mule ndani piga kila sehemu sugua kila kitu huo huo usiki nikafua mashuka nikayaanika kisha nikarudi mule ndani . Ilibidi nikae chini nianze kujiuliza hivi agustino atakuwa amefariki kweli ndani ya moyo wangu nilikuwa nasema hapana na kama mtu aliyetufanyia hii mikosi sio mwingine atakuwa ni yule mganga maana ule mtaa wote tulikuwa hatuna bifu na mtu.

Ilibidi niwaze tena au ni huyu mama mwenye nyumba maana yeye ikifika saa moja tu tayari ameshajifungia ndani nyumba yake ilikuwa ya ndani kwa ndani na geti kubwa sisi wapangaji ndio tunaishi njee kwenye chumba ambacho jambazi akipiga mlango teke moja tu amekufikia

Lakini sikuwa na uhakika wowote hata siku ile amemtokea agustino kule nyuma ya nyumba nikasikia anakimbia. agustino baada ya kurudi asubuhi aliniambia kuwa hakusikia geti kama limefumguliwa maana lile geti mama mwenye nyumba akifungua hadi mtaa wa pili wanasikia

Basi nikasema ngoja nimtafute yule jamaa wa shinyanga nimwambie hali halisi maana nilijua fika wenyewe wanaweza nisaidia kutatua tatizo daa kushika simu ya agustino sikuona namba hata moja hapo ndio nikachoka nikajua hapa ni ushirikina moja kwa moja nikatoa line yake nikaweka kwenye simu yangu zote zikasoma emergency call .

Hapo nikasema daa mimi jooohs leo nimekamatika siku zote ndege mjanja hunaswa kwenye tundu bovu nilibaki pale chini hadi nikasikia kunaenda pambazuka kuku wanaanza kuwika basi nikaamka fasta pale nilipokuwa nimekaa nikaenda kumuamsha agustino kwa mara nyingine lakini alikuwa kama mtu aliyepooza hapumui wala nini.

Basi nikatoka njee kwenda kukojoa wakati narudi kuangalia yale mashuka pale njee yana alama za damu nikama sikuzifua vizuri basi ikabidi nizianue fasta hivyo hivyo mbichi nikaziingiza ndani nikaziweka kwenye kamba iliyokuwa juu ya dirisha .

Ikabidi nitoke njee nikafunga mlango na kufuli halafu nikatoka njee nikiwa nimemuacha agustino mule ndani nikasema ngoja niangalie usawa wa msosi maana nilikuwa nasikia njaa ya kufa mtu wakati bado nawaza kushika mfukoni sina kitu hata mia mbovu

Ikabidi nirudi getto pale kuchukua nilifungua mlango nikaanza kutafuta wapi nilikuwa nimeweka hela zangu daa sizioni nikapiga mahesabu nikasema jamaa agustino huwa anawaleti tafuta nikaikosa nilikuwa nimemlaza chali ikabidi nimgeuze bado sikuona Walet daa nikasema hapa sijui nifanye nini ikabidi nikae pale chini nikasema niende wapi mimi

Baada ya dakika chache nikasema ngoja nikamtafute kunajamaa alikuwa mshikaji wetu sana alikuwa ni mpishi kwenye ile shule tuliokuwa tunasoma maana tulikuwa tunamsaidia sana na bangi akiwa na uhitaji basi nikamuacha agustino mule ndani nikafunga mlango nikaondoka kuelekea shuleni kumbuka hiyo wiki wanafunzi wameanza kuripoti shule wale kina john visomo

Nilipita pale njia panda nikaona baadhi ya wanafunzi wako kwenye kile kimgahawa wamapiga chai nikapitiliza huku nikitazama mifupa ya wale kuku tulio watupa pale ilivyotapakaa na kuharibika sana kwenye ile bara bara

Basi mimi nikapita tu kama sifahamu kinachoendelea huku moyo wangu ukiwa unaenda mbio hadi mdundo wa mapigo ya moyo nikawa nausikia masikioni niliteremka na barabara hadi nikafika shuleni nikawa naona kwa mbali wenzagu na baadhi ya kidato cha sita wakiwa wanapiga msuli, wengine wanapigiana table teaching daa nikasema mtaka vyote mkosa vyote ndio nisha feli hivyo

Bila kupoteza muda nikapita moja kwa moja hadi jikoni nikamkuta mpishi anahangaika na kuongeza magogo ndani ya jiko huku uji wa mahindi ukiwa unatokota mdogo mdogo ndani ya sufuria basi alivyoniona tukapeana salamu kitu cha kwanza akaniuliza agustino yuko wapi nikamwabia alienda kufata mzigo bado hajarudi maana hiyo ishu ya bangi yule mpishi alikuwa anahijua before hata mimi sijaijua.

Nikamwabia anisaidie kwanza bangi kweli alinipatia kakipisi kadogo nikasogea chemba nikaanza kupuliza baada ya kumaliza wazo likaniijia ebu mwambie huyu mpishi jambo lililomkuta agustino ikabidi niinuke nilipokuwa nimejibanza nikaanza kumfata kule jikoni baada ya kufika nikamwabia nisaidia uji ikabidi achote animiminie kwenye sahani ya plastiki nilikunywa uji mpaka jamaa akabaki anashangaa

Nilipomaliza wazo lingine likakiambia ondoka ila nilimwabia nitarudi jioni kuna mishe nataka tuongee basi nikaondoka kurudi getto hapo mawazo ya kumtoa agustino mule ndani na kumpeleka popote yakanza kuniingia nadhani labda ni kile kibangi nilichokuwa nimevuta wakati natembea kurudi getto nikaanza kupepesa macho ni chaka gani zuri la kwenda kuutupa ule mwili halafu ikiwezekana nikatoe taarifa za kupotea kwake

Nilifikiria nikaona hilo litakuwa wazo zuri wakati nafika pale getto nikamkuta mama mwenye nyumba amekaa njee anatwanga kitu kwenye kinu nikamsalimia hakuitikia nikasema potelea mbali nikaingia na kufungua mlango

Ile nimeingia tu nikakaribishwa na michirizi ya damu kibao pale chini nikaingia ndani fasta nikajifungia kumcheki agustino hana hata dalili ya kuamka nikasema leo usiku ikiwezekana nimbebe nimtupe mahali maana akianza kunuka hapa itakuwa noma kushika simu haina chaji tafuta pesa mule ndani sioni kitu .nikasema nitafanya nini jasho likaanza kunitoka ,nikahisi kuchanganyikiwa nahisi kulia lakini kwa mawazo niliyokuwa nayo hata ningelia isinge saidia kitu

Ilibidi nivue shati nikabaki kifua wazi nikalala pale chini sakafuni huku nikiendelea kujiuliza hizi damu nani anazileta humu ndani nilitamani nitukane matusi ya nguvu ili yule mama hasikie lakini ilibidi nitulie tu

Nililala pale mpaka kwenye majira ya saa kumi hadi nikaanza kuota mpango wa mganga ilifanikiwa tunafanya matanuzi wewe weweee nilikuja kuamshwa pale chini na njaa ya kufa mtu nilivyoamka nikasimama nikaenda kuanza kumchunguza agustino nikaona kweli jamaa amefariki ikabidi nianze kutest kama naweza kumbeba daa alikuwa mzito balaa.

Kisha nikatoka njee nikafata dekio nikaanza kufuta zile damu pale baada ya hapo nikaenda moja kwa moja hadi shuleni hiyo jioni tulipiga story na mpishi huku nikitaka kumueleza shida yangu lakini moyo ulikuwa unasita nilichumguza marafiki pale shuleni kama muddy atakuwa kasha fika lakini niliambulia patupu sasa baada ya kula ikabidi niondoke nikasema leo lazima usiku totoro nitoe ule mwili pale ndani halafu asubuhi nianze gia za kumtafuta

Njiani nilikiwa nimechanganyikiwa kabisa yaani sura yangu ilikuwa inaonesha huyu mtu amekata tamaa yaani nilikuwa nimebaki kama puto muda wowote ule naweza pasuka nilitamani niende hata kwa yule babu anipatie bangi niondoe mawazo lakini nilijua mzigo hana lakini nikasema haina shida nitapiga tu free style

Nilirudi kufungua getto nilikuta kama mwili wajamaa unaanza kama kuharibika huku nikajaribu kiugeuza mwili mgongoni alikuwa kama anavuja damu

Daa nikasema leo sita lala hapa naondoka na mwili halafu nachukua kila kilicho changu nasepa basi nikaendelea kukaa pale chini hadi muda kama saa 6 hivi usiku

Nikavua shati niliokuwanayo nikavua suruari kulikuwa na bukta ya jinsi nikavaa nikachukua vile viatu vya mpira nikavaa kisha nikachukua ule mwili nikauweka chini. Kisha nikasema ngoja nitoke njee nizuge kama naenda chooni nisome mazingira ya kumtoa mwana mule ndani .

Nikafungua mlango taratibu kisha nikatoka njee nikiwa kifua wazi basi nikaenda chooni wakati narudi kupiga chabo kwenye geti la mama mwenye nyumba naona yuko kwa ndani amesimama anachungulia yaani alikuwa amefungua mlango wa mbao kwa ndani ananichungulia kwenye nondo za urembo zilizokuwa juu ya geti .

Basi nikazuga narudi kulala ila nikasema lazima ule mwili utoke mule ndani usiku ule ule





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah..kunakoeleeka huko kutamu..we jamaa andika hata usiogope au kutuhurumia wasomaji..usiruke kipengele..

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii stori inafundisha sana, kwa kijana aliyekata tamaa ya maisha katika utafutaji wa pesa halafu ana mawazo ya kwenda kwa mganga kutafuta utajiri stori hii itabadili mtazamo wake, haya mateso waliopata jamaa makubwa sana, mwisho wa siku Rafiki ameng'ata godoro huku jamaa mbegu zimepotea. Dah

Bora hiyo kazi ya kupanda mbegu wangemalizia kwa mganga maeneo yaleyale. Iwe rahisi kupata assistance ya mganga

Sent using Fly in any Weather.
Ooops kumbe imeishaaa..!??

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani m mvivu wa kusoma hadith hii umetisha,na yule jamaa alielezea alivyokutana na mke wake mmetisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Karibu inaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom